Mtambuzi
Kuna ukweli ndani ya makala yako lakini lazima mtu uangalie kwa ndani
kwa uoni wangu ukiwa na mke mmoja majanga ni mengi na kuringa kwingi kwa
mke, ukiongeza wa pili utakuwapo ugomvi na hasa mke wa mwanzo lakini
ukiongeza wa tatu yule wa mwanzo anakuwa na furaha sana na wa pili ndio
ugomvi kwake
njia nzuri ya kuishi nao wafanye wagombane wewe utakuwa umeepuka
pressure
nafikiri ililetwa makala humu kuwa ukiwa unafanya maingiliano na mkeo
kila ya muda mfupi msingano wa akili hupunguwa na mzunguko wa damu
mwilini huwa mzuri hata mafuta kwenye damu huyayuka,
lakini wanawake wengi huanza nyodo baada ya kupata mtoto au watoto
wawili na wanajuwa kuwa unahitaji pumziko ukioa mke mwengine kuongeza wa
pili na watatu mzunguko wako unakuwa mwepesi kila nyumba unayokwenda
kuna pumziko la kutosha
ngoja nikatafute nami niongeze umri kwa kuanzia watatu
wanaoshupalia kuhalalisha ndoa za mitala mi nawashangaaga sana, kuna mmoja aliibuka eti kwa sababu za kimaumbile wanaume waoe wake wengi na huyu naye kaibuka na utafiti feki. huo ni uzinzi bin ufuska kwani tangu mwanzo Mungu alimuumba Adam akampa mke mmoja tu. Eti kimaumbile, kwani wewe unazo ngapi (penis)?
Nakutakia safari njema (hapo kwenye red).
![]()
Imebainika kwamba kuna ukweli mkubwa kuwa wanaume wenye kufanya mapenzi halali kwa wingi au mara nyingi huishi muda mrefu zaidi. Hii ina maana pia kwamba, labda wanaume wenye wake wengi huishi muda mrefu zaidi, kuliko wale wenye mke mmoja.
Kuna wazee wengi ambao ninawafahamu wenye umri mkubwa sana. Lakini nikichunguza kwa makini naona kama wengi kati yao walikuwa au wameoa wake wengi. Inawezekana kuwa hiyo ni nasibu (coincidence)tu ya mambo, lakini kwa sehemu kubwa haionyeshi hivyo.
Ngoja nikupeni mfano wa mzee mmoja kule nchini India. Huyu mzee alifariki akiwa na umri wa miaka 84 kufuatia ajali ya gari hapo mnamo mwaka 2005. Alikuwa ameoa wanawake 91. Mzee huyu, Udaynath Dakhinaray, alianza kuoa mke wa kwanza wakati akiwa shuleni, lakini ndoa yake ilivunjika. Baada ya ndoa kuvunjika alijiapiza kwamba, ni lazima angeoa wanawake 100 katika maisha yake.
Kwa bahati mbaya, wakati akiwa na mke wa 91 alipata ajali ya gari na alifariki baadaye, bila kukamilisha ndoto yake. Lakini kufikia miaka 84 na bado kuwa na nguvu, huenda ni ushahidi kwamba, kuoa wake wengi kuna faida kwenye suala la umri.
Lakini kama ambavyo imekuwa ikisemwa siku zote, afya inayotokana na tendo la ndoa huwajia wale tu ambao wanalifanya kihalali. Hapa naomba Mzee wa Kugegeda mzabzab anisome kwa makini. Usije ukaanza kuhangaika kutafuta umri mkubwa kwa kuparamia vibinti na kuvigegeda, tutakuzika ukiwa kijana mbichi bado.
Hebu jaribu kuvuta kumbukumbu zako uwaweke mawazoni mwako wazee wote unaowafahamu, wawe hai au wawe wamekufa. Halafu jaribu kufikiri ni wangapi wamefikisha umri wa miaka 80. Najua utashangaa kwamba, ni karibu wote walikuwa wameoa wanawake wengi.
Kuna wanaosema, hiyo inatokana na ukweli kwamba, hao wanaooa wake wengi hawako wengi. Ina maana kwamba, fikiria kuhusu wazee wenye wake au waliokuwa na wake wengi, halafu fikiria wale ambao hawana wake wengi, halafu upige hesabu kwa slilimia ya wale walio hai na waliokufa, halafu weka majibu yako hapa.
Hii haina ukweli wowote ule, kinyume chake watu wanaooa wake wengi ndio wanaongoza kufa mapema, mm mwenyewe babu zangu walikuwa wameoa wake wengi, baba mkubwa wangu naye alikuwa na wake wengi na wengineo lakini hawakufikisha hata miaka 70. wengi wanakufa mapema kwasababu ya magomvi ya wake zao ambao wengine huishia kulogwa au kupewa sumu ili wakose wote. ww fanya practical example utarudi kutueleza haya ninayokuambia
mtu kuishi miaka mingi inategemea na health factors nyingi sana, mfano body immunity yake na endapo anaepukana na risk behaviours including unnecessary stress whether at home or workplace
mbona ejnzi za biblia watu waliooa mke mmoja waliishi hadi miaka 986 -soma umri wa Adamu. hivyo, your conclusion has conflict of interest