Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Ujinga uliopitiliza. Yani kufeli mara 2 tu anajiua.
kuna watu wanafeli zaidi ya mara 10 lakini hawakati tamaa na ikitokea fursa hawabaki nyuma.
Hakujifunza hata kwa Odinga
Badala ya kumwita marehemu mjinga alopitiliza nadhani ungejiweka kwenye nafasi yake ukamhurumia na huko aendako.
Alihutaji faraja na kutiwa moyo...akavikosa.Afu sidhani kama alikuwa na demu kitaa.Angepiga mabao ya hasira unafikiri kitanzi angekiwazia?
 
shida wazazi wanatukaririsha kama elimu ni ufunguo wa maisha...

mzazi wa diamond angekuwa na vihela muajiriwa wa serikali.. nina imani angemkomalia diamond asome sana hata kwa viboko.. na leo angekuwa anazunguka na bahasha au amejinyonga kwa kufeli...

kuna maisha mengi mazuri nje ya elimu
Rubbish, out of millions wangapi wamekuwa kama Diamond, unaleta kubahatisha kuwa ndio main route ro life
 
Dah, si angeomba hata Bomu moja akajilipue kule "kikini" ili walau atukomboe watanzania wenzie, hii ni hasara.
[emoji2] [emoji1] [emoji119] [emoji119]
Una utani we jamaaa we haya tu.
 
Yatima inahusiana nini na kujinyonga? mtu miaka 28 unajihesabia yatima?
nilidisco nipo mwaka 3 sikukata tamaa nikarudia upya mwaka wa kwanza! nikatusua vizuri tu.
Kujinyonga ni ujinga
We kaka muongo, eti ulidisko ukarudi [emoji51] [emoji16] [emoji119] [emoji119]
 
we kilaza uli disco vipi chuo
Namshangaa sana huyu kaka eti alidisko halafu akarudia mimi nisingeweza kurudia ningeacha kabisa kusoma. [emoji1] [emoji2] [emoji3] [emoji119] [emoji119]
 
fa8c4df43d554b071229c912cffc4dd7.jpg

Dah mwanafunzi wangu huyu, nimesikitika sana.
 
This is the saddest thing nimesoma leo. Reflecting all the time you hit the margin marks.. but yet we never lost hopes.

Mungu awaongoze na kuwa faraja kwa wanafunzi wanaopitia hii hatua
 
This is the saddest thing nimesoma leo. Reflecting all the time you hit the margin marks.. but yet we never lost hopes.

Mungu awaongoze na kuwa faraja kwa wanafunzi wanaopitia hii hatua

Hakuna kitu kibaya kama kupoteza tumaini. Unadhani maisha yamefika mwisho. Mtu asipopata msaada ya kiroho na kisaikolojia anaweza ku opt kujidhuru. Mungu atusimamie pale tunapokua tunapitia changamoto za kimaisha
 
Kusoma Muhimbili hakukupi justification ya kudisco., ingekuwa hivyo ratio ya wanaodisco ingekuwa kubwa kuliko wanaograduate., kupata supplementary unaweza jitetea ila disco inatokana na kuzembea kwa Mwanafunzi haijalishi umesoma Chuo cha namna gani ilimradi wamekudahili maana yake hauna tofauti na wengine!
Muhimbili iache iitwe muhimbili... watu wanaodisco pale 90% sio vilaza.... there is a very thin line kati ya kudisco na kupass especially modular system.
Usidharau anaedisco hata siku moja unless wewe umesoma chuo husika na kozi husika.
 
Mdogo wangu alifeli pale Muhimbili akiwa mwaka wa 3, alilia sana. Kilichotuumiza hata sisi familia ni kwamba kijana alikuwa vizuri sana kichwani, form four alipata div one ya point 8, form six PCB akagonga BBB (pointi sita). Tuliumia sana. Tukakaa naye na tukawa tunamchunga kila siku tukiogopa angejidhuru. Baada ya mwaka mmoja nyumbani alibadilika sana, kwanza aliyachukia kabisa yale masomo na hakutaka kuyasikia tena. Akajiunga chuo kikuu kingine kwa BA community development. Baada ya miaka 3 akamaliza na kuunga MA na baadaye PhD. Sasa hivi ni consultant wa kazi za world bank na mashirika mengine ya UN, yuko vizuri mara nyingi kuliko wale waliofaulu ile kozi ya Muhimbili aliyofeli, na ni nguvu yetu sasa kwenye familia.

Na Muhimbili walizidi sana kuwafelisha vijana wazuri, kumbe kozi zao hata hazina tija, wanaozifaulu tunawaona wanalialia tu njaa mitaani na kusimangwa hadharani na wanasiasa kuwa ni wezi wa dawa! Kwa hali ilivyo katika taaluma hiyo, mtu akifeli mtihani anatakiwa amshukuru Mungu kwa kumtoa kwenye lindi la dhiki!
Kwa kusummarize maelezo yako.... sio kila anaedisco ni kilaza au mzembe.
 
Acha kujidanganya mkuu wadahiliwa wa vyuo wanatofautiana sana. Huwezi kulinganisha mdahiliwa wa Muhimbili na wa Tumaini au SAUTI
Inawezekana hajui cream ya taifa ya PCB imejaa pale pharmacy na medicine.
Pia hajui vyuo vingine vingi tu vya afya vinaazima walimu muhimbili.... muhas haifananishwi.
Angesema kufanikiwa baada ya chuo haijalishi umesoma chuo gani angeeleweka zaidi na sio kufananisha muhas na vyuo vya juzi... chuo profs wa kuokota, PhD holders wa kuunga unga, student GPA 4 akija kusoma masters muhas mtupu kichwani as if hajapitia degree....
 
Muhimbili iache iitwe muhimbili... watu wanaodisco pale 90% sio vilaza.... there is a very thin line kati ya kudisco na kupass especially modular system.
Usidharau anaedisco hata siku moja unless wewe umesoma chuo husika na kozi husika.
Kiongozi hakuna aliemdharau aliedisco. Aidha kuna tofauti kubwa kati ya Kilaza na Mzembe, Mzembe ni yule ambae anauwezo Mkubwa lakini hayupo makini, anapuuzia mambo, mambo mengi kwa wakati mmoja n.k, haliyakuwa Kilaza uwezo wake ni mdogo ama ana kiwango kidogo cha uelewa tofauti na wenzake sasa hebu linganisha na ulichokiongea wewe!
 
yeye ndiye ajuaye magumu aliyo yapitia, kumuita/kuita kitendo chake upuuzi mnakosea.

kuna ile unatoka home unaona kabisa namna walivyo uza mashamba, viwanja kwa ajili yako na tumaini pekee likawekwa kwako. huku ukisindikizwa na maneno kasome yaani ukifeli umeiua familia.

inatokea unafeli, unaziona lawama taslimu za ndugu, familia na ukoo mzima. huoni mchongo wa kuzipa gape hauna wa kumshirikisha maswahibu yako hapo r.i.p itakuhusu.

humu wengi mnaongea tu hata kulala njaa hajawahi, mmesomea shule nzuri bila bugudha ya wazazi kuuza kila kitu na kuweka tumaini lote kwako.

acheni haya mambo kama una moyo laini, kitanzi kitahusika tu
 
Watu wengi wanaojiua uwa siyo sababu ya kile kinachodaiwa ndiyo chanzo cha kujiua kwao.
Uwa ni series of events na anajikuta hana wa kumwambia yanayomsumbua anajiona yuko peke yake.
Hilo la mwisho uwa ni kama limevuta triger ya bastola, lakini inakuwa ni mfululizo wa matukio.
Point!!!
 
Back
Top Bottom