Mambo haya ni kweli kabisa na ndio kipimo cha uganga kwenye miji ya watu, wengi unapozungumziwa uganga wanadhani ni kitu cha mchezo......wapo waliokataa kazi hizi kwa sababu tu ya kuogopa mitihani yake.
Na wakati mtu anakabidhiwa uganga (ule halisi na sio matapeli) huwa anaaswa sana juu ya vita za kazi hizi na kwamba asijionyeshe wala kujinasibu kwa watu bali atulie na kufanya tiba.
Vijana wengi waliovamia hizi kazi na kisha kwenda katika miji ya watu walipata mitihani na hata kufa
Unaweza agiza kuku ukaletewa bundi na ukimchinja umekwenda na maji, hapa ukikutana na bingwa anatoa fimbo yake na kumgusa kisha anageuka bundi, anakwambia michezo yako nimeiona subiri zamu yangu.
Unaweza agiza mbuzi ukaletewa fisi
Unaweza letewa mtoto umtibu kumbe ni kinu, ukimchanja kwa lengo la kumpaka dawa umekwenda na maji.
Hapa nina mikasa mingi niliyopitia wakati nipo huko miaka hiyo, ila tu nitaelezea mmoja kifupi tu.
Nilishawahi letewa binti mmoja nimtibu ila tukapanga nishughulike siku nyingine, cha ajabu jioni ya siku ile akaja bibi mmoja ambae ni mama wa yule mgonjwa na kuniambia hivi "baba nakuomba yule mwanangu usimuague maana nataka kumtoa kikoa nadaiwa nyama katika ugoma wetu wa usiku, hivyo mkuu kanikomalia nimtoe mwanangu sasa baba usithubutu kunirudisha nyuma mwache kama alivyo.....kesho nitamwambia wewe haupo umesafiri.
Hakika ni kazi zenye mitihani, dhoruba, majaribu na kila aina ya vituko
Namshukuru Mungu leo hii sipo huko.