Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Yatima inahusiana nini na kujinyonga? mtu miaka 28 unajihesabia yatima?
nilidisco nipo mwaka 3 sikukata tamaa nikarudia upya mwaka wa kwanza! nikatusua vizuri tu.
Kujinyonga ni ujinga upumbafu
Kwa kozi kama daktari au Architecture ambazo degree ni miaka mitano, it is likely kwamba mpaka anapata matokea ya kufeli kwa mara ya pili ni kwamba ameshainvest up to 7yrs of his life hapo chuoni, kumwambia aanze upya ni likely atenge tena 5yrs of his life ili jumla iwe 12yrs. Ila kujinyonga sio suluhisho, tupo tumesoma hizo kozi ndefu na kufaulu vizuri ila tunafanya shughuli zingine tofauti, simply because kuna fursa nyingine zenye manufaa zaidi.., so hata alivyofeli bado angetusua
 
......Mwanafunzi wa chuo unajinyonga kwa kufeli mtihani?, bado elimu yetu haijaweza kumsadia mwanafunzi kujitambua..poleni wafiwa.
 
Mdogo wangu alifeli pale Muhimbili akiwa mwaka wa 3, alilia sana. Kilichotuumiza hata sisi familia ni kwamba kijana alikuwa vizuri sana kichwani, form four alipata div one ya point 8, form six PCB akagonga BBB (pointi sita). Tuliumia sana. Tukakaa naye na tukawa tunamchunga kila siku tukiogopa angejidhuru. Baada ya mwaka mmoja nyumbani alibadilika sana, kwanza aliyachukia kabisa yale masomo na hakutaka kuyasikia tena. Akajiunga chuo kikuu kingine kwa BA community development. Baada ya miaka 3 akamaliza na kuunga MA na baadaye PhD. Sasa hivi ni consultant wa kazi za world bank na mashirika mengine ya UN, yuko vizuri mara nyingi kuliko wale waliofaulu ile kozi ya Muhimbili aliyofeli, na ni nguvu yetu sasa kwenye familia.

Na Muhimbili walizidi sana kuwafelisha vijana wazuri, kumbe kozi zao hata hazina tija, wanaozifaulu tunawaona wanalialia tu njaa mitaani na kusimangwa hadharani na wanasiasa kuwa ni wezi wa dawa! Kwa hali ilivyo katika taaluma hiyo, mtu akifeli mtihani anatakiwa amshukuru Mungu kwa kumtoa kwenye lindi la dhiki!
 
Vifo vingine hutokea ili waliobakia wajifunze jambo.

Poleni sana wazazi, ndugu na jamaa pia marafiki.

Mungu amlaze marehemu sehemu yake anayostahili.
 
Mnaosoma muache kukariri kuwa elimu ni njia ya kuupata utajiri au kuyapatia maisha, elimu ni njia ya kupambana na umasikini.
Kuna watu darasa la saba hawakumaliza ila ni matajiri wakubwa, wamekujajisomesha baada ya kupiga maisha.
 
fa8c4df43d554b071229c912cffc4dd7.jpg
 
Ila kuna wakati n mgumu sana hapa duniani, sometyms MTU na digrii yako still ck mbili unakaa bila kula coz vyuma vimekaza. Anyway hata hivyo kujinyonga kwa kufeli mtihan hakumfany marehemu aufaulu huo mtihan
 
Yoyote anayesomea udaktari na anafeli hatakiwi kuwa daktari, huyu alilazimisha kitu asichiweza
Kakosa vyote sasa
 
Mabisi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mgeninani, Kata ya Kijichi wilayani anadaiwa kukutwa amejinyonga jana saa saba mchana maeneo ya Mgeninani.


Sad news, RIP Mabisi, alitafakari akaona atakuwa Mgeni wa nani maana hata jina la mtaa wake linamkumbusha
 
Back
Top Bottom