Yanga bado hatujaweza kutia akili. Tunategemea sana Viongozi wa Kisiasa kutubeba

Ikija tokea kukawa na viongozi ambao hawalalii upande wetu ......TUMEKWISHA. Sasa hivi nachoka hata kuishabikia Yanga baada ya kuona kila jambo tunabebwa na viongozi wa Kisiasa.

Matches zetu zinachezwa hivyo hao TFF wameshaingia woga linapokuja suala letu maana simu zinazopigwa kwao zinawatisha.

Tumebaki kuponda Simba kwenda Dubai na tunasahau jinsi ambavyo tumeaibika na suala la Feisal Toto. Tumetumia nguvu kubwa sana na kuitisha Kamati. Mi nadhani tungemwacha aende zake. Sisi tunaweza pata mchezaji yeyote tumtakaye. Why Fei atutese hivi?

Tumejaribu kumbembeleza hadi kwa mama yake. Tumetumia viongozi wa siasa....anyway hapo tusubiri matunda yake maana naye ni binadamu. Ila kiukweli tunatia huruma. Hatukupaswa kughafirika hivi.

Na bahati mbaya tuna msemaji ambaye naye tumemtoa akili amekuwa kama yule wa Simba Ahmed Ali usemaji wa Kizwazwa kama wa Jamaa ambaye tulimchukua baada ya kufukuzwa Simba na juz juz hapa watu wamemlia mke wake.

Namkumbuka Bumbuli kwa kweli alikuwa anajitahidi kuwa msemaji wa kiweledi mpaka pale naye alipoanza kujichanganya na yule tutusa zeruzeru. Sasa nikafikiri Ally Kamwe atakuwa na weledi kumbe ni takataka zile zile.

Inafikirisha sana haya mateam yetu. Natamani tungempata mtu kama Ezekiel Kamwaga. Alikuwa smart. Yanga sisi watu wa kusemewa ujinga ujinga kweli? Tunaambiwa nchi itasimama kuzinduliwa Yanga TV? Kweli? Mimi nimeitafuta Yanga TV siku ile nzima sijaona....

Ndo maana Fei Toto anatuona sisi watoto wenzie....
Eti Yanga wakati ni kolo kuu
Fatilia yenu huko dubingo
 
Yani mkuu Chizi Maarifa

Hili jina na uwezo wako ni vitu viwili tofauti.

Akili yako ni kubwa mno, ulianzaje kuanza na Neno chizi?????

Kama ingewezekana ungefuta jina la chizi.
 
Back
Top Bottom