Prince Kunta
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 22,869
- 29,057
Mshana jr katika ubora wake
View attachment 333904
Hakuna kazi inayokosa changamoto, hata uwe mwerevu na mahiri vipi lakini lazima tu utakutana na kisiki
Waganga wa kienyeji nao hawajapona kwenye hili wengi walishapitia na majanga makubwa tu
Ukiacha yale ya kitapeli wa na wateja au kuua wa live au kupokea kichapo lakini vile vile kuna majanga kama haya
-kumchinja kuku kisha asife bali asimane bila kichwa
-kumchinja kuku kisha asitoke tone la damu
-kupasua nazi ikatae kabisa kupasuk
-kupika nyama isiive kabisa nk nk
Kuna baadhi ya waganga huwakataa wateja...kwakuwa wanajua huu ni mtego, kwenye ulimwengu wa roho ulimwengu wa giza kuna kujaribiana na kuoneshana nani zaidi
Zipo njia nyingi tu za mapambano ya aina hiyo na hii hutokea zaidi mmoja akiwa mahiri zaidi ya wengine au mmoja akijifanya mjuzi sana na kutambia wengine
Unaposikia mganga kafa kaugua au kapatwa na dhahama yoyote mara nyingi huyo kajaribiwa na wenzake.
Akipambana akashinda cheo huongezeka akipambana akashindwa lakini akaokoka na kifo aidha huacha kabisa uganga na kumrudia Mungu au hurudi kujipanga upya...sio wote wanaoacha uganga na kuokoka hufanya hivyo kwa ridhaa
![]()
Teh teh wewe mshana ahhhh nitaanza kukuogopa sasa,Kila aliyenijaribu alidondoka
Hii kazi Ni hatari sana! Bora nirisk Maisha yangu Kwa kuendesha bus Za dar mwanza kuliko hii! Hapana Aisee, one mistake, GONE!Mkuu jichawi unalosema kweli japo mimi siyo mganga ila niliwahi kutana na kitu kama chako.
Mwaka 2009, nilienda mtembelea binamu yangu alikuwa kaolewa na mganga. Mimi ndipo nilikuwa nimeingia kidato cha tano, wao walikuwa wanaishi maeneo ya nyaishozi huko tegeta.
Wakati niko pale akaja baba mmoja na mkewe wakasema mtoto wao wa kike anaumwa sana anahitaji matibabu ya haraka sana.
Yule mme wa jirani yangu akawambia sasa mbona mgonjwa hamkumleta, wakamwambia ataletwa jioni. Akawambia nenda nielekezeni mnapoishi nitakuja nimwone kwanza huko huko.
Wakamuelekeza kumbe walikuwa wanaishi sehemu siyo mbali na hapo, walipoondoka baadae mme wa binamu yangu akaniomba nimsindikize akamwone huyo mgonjwa.
Tulipofika kweli tulimkuta mdada anaomwa kakonda kweli yani alikuwa katika hali mbaya sana kakonda kweli na mbaya zaidi alikuwa na mtoto mdogo.
Akawatajia vifaa halafu tukaondoka. Ajabu kesho yake nikamuuliza mbona yule mgonjwa hakuletwa, akanijibu usiku alifuatwa na mama yake akamwambia yule ni mwanaye anataka mtoa kama nyama kwenye mambo yao. Alikuja tu kwa shinikizo la baba mme wake.
Na nilikuja ambiwa kuwa yule dada alifariki.
Hapo hapo akanisimulia tukio lingine kuwa aliwahi letewa mgonjwa anaumwa sana aliletwa na mkewe.(yani mke alimleta mmewe)
Akakaa naye pale siku tatu anamtibu pale, siku ya ijumaa akaamka kama kachanganyikiwa akaanza gawa nguo vitu vyake kwa wanaye, analipa madeni na kila kitu.
Mara sauti ikawa inamwambia kimbia kabla hazana haijaita uwahi kwa baba yake huyo mgonjwa ukamuone.
Anadai akachukua baiskeli bila kuga mtu mpaka kwa baba yake huyo mgonjwa alipofika akamkuta mzee yuko nje anafanya usafi. Akakaribishwa ndani na huyo mzee, mzee akamwambia si unajifanya kidume sasa tutaona kati yangu mimi na wewe nani zaidi.
Mara eti akamuona yule mgonjwa aliyemuacha kwake anamtibia kaja na glass ya maji akamletea mzee akamwambia pokea, jamaa akapokea akamwambia chagua kati ya kunywa yote na kunywa nusu.
Jamaa akanywa yote, akamwambia bahati yako haya nenda..
Alipofika akamwambia mke wa jamaa mgonjwa kanishinda kumbe baba yake jamaa ndiye alikuwa anataka mchukua mwanae msukule kwa ajili ya biashara zake. Na kesho yake akapata taarifa kuwa mgonjwa kafariki.
Laito yale maji angekunywa nusu naye angekufa.
Aiseee, pole sana Mkuu! Kwahiyo asubuhi mtu mzima ukaondoka Au uliwajulisha wenyewe kwamba hili zoezi haliwezekani?Kwa kuwa nilikuwa miaka mingi ndani ya hizi shughuli hivyo hata visa nilivyopitia ni vingi kiasi kwamba siwezi kusema hiki ni kizito zaidi, ila tu kila jaribu linalokuja ukifanya mistake tu ni kifo.
Miaka ya nyuma niliwahi kuitwa Dar es salaam maeneo ya chang'ombe ya sokota, hapo palikuwa na nyumba nzito hapalaliki wala hapashindiki.
Nyumba ilitawaliwa na madhara ya aina mbili, madhara ya moja kwa moja na yale ya vitimbi.
Madhara ya moja kwa moja ni kwamba kila wakiamka walikuwa wanaumwa nyumba nzima na wakienda hospital vipimo havionyeshi maradhi.
Vitimbi ni kwamba wakati mwengine wanakuta damu milangoni, mara usiku wanasikia kama mtu anatembea, mda mwengine mabomba yanafunguliwa usiku bila kujua nani anafungua, mara bulb zinaungua kwa mpigo na fundi akiangalia mifumo ya umeme ipo sawa.
Ni nyumba ya kisasa na hata wenyewe walikuwa ni watu wenye uwezo kipesa na pia mume ni kiongozi wa dini fulani, lakini yote waliyojaribu bado mateso yaliendelea.
Nilifika pale muda wa mchana na nikakuta nilivyoagiza vyote vimeshanunuliwa ila nikawaambia kazi itaanza kesho, tukakubaliana na nikalala pale.
Katikati ya usiku uliwaka mwanga wa ajabu katika chumba nilicholala na ukapiga upepo mkali kama nipo baharini, ghafla nikaona kiumbe kimoja ambacho sijakiona tangu nizaliwe.
Alikuwa na umbo kubwa kama tembo, alikuwa na manyoya mengi kama sokwe, alikuwa na macho mekundu kama damu, na alikuwa na kucha ndefu za kuogofya huku amesimama na miguu miwili mithili ya binadamu.
Akatoa kauli yenye mwangwi na kuniambia nimetumwa kuwatesa hawa watu na kisha kuwaangamiza, umeingilia kazi yangu hivyo usijaribu kabisa kupambana nami kwa usalama wako....asubuhi uondoke haraka.
Mpaka nimeweza kuhimili yote hayo ni sababu nilikuwa na vyombo vizito vinginevyo zile ishara za mwanzo tu pengine ningezimia.
KUNA MENGI NYUMA YA PAZIA TUSIYO YAFAHAMU NA MDA MWENGINE TUKIANGAMIA KATIKA HAYO.......MUNGU AMETAKA TUMUABUDU KWA DHATI ILI TUISHINDE VITA HII MAANA ANAJUA DUNIA INA MASHAKA
Changamoto nyingine in hiiDada embu njoopande hizi fasta, Kuna ujumbe mwingine hukuuu
Daah mkuu jichawi kweli umepitia mengi!!Kwa kuwa nilikuwa miaka mingi ndani ya hizi shughuli hivyo hata visa nilivyopitia ni vingi kiasi kwamba siwezi kusema hiki ni kizito zaidi, ila tu kila jaribu linalokuja ukifanya mistake tu ni kifo.
Miaka ya nyuma niliwahi kuitwa Dar es salaam maeneo ya chang'ombe ya sokota, hapo palikuwa na nyumba nzito hapalaliki wala hapashindiki.
Nyumba ilitawaliwa na madhara ya aina mbili, madhara ya moja kwa moja na yale ya vitimbi.
Madhara ya moja kwa moja ni kwamba kila wakiamka walikuwa wanaumwa nyumba nzima na wakienda hospital vipimo havionyeshi maradhi.
Vitimbi ni kwamba wakati mwengine wanakuta damu milangoni, mara usiku wanasikia kama mtu anatembea, mda mwengine mabomba yanafunguliwa usiku bila kujua nani anafungua, mara bulb zinaungua kwa mpigo na fundi akiangalia mifumo ya umeme ipo sawa.
Ni nyumba ya kisasa na hata wenyewe walikuwa ni watu wenye uwezo kipesa na pia mume ni kiongozi wa dini fulani, lakini yote waliyojaribu bado mateso yaliendelea.
Nilifika pale muda wa mchana na nikakuta nilivyoagiza vyote vimeshanunuliwa ila nikawaambia kazi itaanza kesho, tukakubaliana na nikalala pale.
Katikati ya usiku uliwaka mwanga wa ajabu katika chumba nilicholala na ukapiga upepo mkali kama nipo baharini, ghafla nikaona kiumbe kimoja ambacho sijakiona tangu nizaliwe.
Alikuwa na umbo kubwa kama tembo, alikuwa na manyoya mengi kama sokwe, alikuwa na macho mekundu kama damu, na alikuwa na kucha ndefu za kuogofya huku amesimama na miguu miwili mithili ya binadamu.
Akatoa kauli yenye mwangwi na kuniambia nimetumwa kuwatesa hawa watu na kisha kuwaangamiza, umeingilia kazi yangu hivyo usijaribu kabisa kupambana nami kwa usalama wako....asubuhi uondoke haraka.
Mpaka nimeweza kuhimili yote hayo ni sababu nilikuwa na vyombo vizito vinginevyo zile ishara za mwanzo tu pengine ningezimia.
KUNA MENGI NYUMA YA PAZIA TUSIYO YAFAHAMU NA MDA MWENGINE TUKIANGAMIA KATIKA HAYO.......MUNGU AMETAKA TUMUABUDU KWA DHATI ILI TUISHINDE VITA HII MAANA ANAJUA DUNIA INA MASHAKA
Hii Ni hatari sana! Hii Dunia tuonAvyo sivyo ilivyo!Sikuondoka mkuu
Kwa kuwa nilikuwa na jina kubwa ndani ya hizi kazi na pia nilikuwa nafuga majini wengi na wakali zaidi yake hivyo niliamua kucheza mchezo wa pata potea, zake zangu na nahisi mori na ujasiri ulionifanya niifanye kazi ile umetokana na majini nilionao hawakukubali kushindwa.
Asubuhi nilifanya kazi kwa misukosuko na akaangushwa pale pale dada wa kiarabu ambae ndie mke wa mwenye nyumba.
Ni lile jini makata liliamua liondoke na yeyote na kwa kuwa nilikuwa na mkoba mzima hapakuharibika kitu, nikamuwahi na kazi ikamalizika salama na mambo yakawa shwari mpaka leo.
Wengi wakisikia waganga neno linalowajia ni upigaji sababu ya hawa waliobandika mabango kila kona mijini, mkuu ukimuona mtu anaulilia uganga muhurumie sana
Mkuu tangu mganga asaidie kurejesha SIMU niliyoibiwa ndiyo siku niliyoamini nguvu za Giza zipoSikuondoka mkuu
Kwa kuwa nilikuwa na jina kubwa ndani ya hizi kazi na pia nilikuwa nafuga majini wengi na wakali zaidi yake hivyo niliamua kucheza mchezo wa pata potea, zake zangu na nahisi mori na ujasiri ulionifanya niifanye kazi ile umetokana na majini nilionao hawakukubali kushindwa.
Asubuhi nilifanya kazi kwa misukosuko na akaangushwa pale pale dada wa kiarabu ambae ndie mke wa mwenye nyumba.
Ni lile jini makata liliamua liondoke na yeyote na kwa kuwa nilikuwa na mkoba mzima hapakuharibika kitu, nikamuwahi na kazi ikamalizika salama na mambo yakawa shwari mpaka leo.
Wengi wakisikia waganga neno linalowajia ni upigaji sababu ya hawa waliobandika mabango kila kona mijini, mkuu ukimuona mtu anaulilia uganga muhurumie sana
Mshana kweli uko kikazi, swali lako la kwanza ni mgawo wa mapato?[emoji134] [emoji23] [emoji134] [emoji15] mgao wa mapato utakuwaje?