Tetesi: Kipa Djigui Diarra mbioni kuondoka Yanga

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Tetesi kutoka kwenye chanzo Cha kuaminika kutoka nchini Mali kuhusu Kipa wa Yanga SC Djigui Diarra zinasema Kuna timu ya ligi nchini Uturuki inahitaji huduma ya golikipa Huyo Bora ndani ya Africa akiwa amefanikiwa kutwaa tuzo ya golikipa Bora mara mbili ya ligi kuu,lakini akitwaa tuzo ya kipa Bora kwenye fainali kombe la shirikisho fainali dhidi ya USM Alger.

Wamevutiwa na ubora wa kipa Huyo baada ya kuingia kwenye kinyang’anyiro Cha kugombea kipa Bora katika tuzo za CAF na makipa wakubwa Afrika lakini pia amekuwa akitwa kwa muendelezo katika timu ya taifa ya Mali.

Lakini ukiacha yeye timu hiyo pia imevutiwa na mchezaji mwingine kiungo kutoka Mali Aliou Dieng kutoka klabu ya Al Ahly ya Misri nae akitakiwa kwenda kwenye hiyo klabu ya Uturuki pamoja na Screen protecter Diarra.
 
Na zibaki kuwa tetesi, bado sipo tayari kutokumuona Diarra pale golini.
Uwanjani hakutaendeka!

Japo utafika wakati ataondoka ila sio sasa.
Sifa ya timu bora kama yanga unaijua? Hata akiondoka tutapata perfect replacement ya Diara, anaweza asifikie uwezo kamili ila atakuwa na ubora. Atuwezi acha mabilioni 100 ya dili la diara.

Kuna watu wananuna ila wakikumbuka wao alitobolewa 5 sijui watamuuza soko gani, labda sterio 😂.
Hata timu yetu ya mtaa haitaki huduma ya bwana mdogo yule.
 
Usinichekeshe kwenye habari ya huzuni, kabla ya ujio wa Aziz Ki Diarra ndio alikuwa mchezaji wangu bora pale, and still he is.
 
Usinichekeshe kwenye habari ya huzuni, kabla ya ujio wa Aziz Ki Diarra ndio alikuwa mchezaji wangu bora pale, and still he is.
Yani wewe ni mimi kabisa, hakuna wachezaji ndani ya yanga kwa sasa nawakubali kama hao ukiongeza na Aucho.

Usihuzunike na niwatoe hofu wananchi wenzangu, hili la kipa nilishaongea na injinia nikamwambia takwa la wananchi na akaahidi kamwe hawezi kuleta kipa sampuli ya Ayubu maana ni aibu.
 
Kama ni kweli ,basi kila la kheri aendako mpira wenyewe ni ajira fupi mno, mtu mwenye miaka 33 tayari ni Mzee
 
Back
Top Bottom