Yathibitika: kuoa wake wengi huongeza umri….!

Yathibitika: kuoa wake wengi huongeza umri….!

Last edited by a moderator:
Kwa hiyo Zuma naye ataishi miaka mingi maana nasikia naye ameoa oa!
 
[FONT=palatino
linotype]
21came600.1.jpg


Imebainika
kwamba kuna ukweli mkubwa kuwa wanaume wenye kufanya mapenzi halali
kwa wingi au mara nyingi huishi muda mrefu zaidi. Hii ina maana pia
kwamba, labda wanaume wenye wake wengi huishi muda mrefu zaidi, kuliko
wale wenye mke mmoja.

Kuna wazee wengi ambao ninawafahamu wenye umri mkubwa sana. Lakini
nikichunguza kwa makini naona kama wengi kati yao walikuwa au wameoa
wake wengi. Inawezekana kuwa hiyo ni nasibu (coincidence)tu ya mambo,
lakini kwa sehemu kubwa haionyeshi hivyo.

Ngoja nikupeni mfano wa mzee mmoja kule nchini India. Huyu mzee
alifariki akiwa na umri wa miaka 84 kufuatia ajali ya gari hapo mnamo
mwaka 2005. Alikuwa ameoa wanawake 91. Mzee huyu, Udaynath Dakhinaray,
alianza kuoa mke wa kwanza wakati akiwa shuleni, lakini ndoa yake
ilivunjika. Baada ya ndoa kuvunjika alijiapiza kwamba, ni lazima angeoa
wanawake 100 katika maisha yake.

Kwa bahati mbaya, wakati akiwa na mke wa 91 alipata ajali ya gari na
alifariki baadaye, bila kukamilisha ndoto yake. Lakini kufikia miaka 84
na bado kuwa na nguvu, huenda ni ushahidi kwamba, kuoa wake wengi kuna
faida kwenye suala la umri.

Lakini kama ambavyo imekuwa ikisemwa siku zote, afya inayotokana na
tendo la ndoa huwajia wale tu ambao wanalifanya kihalali. Hapa naomba
Mzee wa Kugegeda mzabzab anisome kwa makini.
Usije ukaanza kuhangaika kutafuta umri mkubwa kwa kuparamia vibinti na
kuvigegeda, tutakuzika ukiwa kijana mbichi bado.

Hebu jaribu kuvuta kumbukumbu zako uwaweke mawazoni mwako wazee wote
unaowafahamu, wawe hai au wawe wamekufa. Halafu jaribu kufikiri ni
wangapi wamefikisha umri wa miaka 80. Najua utashangaa kwamba, ni karibu
wote walikuwa wameoa wanawake wengi.

Kuna wanaosema, hiyo inatokana na ukweli kwamba, hao wanaooa wake wengi
hawako wengi. Ina maana kwamba, fikiria kuhusu wazee wenye wake au
waliokuwa na wake wengi, halafu fikiria wale ambao hawana wake wengi,
halafu upige hesabu kwa slilimia ya wale walio hai na waliokufa, halafu
weka majibu yako hapa.[/FONT]

Sijawahi sikia habari kama hii!
Wewe umeoa wangapi?
 
Last edited by a moderator:
Kama hivyo mwenzenu nitakufa mapema maana hata huyo mmoja bado sijampata na miaka inakimbia 30 sasa.
 
Nakubaliana na ww..mjini kwetu (sio kijijini) wazee wengi including mydad wana wake wengi na wamekula chumvi ya kutosha..
 
inaitwa 'moritutu'

nione kama ana ujanja wa kuzunguka vyumba 20
na kila mmoja apate haki yake.

Mkuu Mamdenyi inaelekea umechoka kuishi uraiani hivyo unatafuta sababu ya kwenda jela!

Akitumia moritutu hata nusu chumba hazunguki!!
 
Back
Top Bottom