Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,265
DAR-ES-SALAAM YANGA AFRICANS YASIMAMISHA MAANDAMANO MSIKITI WA MAKONDE ILIPOTOKA ADHANA
Waandamanaji wa Yanga waliokuwa katika maandamano makubwa wakiwa wamebeba kikombe chao cha ubingwa wa Ligi ya Tanzania walichokabidhiwa Mkwakwani Stadium Tanga wakitokea Uwanja wa Julius Nyerere wakielekea klabuni kwao walisimama kwa muda wakiwa kimya na kusimamisha ngoma zao na shamrashamra zote mara tu waliposikia adhana kutoka Msikiti wa Makonde.
Msikiti wa Makonde uko kwenye kona ya Mtaa wa Msimbazi na Swahili sehemu yenye shughuli nyingi sana nyakati za mchana.
Hapa si mbali na Mtaa wa Twiga yalipo Makao Makuu ya Yanga.
Mara waandamanaji waliposikia, "Allahu Akbar, Allah Akbar," breki za pikipiki zilizokuwa zikiongoza maandamano na magari yaliyokuwa nyuma zilipigwa.
Umma ukasimama ukiwa kimya hadi adhana ilipokamilika kuadhiniwa.
Msikiti wa Makonde ni msikiti ambao ulichelewa sana kukarabatiwa kugeuzwa kuwa msikiti wa kisasa pale misikiti ya Dar es Salaam ilipoanza kujengwa upya miaka ya 1970.
Sheikh Ali Abbas aliyekuwa mshabiki mkubwa ya Yanga ambae sasa ni marehemu alipata kuniambia kuwa ikiwa nataka kuona misikiti ya zamani ya Dar es Salaam ya 1940 niende nikasali Msikiti wa Makonde.