Yanga mnaupiga mwingi, mafanikio ya msimu mmoja tu ndani ya michuano ya CAF ni kielelezo cha ubora wa timu yenu

Mtanzanias

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
1,747
3,723
Hakuna asiejua msoto aliopitia yanga miaka ya nyuma kwenye michuano ya kimataifa, mafanikio pekee aliyokuwa nayo ilikuwa ni kuingia hatua ya makundi kombe la shirikisho na akavuta mkia kwenye kundi lake, kipindi icho ilikuwa ni yanga ya kuungaunga sana.

Lakini baada ya uwekezaji mkubwa kwa kusajili wachezaji wenye quality kubwa na benchi bora la ufundi likichagizwa na uongozi imara pamoja na GSM yanga ndani ya msimu mmoja tu wa 2022/2023 imeweza kupanda kwa kasi ya kimbunga kwenye rank za caf, kabla michuano ya Caf aijaanza msimu huu yanga alikuwa nafasi ya 75 kwa ubora barani africa, baada ya kuitoa club africain na kutinga makundi yanga akapanda mpaka nafasi ya 48 kwa ubora, baada ya kutinga robo fainali amepanda mpaka nafasi ya 28 kwenye rank za CAF.

Na iyo ni ndani ya msimu mmoja tu,, sio jambo la kitoto iyo inakuonyesha ni namna gani wako vizuri msimu huu ndani na nje ya uwanja wamejipanga, Siwezi kujua wakifuzu nusu fainali watapanda mpaka nafasi ya ngapi caf ndio wanajua,,kiufupi uwezi kupata mafanikio ya haraka haraka kwenye soka la afrika kama unayo timu ya kuungaunga ni ngumu sana.

Yanga wapewe heshima yao na ninawaona wakifanikiwa zaidi na zaidi kulingana na mipango madhubuti waliyonayo, kile kichaka cha kutofanya vizuri kimataifa naona wanakifyeka mdogo mdogo na wale wasioitakia mema wanaangalia namna nyingine ya kuibua kichaka kingine baada ya hoja iyo kufa kifo cha kawaida,

Kongole wananchi🙌🙌🙌🙌🙏🙏🙏
 
Kombe la mazezeta ndilo Lililo waumbua Simba Kwa kufanya vitendo vya kishirikina Kwa kuwasha moto uwanjani pale Kwa Madiba.
Mkuu miye nilikuwa najua Hawa jamaa washacheza fainali shirikisho kumbe uongo
 
Hakuna asiejua msoto aliopitia yanga miaka ya nyuma kwenye michuano ya kimataifa, mafanikio pekee aliyokuwa nayo ilikuwa ni kuingia hatua ya makundi kombe la shirikisho na akavuta mkia kwenye kundi lake, kipindi icho ilikuwa ni yanga ya kuungaunga sana.

Lakini baada ya uwekezaji mkubwa kwa kusajili wachezaji wenye quality kubwa na benchi bora la ufundi likichagizwa na uongozi imara pamoja na GSM yanga ndani ya msimu mmoja tu wa 2022/2023 imeweza kupanda kwa kasi ya kimbunga kwenye rank za caf, kabla michuano ya Caf aijaanza msimu huu yanga alikuwa nafasi ya 75 kwa ubora barani africa, baada ya kuitoa club africain na kutinga makundi yanga akapanda mpaka nafasi ya 48 kwa ubora, baada ya kutinga robo fainali amepanda mpaka nafasi ya 28 kwenye rank za CAF.

Na iyo ni ndani ya msimu mmoja tu,, sio jambo la kitoto iyo inakuonyesha ni namna gani wako vizuri msimu huu ndani na nje ya uwanja wamejipanga, Siwezi kujua wakifuzu nusu fainali watapanda mpaka nafasi ya ngapi caf ndio wanajua,,kiufupi uwezi kupata mafanikio ya haraka haraka kwenye soka la afrika kama unayo timu ya kuungaunga ni ngumu sana.

Yanga wapewe heshima yao na ninawaona wakifanikiwa zaidi na zaidi kulingana na mipango madhubuti waliyonayo, kile kichaka cha kutofanya vizuri kimataifa naona wanakifyeka mdogo mdogo na wale wasioitakia mema wanaangalia namna nyingine ya kuibua kichaka kingine baada ya hoja iyo kufa kifo cha kawaida,

Kongole wananchi🙌🙌🙌🙌🙏🙏🙏
Sema hatua ya makundi ya NUSU FAINALI.
 
Back
Top Bottom