Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,441
Imebainika kwamba kuna ukweli mkubwa kuwa wanaume wenye kufanya mapenzi halali kwa wingi au mara nyingi huishi muda mrefu zaidi. Hii ina maana pia kwamba, labda wanaume wenye wake wengi huishi muda mrefu zaidi, kuliko wale wenye mke mmoja.
Kuna wazee wengi ambao ninawafahamu wenye umri mkubwa sana. Lakini nikichunguza kwa makini naona kama wengi kati yao walikuwa au wameoa wake wengi. Inawezekana kuwa hiyo ni nasibu (coincidence)tu ya mambo, lakini kwa sehemu kubwa haionyeshi hivyo.
Ngoja nikupeni mfano wa mzee mmoja kule nchini India. Huyu mzee alifariki akiwa na umri wa miaka 84 kufuatia ajali ya gari hapo mnamo mwaka 2005. Alikuwa ameoa wanawake 91. Mzee huyu, Udaynath Dakhinaray, alianza kuoa mke wa kwanza wakati akiwa shuleni, lakini ndoa yake ilivunjika. Baada ya ndoa kuvunjika alijiapiza kwamba, ni lazima angeoa wanawake 100 katika maisha yake.
Kwa bahati mbaya, wakati akiwa na mke wa 91 alipata ajali ya gari na alifariki baadaye, bila kukamilisha ndoto yake. Lakini kufikia miaka 84 na bado kuwa na nguvu, huenda ni ushahidi kwamba, kuoa wake wengi kuna faida kwenye suala la umri.
Lakini kama ambavyo imekuwa ikisemwa siku zote, afya inayotokana na tendo la ndoa huwajia wale tu ambao wanalifanya kihalali. Hapa naomba Mzee wa Kugegeda mzabzab anisome kwa makini. Usije ukaanza kuhangaika kutafuta umri mkubwa kwa kuparamia vibinti na kuvigegeda, tutakuzika ukiwa kijana mbichi bado.
Hebu jaribu kuvuta kumbukumbu zako uwaweke mawazoni mwako wazee wote unaowafahamu, wawe hai au wawe wamekufa. Halafu jaribu kufikiri ni wangapi wamefikisha umri wa miaka 80. Najua utashangaa kwamba, ni karibu wote walikuwa wameoa wanawake wengi.
Kuna wanaosema, hiyo inatokana na ukweli kwamba, hao wanaooa wake wengi hawako wengi. Ina maana kwamba, fikiria kuhusu wazee wenye wake au waliokuwa na wake wengi, halafu fikiria wale ambao hawana wake wengi, halafu upige hesabu kwa slilimia ya wale walio hai na waliokufa, halafu weka majibu yako hapa.
Last edited by a moderator: