Waganga wa kienyeji jihadharini

Waganga wa kienyeji jihadharini

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,343
Reaction score
859,913
Nilikuwa mmoja wenu nikafika level za juu.. Haikuwa rahisi nilikwepa mitego mingi na kuzishinda changamoto nyingi

Kuna jambo jipya kiasi linajiinua kwa kasi ya ajabu.. Mnahusishwa na mauaji yanayoendelea nchini..

Je mnahusika kweli?

Je mnageuzwa mbuzi wa kafara?
Mauaji ya Katibuni

1. Yule producer aliyeuliwa na mpenzi wake sangoma wa kike
2. Temba aliyetenganishwa kichwa na kiwiliwili.. Kichwa kimepatikana kwa mganga
3. Mfanyabiashara wa Arusha.. Kifo chake kimehusishwa na uganga/mganga

Kuna chama cha waganga wa asili Tanganyika chenye usajili kabisa.. Kinatoa vyeti rasmi kwa wanaokidhi vigezo
Sasa kwenye haya yanayoendelea nchini mbona kiko kimya?
Kijitokeze kitoe tamko. Kiseme neno..! Haki itendeke

Anayehusishwa na ujinga achukuliwe hatua kali ikiwemo kufutiwa usajili... Anayetuhumiwa tu ama kugeuzwa mbuzi wa kafara naye atendewe haki pia...

Mwisho wa siku sote sisi ni watanganyika wengine ni wakuja na wengine ni kenge kwenye msafara wa mamba
1778914923206.jpg
1778914929177.jpg
 
Mbona mimi ni mganga na sina ushirikina huo? Natibu magonjwa pamoja na utajiri ila sifanyi makafara na ramli chonganishi. Nitoe rai kwa waganga wenzangu,kwanza tuachane na ramli chonganishi na ramli zozote zile pia tuache kutoa masharti ambayo yatapelekea kutendeka kwa ukatili na mauaji. Tujikite katika kutoa tiba mbadala. Karibuni kilingeni natoa utajiri bila kafara ya aina yeyote. Kianzio uje na laki na hamsini.
 
Mbona mimi ni mganga na sina ushirikina huo? Natibu magonjwa pamoja na utajiri ila sifanyi makafara na ramli chonganishi. Nitoe rai kwa waganga wenzangu,kwanza tuachane na ramli chonganishi na ramli zozote zile pia tuache kutoa masharti ambayo yatapelekea kutendeka kwa ukatili na mauaji. Tujikite katika kutoa tiba mbadala. Karibuni kilingeni natoa utajiri bila kafara ya aina yeyote. Kianzio uje na laki na hamsini.
hapa hakuna mganga.Mganga anayetanguliza hela hyo hafai.
 
Uganga jau sana, nasikia wana chama chao kabisa bongo hii. 😁
Chama kikuu kinachowaunganisha waganga wa jadi nchini ni Chama cha Waganga wa Tiba Asilia na Wakunga wa Jadi Tanzania, kinachojulikana kwa kifupi kama CHAWATIATA.

Chama hiki hufanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Afya pamoja na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala. Lengo lao kuu ni kusimamia na kuratibu shughuli za waganga wa kienyeji na wakunga wa jadi nchini kote.

Majukumu makuu ya CHAWATIATA

Kuhakiki wanachama:
Kusajili na kukagua waganga ili kubaini wanaokidhi vigezo vya kutoa huduma.

Kutokomeza matapeli:
Kuendesha misako dhidi ya watu wanaojifanya waganga (waganga feki) ili kulinda usalama wa wananchi.

Kudhibiti ukatili:
Kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya waganga wadanganyifu kwa kisingizio cha matibabu.

Kulinda amani:
Kupiga marufuku upigaji wa ramli chonganishi unaoweza kuhatarisha usalama katika jamii.

Kuhifadhi mila:
Kuhakikisha watoa huduma wanasimikwa rasmi na wazee wa jadi kwa mujibu wa mila na desturi.

Muundo wa Chama

Chama hiki kina viongozi na matawi katika ngazi mbalimbali nchini ikiwemo ngazi ya mikoa kama vile Tanga, Dodoma, na Singida ili kurahisisha ufuatiliaji wa karibu wa wanachama wake.
Huduma zote za matibabu ya asili nchini Tanzania zinatakiwa kufuata sheria na kusajiliwa rasmi na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala lililo chini ya serikali.
 
Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Institute of Finance Management, James Temba, anayejulikana kwa jina la Said Ally Mkomwa (31) maarufu kama “Saidini”, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya mahakama hiyo, upande wa mashtaka ulidai kuwa mtuhumiwa anakabiliwa na shtaka la mauaji, kosa ambalo Mahakama ya Wilaya haina mamlaka ya kulisikiliza hadi mwisho.
Kutokana na sababu hiyo, mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo. Aidha, alirudishwa mahabusu kutokana na kesi ya mauaji kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Juni 2, 2026 kwa ajili ya kutajwa tena huku uchunguzi na taratibu nyingine za kisheria zikiendelea.
Tukio hilo limeendelea kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi na wanafunzi, wengi wakitaka haki itendeke kufuatia kifo cha mwanafunzi huyo kilichotikisa jamii.

1779266269211.jpg
 
Back
Top Bottom