Yanga ni Klabu Bora Afrika kwa Mwaka 2022/2023 ndio maana imeingia kwenye Tuzo za CAF!

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
609
1,563
CAF wanathibitisha ubora wa Yanga kivitendo ndio maana wameiteua kuingia kwenye tuzo zao za kuchagua Timu Bora barani Africa kwa mwaka 2023.

Yanga ni timu pekee kwa Ukanda wa Africa Mashariki iliyoingia kugombania tuzo hizo!

Yanga hawakuingia kwa bahati mbaya bali wamebebwa kwa mafanikio yao na usajili bora wa kikosi husika walichonacho, ndio maana pia wametoa Kipa Djigui Diara kugombania tuzo ya kipa Bora barani Afrika!

Unaposema timu yako ni Bora basi CAF wenyewe ndio wenye vigezo halisi vya kujua timu gani ni Bora na sio propaganda za kwenye mitandao na vijiwe vya kahawa!

Timu nyingine ambazo kutwa nzima zinashinda kwenye media na kujiita Bora sijaziona na wala sijaona hata mchezaji wao mmoja ameingia kwenye tuzo hizo za Afrika, kupiga domo na porojo bila uhalisia ni sawa na kumnyemelea kiziwi ukidhani anakusikia!

Kitendo cha CAF kuichagua Yanga kuingia kwenye tuzo hizo ni ishara tosha ya kwamba yanga iko vizuri na itaendelea kuwa vizuri siku hadi siku!

Kongole Eng. Hersi Said na Menejiment nzima kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya na Mungu awabariki.👏👏👏👏
 
Nyie utopolo mtaishia kuteuliwa tu ila kubeba tuzo msahau
F92BXiGWUAAWi4R.jpeg
 
Hata Malumo wameingia na wameshuka Daraja.....

Aibu sana
Caf wanaangalia timu yako ilifanya Nini michuano yao na sio michuano ya ndani kwako msijizime data! Malumo kacheza NUSU fainali kombe la shirikisho wewe timu yako ilifika hatua iyo mwaka Gani? Kimataifa malumo kafanikiwa ndio maana yupo apo, vipi wewe uliyecheza robo fainali klabu bingwa umekosa ata kigezo Cha kufikiriwa kuingizwa kwenye kipengele Cha ushirikina kuchoma moto viwanja vya watu?
 
PIGA SPANA, BADO anapumua....
 
Hii habari.. ime wachanganya sana makolo-mbwezo efusi.. tena kama tunavyoelekea kwenye Darby..
 
Hebu niambieni ni vigezo gani vinatumika mpka timu iwekwe kwenye hizo tuzo? Nisije nikaanza kuwaponda simba kumbe sijui a wala b
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom