Yaya aliyemtesa mtoto Uganda aomba msamaha

Yaya aliyemtesa mtoto Uganda aomba msamaha

Anayeweza kusema anamsamehe ni yule mtoto aliyeteswa.
Mimi ningekuwa ndio mzazi wa yule mtoto nadhani ni mimi ambae ningekuwa kizimbani leo kwa kesi tofauti kabisa...
 
  • Thanks
Reactions: kui
Afunge huyo dada roho mbaya al shabab wana afadhari sababu wanaua watu wazima. Video hile inatisha.mie wanangu walishindwa kuiona bali waliishia kulia tu. Pamoja na kifungo anatakiwa kuombea atokwe pepo chafu

Duh!, mkuu ulionyesha watoto?
 
Mimi ningekuwa ndio mzazi wa yule mtoto nadhani ni mimi ambae ningekuwa kizimbani leo kwa kesi tofauti kabisa...

Mkuu kama mie, mpaka naogopa!, this Monster needs both a fine, and rot in jail!
 
Sijui amefikiria iwapo mtoto angepoteza maisha ingekuaje au yule mtoto akionyeshwa ile video kweli atamsamehe. Nafiri angepimwa kwanza kama yuko vizuri kichwani nina mashaka nae huenda anatatizo la akili.
 
Usilete reference ya vitabu vya dini. Mungu anakusamehe lakini anakurudi. Unajua daudi alimwibia uriya mke. Pamoja na toba haswa lakini mwanae daudi alikufa. Asamehewe, afungwe ili akili ikae sawa
Lakini ms chaga tukija kwenye vitabu vya dini anayeomba msamaha anapaswa kusamehewa embu tujiulize ni mangapi sisi tuliomkosea muumba na je kama yeye angekuwa na moyo mgumu wa kutosamehe unafikiri kuna mtu angebaki leo hii?
 
Kumbe ana akili timamu? Me nilijua kwa kitendo kile hayuko timamu. Anapaswa kupewa adhabu kali alichokifanya si ubinaadamu kabisa.
 
Sijui amefikiria iwapo mtoto angepoteza maisha ingekuaje au yule mtoto akionyeshwa ile video kweli atamsamehe. Nafiri angepimwa kwanza kama yuko vizuri kichwani nina mashaka nae huenda anatatizo la akili.

Hata mimi nahisi akili zake haziko sawa.

Angekuwa yuko majuu nadhani mahakama ingeamuru achunguzwe afya ya akili yake (sijui kama hiyo mahakama ya Uganda imeamuru hivyo).
 
Ila ile video ilikuwa wake up call kwa wazazi wachunguze watoto wanabakije nyumbani?
 
Pumbavu huyo afungweee faini ya dola mia 400 kama laki 6 na ucheee anaweza kulipiwa
 
M bona mzuri wa sura hivyo? Atakuwa anatumia huhuo urithi wa bibi umwokoe.
Majakazi yana roho ya shetani. Hawafai.
 
Mimi kama ndo baba wa yule mtoto namuombea asifungwe ili nimuue mwenyewe
 
141208112849_uganda__640x360_bbc_nocredit.jpg

Jolly Tumuhirwe

Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.

Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto

Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.

Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.

Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.

CHANZO: BBC


Dada mzuri kweli!!asamehewe tu huyu mrembo nimchukue.
 
Afungwe miaka 15 tu,dola 400 kitu gani kwa mateso aliyoyapata mtoto.
 
Naomba kusaidiwa na wana sheria hiv mtu akikiri kosa na hajaisumbua mahakama adhabu yake inapungua, inaondolewa au unabaki pale pale? Naomba pia wakati unanisadia zingatia kosa la mhusika na alietendewa kosa.
 
Wagura kenya:adhabu kali ichukuliwe iwe fuzo kwa wengine..sisi twajua hayo 2 ya video, na je? Mtoto angesema mateso aliopitia
 
msamaha utakaomfaa ni kifungo tu ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo, ule sio ubinadamu hata kidogo kumtesa mtoto mdogo vile hata kama sio wako.
Wazazi wamsamehe,ila waiache dola ifanye kazi yao!Miss u sana!
 
Back
Top Bottom