Yawaje sasa mwapeana migongo, kulikoni?

Yawaje sasa mwapeana migongo, kulikoni?

Mwambie kweli mimi na kupepesa kwangu macho muda wote hapa MMU nitaacha kuupitia kweli huo uzi? Au ndo ananitafutia sababu tu? Mimi siyo kusugua tu, hadi kuosha naosha. Viwango ni vya kimataifa.

gfsonwin haya majibu yananisukuma nisema Sumu umpe nafasi ya majaribio................................kama zoezi la kumsaili akishindwa asiwe na kumlaumu......................maana naona malenga ni kibao sana.......
 
Last edited by a moderator:
naogopa kufa baba si umesema mwenyewe ana black mamba?

gfsonwin sijui kwenye hilo ila ni hisia tu...........................nitapanga timu ya mauuguzi na vifaa vyote ile tiba upate mapema kabisa.............kama Sumu ni kali basi tuithibiti mapema.
 
Last edited by a moderator:
aahh! baba unakaba??
haya mfukoni kumetuna?? ama ndo kulia juani??

Huyu Sumu amejaa kishenzi vile.....................kwenye hilo ondoa khofu................maana katuna na kutunisha kila pembe labda khofu ni kwako tu............ gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
Nimeisoma tayari. Kama ndo hivyo, mimi nitakusugua kisaawia ili nijue utaniuliza swali gani.

Sumu kakuaahidi kukusugua kisaawia upo khapo gfsonwin jiandae au mwandalie mavituzi.........
 
Last edited by a moderator:
Haya Ruta malenga wetu ila uliyoandika ni ya kweli.Nautamani sana mchango wa Preta, Ciello,gfsonwin, FirstLady, Wiyelele(ingawa siku hizi kaingia mitini)lara1 atatibua,labda The Boss,Nyani Ngabu yeye ni Lawyer kwa hili mtu anawezasumbuka akili akijibiwa naye, Bujibuji sawa, kongosho a.k.a Triplex atakaanga mtu hapa. Ngoja niwe mpole nisijeumbuka.[QUOTE=Rutashubanyuma;5337177]View attachment 77406View attachment 77407View attachment 77408View attachment 77409
Hicho ni kitanda chako, hakistahili kupeana migongo, lol


Mlipoanzana sisi hatukuwepo kabisa!
Mlipotongozana siye hamkutualika!
Mlipokuwa mkibipiana ilikuwa siri yenu!
Mlipokuwa mkikonyezana mlikuwa pweke!
Mlipoanzana kufukuziana hamkutujuza hata!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Mlipowekana sawa sote mlitualika!
Mlipovalishana pete ilikuwa karamu!
Mlipovikana vilemba vya ukoka...........
Mlipotumiana posa si mliniita mshenga?
Mlipomiminiana mizawadi mbona furaha?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Miaka kweli haina subira, hupeperuka tu!
Miaka kweli imesonga tangia uushike ufyagio!
Miaka kweli imetupa kisogo tangia uuteme ukapera!
Miaka kweli imeishia tangia ufue na kusuuza kufuli zako!
Miaka kweli haichelei tangia uunguze kidole gumba jikoni!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Yaelekea sasa umemchoka na humtaki tena!
Yaelekea sasa umegundua kumbe ni chongo tu!
Yaelekea sasa umetambua havielei hivi hata!
Yaelekea sasa umefumbuka macho, hakuna chenga!
Yaelekea sasa mtaani umeonjeshwa asali na manenge!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Zile ahadi na mapochopocho kweli hukumbuki?
Kama kazeeka na wewe je ungali mbichi?
Kama hawaki je na wewe nawe wawaka?
Kama kajiachia na wewe kweli hujioni?
Mbona hivyo walakini wawaka tamaa hivyo?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

[/QUOTE]
 
Haya Ruta malenga wetu ila uliyoandika ni ya kweli.Nautamani sana mchango wa Preta, Ciello,gfsonwin, FirstLady, Wiyelele(ingawa siku hizi kaingia mitini)lara1 atatibua,labda The Boss,Nyani Ngabu yeye ni Lawyer kwa hili mtu anawezasumbuka akili akijibiwa naye, Bujibuji sawa, kongosho a.k.a Triplex atakaanga mtu hapa. Ngoja niwe mpole nisijeumbuka.

Thanda usipofunguka wewwe sasa ni mchoyo wa elimu funguka nasi tuelimike.........................
 
Last edited by a moderator:
Huyu Sumu amejaa kishenzi vile.....................kwenye hilo ondoa khofu................maana katuna na kutunisha kila pembe labda khofu ni kwako tu............ gfsonwin

Na kama atanipa vitu adimu ndo kabisaa, hati za majumba yangu ya hapa mjini nitaandika jina lake.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
baba uju sjapenda bado.ila unanilazimisha.

gfsonwin mwanangu mimi nilifikiria ni chaguo lako kumbe hapana basi nimeuvua ushange kuanzia leo itabidi Sumu ajipange upya...........simpigii debe tena!
 
Last edited by a moderator:
haya baba nasubri uniage kwa heshima zote ndo nitoke.

gfsonwin kama humpendi itabidi nisikuage kwa heshima zote maana utaodoka na vinyongo kuwa baba kakulazimisha..........
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin thamani naikumbuka lakini ukipenda nifanyaje zaidi ya kukuruhusu tu...................

Umenikosha sana mkwe kwa maneno yako ya hekima ya kiwango cha juu kabisa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Na kama atanipa vitu adimu ndo kabisaa, hati za majumba yangu ya hapa mjini nitaandika jina lake.

Sumu mbona wanitisha na hizo bidhaa adimu zikoje isije kuwa ni kile kifaa........
 
Last edited by a moderator:
Umenikosha sana mkwe kwa maneno yako ya hekima ya kiwango cha juu kabisa.

Sumu inaelekea wewe ni mkono wa birika binti yangu atapata shida ukimchukua....maana hata kumgongea gfsonwin "likes" humgongei kwa maneno yake matamutamu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom