Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

Yatima, mwanafunzi wa IMTU ajinyonga baada ya kufeli mtihani

......Mwanafunzi wa chuo unajinyonga kwa kufeli mtihani?, bado elimu yetu haijaweza kumsadia mwanafunzi kujitambua..poleni wafiwa.
SIO HAPA TU HATA HUKO UGHAIBUNI NIMEWAHI SOMA WAKIFANYA HIVO HIVO. SIJUI NI NINI LAKINI INALETA DEORESSION UKIRUDISHWA NYUMBANI
 
Kusoma Muhimbili hakukupi justification ya kudisco., ingekuwa hivyo ratio ya wanaodisco ingekuwa kubwa kuliko wanaograduate., kupata supplementary unaweza jitetea ila disco inatokana na kuzembea kwa Mwanafunzi haijalishi umesoma Chuo cha namna gani ilimradi wamekudahili maana yake hauna tofauti na wengine!
Acha kujidanganya mkuu wadahiliwa wa vyuo wanatofautiana sana. Huwezi kulinganisha mdahiliwa wa Muhimbili na wa Tumaini au SAUTI
 
hiii taarifa imenikumbusha mbali sana kulikuwa na jamaa yetu alipotea kwa ,mazingira kama haya.
lakini kuna haja ya hizi taasisi za elimu kuweka utaratibu wa kuwaanda kisaikolojia hwa vijana kabla ya kuwapa matokeo.
vijana wengi wanaamini wakifeli mitihani ndo mwisho wao lkn mimi ninavijana wangu wengi walifeli lkn walipata mafanikio mengine zaida ya pale pengine wamefanikiwa kuzidi wale waliowaacha wanasoma.

mwisho vyuo viache kuchukulia haya mambo kawaida vijana wengi wanapotea kazi za madini wa wanafunzi zipitiwe upya.

tukio hili limenikumbusha mbali sana.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Imtu, Daniel Mabisi (28) anadaiwa kujinyonga kutokana na kufeli mitihani.

Mabisi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mgeninani, Kata ya Kijichi wilayani anadaiwa kukutwa amejinyonga jana saa saba mchana maeneo ya Mgeninani.

Taarifa zilizopatikana zinadai siku mbili kabla ya kujinyonga, mwanafunzi huyo alionekana mtaani hapo baada ya kutoka chuo alikokuwa akisoma.

Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo amefeli mara mbili mfululizo.

Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro, baba mdogo wa marehemu, Joseph Lukuba alisema amepokea kwa mshtuko taarifa za mtoto wake.

“Nimepigiwa simu mchana huu nikaambiwa Daniel amejinyonga, nimeshtuka kwa sababu ni juzi tu tulimtumia nauli ili arudi nyumbani Mwanza baada ya kupata taarifa kuwa amefeli kwa mara nyingine,” alisema Lukuba.

Alisema uamuzi aliouchukua unasikitisha kwa kuwa kufeli, isingekuwa sababu ya kushindwa maisha hadi kufikia uamuzi wa kujinyonga.

“Kama familia tumehama na tuko mbali kikazi, tumemuomba jirani asimamie suala hili wakati taratibu za mazishi au kusafirisha mwili zikiendelea,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeninani, Khuruka Mwinyimvua alisema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kukuta mwili ukiwa umening’inia juu ya mwembe.

“Kijana huyo alionekana tangu juzi akizunguka mtaani hapa baada kurejea kutoka chuoni anakosoma, alionekana kama mtu asiyekuwa na furaha,” alisema Mwinyimvua na kuongeza: “Hadi sasa mwili umechukuliwa na polisi kwa taratibu nyingine.”

Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alithibitisha kupokea taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo na kuwaagiza askari walio karibu na maeneo hayo kuchukua mwili huo.

Mwananchi
 
Yatima inahusiana nini na kujinyonga? mtu miaka 28 unajihesabia yatima?
nilidisco nipo mwaka 3 sikukata tamaa nikarudia upya mwaka wa kwanza! nikatusua vizuri tu.
Kujinyonga ni ujinga
Kwa hiyo aliejinyonga mjinga?
 
hakuna dhambi mbaya kama kukata tamaa. Rest In Eternal Light Boy.
 
Acha kujidanganya mkuu wadahiliwa wa vyuo wanatofautiana sana. Huwezi kulinganisha mdahiliwa wa Muhimbili na wa Tumaini au SAUTI
Hicho ulicho kiquote umekielewa lakini? Inawezekanaje Chuo kimoja, course moja wadahiliwe kwa sifa tofauti? Kwa msingi huo ndio nikasema kama wote mmedahiliwa kwa sifa zinazoshabihiana kwenye course hiyo na Chuo hicho hicho then ukadisco huo ni Uzembe wako., na ndio mana wakaweka viwango hivyo wakiamini kuwa wote wenye sifa hizo watamudu course husika, haya niambie nilipodanganya?
 
huyo kijana angejua kwenye hii dunia watu wengi waliofanikiwa maisha ni watu ambao wamesoma kidogo au hawajasoma kabisa labda angebadili uamuzi wake.
 
Ujinga uliopitiliza. Yani kufeli mara 2 tu anajiua.
kuna watu wanafeli zaidi ya mara 10 lakini hawakati tamaa na ikitokea fursa hawabaki nyuma.
Hakujifunza hata kwa Odinga
Watu wengi wanaojiua uwa siyo sababu ya kile kinachodaiwa ndiyo chanzo cha kujiua kwao.
Uwa ni series of events na anajikuta hana wa kumwambia yanayomsumbua anajiona yuko peke yake.
Hilo la mwisho uwa ni kama limevuta triger ya bastola, lakini inakuwa ni mfululizo wa matukio.
 
Wakuu mimi mtu akijinyonga humu tutakosana, na rambirambi yangu hupati. Kudisco chuo ni uzembe, kujinyonga kwa kua umedisco ni uzembe na nusu. Kwa ufupi Marehemu kazihirisha uzembe wake, lazma nimlaumu kifo hakiwez kuhalalisha kosa la yeye kujiua, japo vile vile kujiua kwake hakukuhalalishi wewe kufurahia kifo cha mwenzako.
 
Atakuwa alisoma Law Tumaini university au SAUTI
Na nyie watoto wa UDSM muache kuwananga wenzenu wa Tumaini na SAUTI. Lawyer ni lawyer tu, kwa sifa yake ya kujua sheria na kutetea vizuri kiweledi, si kwa kusoma UDSM. Hata huko UDSM kuna vilaza wengi tu.
Leo kwenye gazeti la Daily News wamechapisha titles za PhD theses walizoandika watunukiwa 80 wa PhD za UDSM mwaka huu, akiwemo mhe Mwigulu Nchemba. Nyingine nimezitazama nikajiuliza hivi hii ni ya PhD au undergraduate? Na nyingi kati ya hizo zinazofanana na za postgraduate hazitofautiani na za masters. Katika zile nimeona PhD za ukweli ni kama 4 tu, ya Mwigulu Nchemba ikiwemo. Nyingine wameandika tu wamalize muda wao wapate degree wasepe.
 
Mtu akijiua moja kwa moja we uliyebaki hai funga domo lako.

Kujiua ni jambo baya kabisa hatukatai...
Lakini hatujui dakika za mwisho za aliyejiua kiakili kama huwa yuko sawa au la kwa hivyo hakuna kuhukumu hapo, MUNGU amsamehe na sisi atuepushe na kujiua maanake hatujui mwisho wetu...

Wapo wanaojiua taratibu kwa uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa ya kulevya,ngono zembe, tena hawa wana akili timamu na wanajua madhara ya hivyo wavitumiavyo, lakini wakiugua wakafa kwa magonjwa yatokanayo na tabia zao hizo hamsemi wamejiua, mnasema wameugua....

MUNGU tuepushe na mabalaa wewe ndiye BWANA MLEZI wetu na ndiye ujuaye hatima zetu.
 
South Korea, Japan, India kunaongoza kwa haya...
RIP kijana
 
Back
Top Bottom