Thomas Odera
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 673
- 155
Kwa hili sina jibu maana sina uhakikana haya uliyoyaandika.
Mi si mzima na naamini wajua kwanini mie si mzima. Nakumisi mbaya.nilijua tu utashabikia! mzima wewe?
Uzinzi mtupu tu, ndoa sawasawa na maagizo ya Muumba wa wanadamu wote ni mume mmoja mke mmoja hadi kifo zaidi ya hapo ni uzinzi tu, Matayo 19:9Mtambuzi, in this day and age bado kuna mtu akili yake inamtuma kuoa zaidi ya mke mmoja ili kukidhi mahitaji yake ya kingono? Naelewa tamaduni za kiafrika polygamy ni kitu cha kawaida. Wake wawili nafikiri ni sawa, lakini wanne wote sidhani kama mwanamme unaweza kukeep up umri ukianza kupanda, so it is unfair to them. Halafu ukizidi kuoa na kuzaa mpaka unafikisha miaka yako ya kuingia kaburini unawanyima nafasi hao watoto wako kukufahamu na kuwa na baba maishani mwao.
King Mswati na mamilioni yake huwezi ku compare na Hamisi aishie Tandale. Huyo Kody wa USA wana dini yao wanayoifuata ndio inaruhusu aoe wake kadhaa lakini kuna state nyingi marekani hawaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja. Unaweza ukatupwa jela kwa kuoa zaidi ya mke mmoja.
Kumbuka mwanmziki Fela Kuti alioa wanawake wengi na alikufa kwa UKIMWI. Wanawake si kuku wa kufuga unajizolea tu. Ukishindwa kukidhi mahitaji (na utashindwa tu) ujue atatembea nje. Ndio maana hiyo mifano mliyotoa wengi wao waliwaacha wake zao kwa sababu ya ku cheat. Hao ambao hawakuachwa labda hakuwa na evidence, but they must have cheated.
Hapa naona shetani yuko kwenye mission maalumu ya kuwanasa watu wengi katika uzinzi "halali" kwa mawazo ya kibinadamu na hakika kwa njia hii atawanasa wengi sana. Mgeukieni Bwana mkapone vinginevyo mtanasha katika mtego wa shetani muuaji na mtashutuka mkiwa motoni tayari.![]()
Imebainika kwamba kuna ukweli mkubwa kuwa wanaume wenye kufanya mapenzi halali kwa wingi au mara nyingi huishi muda mrefu zaidi. Hii ina maana pia kwamba, labda wanaume wenye wake wengi huishi muda mrefu zaidi, kuliko wale wenye mke mmoja.
Kuna wazee wengi ambao ninawafahamu wenye umri mkubwa sana. Lakini nikichunguza kwa makini naona kama wengi kati yao walikuwa au wameoa wake wengi. Inawezekana kuwa hiyo ni nasibu (coincidence)tu ya mambo, lakini kwa sehemu kubwa haionyeshi hivyo.
Ngoja nikupeni mfano wa mzee mmoja kule nchini India. Huyu mzee alifariki akiwa na umri wa miaka 84 kufuatia ajali ya gari hapo mnamo mwaka 2005. Alikuwa ameoa wanawake 91. Mzee huyu, Udaynath Dakhinaray, alianza kuoa mke wa kwanza wakati akiwa shuleni, lakini ndoa yake ilivunjika. Baada ya ndoa kuvunjika alijiapiza kwamba, ni lazima angeoa wanawake 100 katika maisha yake.
Kwa bahati mbaya, wakati akiwa na mke wa 91 alipata ajali ya gari na alifariki baadaye, bila kukamilisha ndoto yake. Lakini kufikia miaka 84 na bado kuwa na nguvu, huenda ni ushahidi kwamba, kuoa wake wengi kuna faida kwenye suala la umri.
Lakini kama ambavyo imekuwa ikisemwa siku zote, afya inayotokana na tendo la ndoa huwajia wale tu ambao wanalifanya kihalali. Hapa naomba Mzee wa Kugegeda mzabzab anisome kwa makini. Usije ukaanza kuhangaika kutafuta umri mkubwa kwa kuparamia vibinti na kuvigegeda, tutakuzika ukiwa kijana mbichi bado.
Hebu jaribu kuvuta kumbukumbu zako uwaweke mawazoni mwako wazee wote unaowafahamu, wawe hai au wawe wamekufa. Halafu jaribu kufikiri ni wangapi wamefikisha umri wa miaka 80. Najua utashangaa kwamba, ni karibu wote walikuwa wameoa wanawake wengi.
Kuna wanaosema, hiyo inatokana na ukweli kwamba, hao wanaooa wake wengi hawako wengi. Ina maana kwamba, fikiria kuhusu wazee wenye wake au waliokuwa na wake wengi, halafu fikiria wale ambao hawana wake wengi, halafu upige hesabu kwa slilimia ya wale walio hai na waliokufa, halafu weka majibu yako hapa.