Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,047
Reaction score
3,979
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Imtu, Daniel Mabisi (28) anadaiwa kujinyonga kutokana na kufeli mitihani.

Mabisi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mgeninani, Kata ya Kijichi wilayani anadaiwa kukutwa amejinyonga jana saa saba mchana maeneo ya Mgeninani.

Taarifa zilizopatikana zinadai siku mbili kabla ya kujinyonga, mwanafunzi huyo alionekana mtaani hapo baada ya kutoka chuo alikokuwa akisoma.

Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo amefeli mara mbili mfululizo.

Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro, baba mdogo wa marehemu, Joseph Lukuba alisema amepokea kwa mshtuko taarifa za mtoto wake.

“Nimepigiwa simu mchana huu nikaambiwa Daniel amejinyonga, nimeshtuka kwa sababu ni juzi tu tulimtumia nauli ili arudi nyumbani Mwanza baada ya kupata taarifa kuwa amefeli kwa mara nyingine,” alisema Lukuba.

Alisema uamuzi aliouchukua unasikitisha kwa kuwa kufeli, isingekuwa sababu ya kushindwa maisha hadi kufikia uamuzi wa kujinyonga.

“Kama familia tumehama na tuko mbali kikazi, tumemuomba jirani asimamie suala hili wakati taratibu za mazishi au kusafirisha mwili zikiendelea,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeninani, Khuruka Mwinyimvua alisema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kukuta mwili ukiwa umening’inia juu ya mwembe.

“Kijana huyo alionekana tangu juzi akizunguka mtaani hapa baada kurejea kutoka chuoni anakosoma, alionekana kama mtu asiyekuwa na furaha,” alisema Mwinyimvua na kuongeza: “Hadi sasa mwili umechukuliwa na polisi kwa taratibu nyingine.”

Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alithibitisha kupokea taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo na kuwaagiza askari walio karibu na maeneo hayo kuchukua mwili huo.

Mwananchi
 
shida wazazi wanatukaririsha kama elimu ni ufunguo wa maisha...

mzazi wa diamond angekuwa na vihela muajiriwa wa serikali.. nina imani angemkomalia diamond asome sana hata kwa viboko.. na leo angekuwa anazunguka na bahasha au amejinyonga kwa kufeli...

kuna maisha mengi mazuri nje ya elimu
 
Hahahahah kwani wewe unadhani muhimbili uwa wanamaliza wote?? disco zipo za kutosha tu,
Wewe ulisoma kozi gani usijekuwa ulisoma Baed muslimu universty ukajiona kipanga
Kusoma Muhimbili hakukupi justification ya kudisco., ingekuwa hivyo ratio ya wanaodisco ingekuwa kubwa kuliko wanaograduate., kupata supplementary unaweza jitetea ila disco inatokana na kuzembea kwa Mwanafunzi haijalishi umesoma Chuo cha namna gani ilimradi wamekudahili maana yake hauna tofauti na wengine!
 
Yani huyu marehem kanichafua kweli.
Aaargh! Wala siendi kwenye msiba wake.
 
Apumzike kwa amani Ndugu yetu
Kuna watu wanacomment humu as wako perfect 100% hivi mnajua depression,burnout halafu ukose ushauri nasaha mzuri???
Wengi wanacommit Suicide kutokana na Vitu mbalimbali kama vile
Unemployment
Social isolation
Divorce
Kufeli maisha
Msongo wa mawazo uliopitiliza nk

La msingi ni vyuo au ofis zetu kuwa na watu wa ushauri nasaha inapotokea mfanyakazi kafukuzwa au mwanafunzi kafeli mitihani yake basi apewe ushauri mzuri na wataalamu.
 
Inawezekana marafiki zake wote wamefauli yeye kajiona ana maana tena kuendelea kuishi ila kachuakua uamuzi wakijinga akuna anayejua kesho
 
Kujinyongea mbali na kwao kakosea sana .kuwapa watu gharama za kumsafirisha.angekunywa sumu ya masaa kadhaa akafie kwao uko au akajinyongee kwao
 
Back
Top Bottom