EDO KUMWEMBE: Fei, Yanga na Azam wote wameshinda japo wametupotezea muda

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
ILE filamu ambayo ilionekana kutoeleweka hatimaye imemalizika kirahisi. Pengine kuliko tulivyofikiria. Ilionekana kama ingekuwa filamu ngumu bila ya kujua nani angekuwa mshindi. Ilimalizika kirahisi Ikulu ya Magogoni kutoka katika kinywa cha miongoni mwa wanawake wenye nguvu Bara la Afrika.

Pale Mama Samia Suluhu Samia alipoamuru, ingawa mwenyewe alidai kwamba anaomba, kwamba Yanga wakamalizane na mchezaji wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika lile sakata ambalo wote tunalifahamu, ilikuwa wazi kwamba jambo lilikuwa limefika mwisho. Hazikuchukua saa 48 sakata lenyewe likafikia mwisho.

Tulidhani sakata lenyewe lingeenda CAS. Tulidhani sakata lenyewe lingeisha Oktoba baada ya misuguano ya hapa na pale, huku CAS wakihitaji nyaraka mbalimbali kama ilivyokuwa katika sakata la Bernard Morrison. Kumbe sakata lenyewe likamalizika ndani ya saa 48.

Kauli ya Mama ilikuwa amri kwa Yanga. Rais akiomba ujue ameamrisha. Huu ndio ukweli kwa sisi ambao tunafahamu protokali. Yanga hawakuwa na namna zaidi ya kumaliza suala ya Fei bila ya mambo ya kwenda CAS. Hatimaye limalizika.

Limemalizika kwa faida ya pande zote tatu. Kabla ya kusema kila kitu wote tulihisi kwamba klabu ya Azam ilikuwa nyuma ya sakata la Feo Toto. Wengi tulihisi hivyo kwamba Azam ndio klabu ambayo walimhitaji Fei Toto. Lakini tusiwasingizie Azam tu, hata Fei Toto alionekana kuwahitaji Azam.

Ghafla ndani ya saa 48 tangu kauli ya mama itoke, Yanga wakatangaza kumuuza rasmi Fei Toto kwenda Yanga. Nilifurahishwa na namna ambavyo katika taarifa rasmi ya Yanga ilivyotoka hakukuwa na neno lolote ambalo lilimtaja mama.Taarifa iliweka wazi tu kwamba ‘Yanga imefikia makubaliano ya kumuuza Feisal Salum kwenda Azam’. Hakukuwa na mahala kwamba labda walikuwa wamemuachia huru Fei kutokana na kuzingatia kauli ya mama aliyoitoa hivi karibuni.

Kwa hiyo Yanga wakafanya biashara. Kitu cha kwanza tukagundua timu ambayo ilikuwa nyuma ya mkasa wote huu. Kumbe ni Azam. Bahati yetu mpira wetu tunauendesha kisela. Ingekuwa kwa wenzetu kuna uchunguzi mkubwa ungefanyika kujua kama Azam haikuwa timu iliyosimama nyuma kumlaghai Fei kujaribu kuhama timu yake huku akiwa na mkataba halali.

Ashley Cole akiwa na Arsenal aliwahi kukumbwa na mkasa huu. Chelsea walimlaghai. Akapigwa picha na viongozi wa Chelsea katika hoteli fulani pale London, huku akiwa na mkataba na Arsenal. Baadaye Chelsea walipigwa faini kubwa, japo walifanikiwa kumpata mchezaji waliyemtaka.

Pande zote tatu zimeshinda. Tuanze na nani? Fei mwenyewe. Ameshinda na anarudi kucheza soka. Mara kadhaa niliandika hapa kwamba kitu cha muhimu ni kwa Fei kucheza soka. Arudi uwanjani. Iwe katika jezi ya Yanga, sawa. Iwe katika jezi ya Azam, sawa. Iwe katika jezi ya Simba, sawa.

Kama nilivyosema awali, angeweza kwenda CAS na bado kesi yake ingechukua muda mrefu. Kulikuwa na uwezekano wa kuanza msimu mpya bila ya kumuona Fei akicheza soka. Bahati mbaya hatungejua sakata lake lingemalizika vipi.

Tofauti yake na Morrison ni kwamba mwenzake alikuwa ana kesi CAS, huku akicheza soka pale Simba. Kesi ya Fei ni tofauti kwa sababu inaendelea kuwa akiwa hachezi soka. Anafanya mazoezi kwa kujifurahisha tu pale Zanzibar.

Kurudi uwanjani kwake ni kitu muhimu hata kama tunaelewa kwamba alikuwa ana kipato kizuri ingawa alikuwa amegoma kucheza soka. Mara mbili alishindwa kuisaidia Taifa Stars kwa sababu hakuwa fiti uwanjani katika mechi dhidi ya Uganda.

Wengine walioshinda ni Yanga. Najua kwamba walitamani kuwa na Fei. Najua kwamba kama ni kuondoka basi walikuwa wametamani Fei aondoke kwa bei kubwa kuliko ile shilingi 112 milioni aliyoiweka katika akaunti yao hapo awali.

Hata hivyo kauli ya mama ilikuwa amri ambayo wasingeweza kuipuuza. Hapo hapo walijua kwamba Azam walikuwa nyuma ya mchezo wote huu. Wakaamua kuwaita Azam mezani na kufanya mazungumzo. Hatimaye nasikia wamepata kiasi cha Shilingi 270 Milioni kama mauzo ya staa huyo. Sio haba.

Mama hata kama angewaamuru Yanga wamuachie Fei bure basi ingewezekana. Hata hivyo kwa dili lilivyokwenda ni kwamba na wao wameambulia kitu. Kitu ambacho naamini kinawastahili. Vinginevyo labda ni kwamba walikuwa wanataka kumkomoa Fei tu.

Mkataba wa Fei umebakiza mwaka mmoja tu. Ni ngumu kumuuza mchezaji wa Kitanzania anayecheza nchini kwenda katika klabu nyingine nchini kwa dau la Dola 200,000. Sio sawa. Sio haki. Kadri mkataba unavyobakiza muda mfupi ndivyo bei inaposhuka.

Leandro Trossard katika umri wake wa miaka 28 na ubora wake alionao, ameuzwa kwa dau la pauni 25 milioni kwa sababu mkataba wake ulikuwa unaelekea mwisho pale Brighton and Hove. Kama angekuwa na mkataba mrefu angeuzwa kwa zaidi ya pauni 60 milioni.

Upande wa tatu ulionufaika ni Azam. wamempata mmoja kati ya viungo bora kuwahi kutokea nchini. Ingawa imegundulika kwamba Azam walikuwa nyuma ya mpango huu kwa muda mrefu lakini njia ambazo walizitumia hazikuwa sahihi. Hata hivyo wamempata mtu wao.Ni kwa sababu tu Azam ni matajiri lakini naweza kusema kwamba wametumia nguvu nyingi kumpata Fei ingawa wangeweza kutumia msuli mdogo tu. wangeweza kumsubiri Fei mpaka amalize mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao na aondoke bure.

Wangeweza kuingia naye mkataba wa awali na kisha wakamnasa Fei bure. Hata hivyo, wenye pesa huwa hawachaguliwi cha kufanya. kutumia kiasi cha shilingi 270 milioni kwa mchezaji aliyebakiza miezi kumi tu ndani ya soka letu ni jambo lisiloeleweka.

Mwisho wa filamu hii ya Fei tunajifunza kwamba pande hizi zote tatu zimetupotezea muda. Walipaswa kulifanya hili walilofanya mapema zaidi bila ya kusubiri kauli ya Mama. Na inawezekana hata wangekwenda CAS bado wangeweza kurudishwa hapa hapa nchini wauziane mchezaji mwenyewe.

Muda mrefu wazo lilikuwa ni Fei kwenda Jangwani na kuomba kuuzwa. Sijui kwanini alikuwa hafanyi hivi. Labda alikuwa anahofia kwamba Yanga wangepanga dau la kumkomoa. Hata hivyo ukweli ni kwamba angekwenda kwanza halafu Yanga wakapanda dau la kumkomoa hili wote tusimame upande wake dhidi ya Yanga. Hata hivyo kitu cha msingi ni kwamba jambo lenyewe limekwisha na kila upande umepata ulichotaka.

CREDIT: MWANANCHI
 
Ni kwa sababu tu Azam ni matajiri lakini naweza kusema kwamba wametumia nguvu nyingi kumpata Fei ingawa wangeweza kutumia msuli mdogo tu. wangeweza kumsubiri Fei mpaka amalize mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao na aondoke bure.... EDO hizi sio hesabu za soka... yaani kila timu ikimtaka mchezaji basi isubiri mpk Mkataba wk uishe..... kisas kukwepa Gharama.... hayo ni mambo ya Wenger na Flamini.... huo ni ujuha... Soka ni Biashara... kama inakulipa unafanya kwa Njia unayoona inakulipa... Barcelona hawakusubiri CESC amalize Contract yake na Arsenal.... Madrid hawakusubiri BECKHAM amalize contract yake na Man U.... Edo mwenyewe hapo umemtaja Ashley COLE kwenda Chelsea kutokea Arsenal.... Chelsea hawakuhitaji kupoteza muda,,,,,

Anachopaswa kujua Edo....tajiri hapangiwi matumizi ya Pesa zake.... Pale CHAMAZI kila siku kuna Ubwabwa wa Mashabiki kabla ya Mechi.... hiyo ni Pesa yk Tajiri... huwezi kuhoji why anawalisha Ubwabwa...

Iwe Yusuf SSB.... au Azam Fc... huko nyuma washawahi kuwasajili wachezaji kadhaa kutoka Yanga akiwemo NGASSA na DOMAYO.... leo hii ndo wafikirie Mkataba mpk uishe kukwepa gharama.... Edo tuache bana... Fei soon anaenda SSC
 
edo akuache ila na wee tuache kwanza,Simba haikuwahi kumtaka fei,simba zao ni akina sawadogo
 
Fei katusaidia tusijue bandari anaachiwa tukashuhudia mjadala kamilifu wa kibandari.Viva fei umewanyoosha nduguze mzungu.
 
ILE filamu ambayo ilionekana kutoeleweka hatimaye imemalizika kirahisi. Pengine kuliko tulivyofikiria. Ilionekana kama ingekuwa filamu ngumu bila ya kujua nani angekuwa mshindi. Ilimalizika kirahisi Ikulu ya Magogoni kutoka katika kinywa cha miongoni mwa wanawake wenye nguvu Bara la Afrika.

Pale Mama Samia Suluhu Samia alipoamuru, ingawa mwenyewe alidai kwamba anaomba, kwamba Yanga wakamalizane na mchezaji wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika lile sakata ambalo wote tunalifahamu, ilikuwa wazi kwamba jambo lilikuwa limefika mwisho. Hazikuchukua saa 48 sakata lenyewe likafikia mwisho.

Tulidhani sakata lenyewe lingeenda CAS. Tulidhani sakata lenyewe lingeisha Oktoba baada ya misuguano ya hapa na pale, huku CAS wakihitaji nyaraka mbalimbali kama ilivyokuwa katika sakata la Bernard Morrison. Kumbe sakata lenyewe likamalizika ndani ya saa 48.

Kauli ya Mama ilikuwa amri kwa Yanga. Rais akiomba ujue ameamrisha. Huu ndio ukweli kwa sisi ambao tunafahamu protokali. Yanga hawakuwa na namna zaidi ya kumaliza suala ya Fei bila ya mambo ya kwenda CAS. Hatimaye limalizika.

Limemalizika kwa faida ya pande zote tatu. Kabla ya kusema kila kitu wote tulihisi kwamba klabu ya Azam ilikuwa nyuma ya sakata la Feo Toto. Wengi tulihisi hivyo kwamba Azam ndio klabu ambayo walimhitaji Fei Toto. Lakini tusiwasingizie Azam tu, hata Fei Toto alionekana kuwahitaji Azam.

Ghafla ndani ya saa 48 tangu kauli ya mama itoke, Yanga wakatangaza kumuuza rasmi Fei Toto kwenda Yanga. Nilifurahishwa na namna ambavyo katika taarifa rasmi ya Yanga ilivyotoka hakukuwa na neno lolote ambalo lilimtaja mama.Taarifa iliweka wazi tu kwamba ‘Yanga imefikia makubaliano ya kumuuza Feisal Salum kwenda Azam’. Hakukuwa na mahala kwamba labda walikuwa wamemuachia huru Fei kutokana na kuzingatia kauli ya mama aliyoitoa hivi karibuni.

Kwa hiyo Yanga wakafanya biashara. Kitu cha kwanza tukagundua timu ambayo ilikuwa nyuma ya mkasa wote huu. Kumbe ni Azam. Bahati yetu mpira wetu tunauendesha kisela. Ingekuwa kwa wenzetu kuna uchunguzi mkubwa ungefanyika kujua kama Azam haikuwa timu iliyosimama nyuma kumlaghai Fei kujaribu kuhama timu yake huku akiwa na mkataba halali.

Ashley Cole akiwa na Arsenal aliwahi kukumbwa na mkasa huu. Chelsea walimlaghai. Akapigwa picha na viongozi wa Chelsea katika hoteli fulani pale London, huku akiwa na mkataba na Arsenal. Baadaye Chelsea walipigwa faini kubwa, japo walifanikiwa kumpata mchezaji waliyemtaka.

Pande zote tatu zimeshinda. Tuanze na nani? Fei mwenyewe. Ameshinda na anarudi kucheza soka. Mara kadhaa niliandika hapa kwamba kitu cha muhimu ni kwa Fei kucheza soka. Arudi uwanjani. Iwe katika jezi ya Yanga, sawa. Iwe katika jezi ya Azam, sawa. Iwe katika jezi ya Simba, sawa.

Kama nilivyosema awali, angeweza kwenda CAS na bado kesi yake ingechukua muda mrefu. Kulikuwa na uwezekano wa kuanza msimu mpya bila ya kumuona Fei akicheza soka. Bahati mbaya hatungejua sakata lake lingemalizika vipi.

Tofauti yake na Morrison ni kwamba mwenzake alikuwa ana kesi CAS, huku akicheza soka pale Simba. Kesi ya Fei ni tofauti kwa sababu inaendelea kuwa akiwa hachezi soka. Anafanya mazoezi kwa kujifurahisha tu pale Zanzibar.

Kurudi uwanjani kwake ni kitu muhimu hata kama tunaelewa kwamba alikuwa ana kipato kizuri ingawa alikuwa amegoma kucheza soka. Mara mbili alishindwa kuisaidia Taifa Stars kwa sababu hakuwa fiti uwanjani katika mechi dhidi ya Uganda.

Wengine walioshinda ni Yanga. Najua kwamba walitamani kuwa na Fei. Najua kwamba kama ni kuondoka basi walikuwa wametamani Fei aondoke kwa bei kubwa kuliko ile shilingi 112 milioni aliyoiweka katika akaunti yao hapo awali.

Hata hivyo kauli ya mama ilikuwa amri ambayo wasingeweza kuipuuza. Hapo hapo walijua kwamba Azam walikuwa nyuma ya mchezo wote huu. Wakaamua kuwaita Azam mezani na kufanya mazungumzo. Hatimaye nasikia wamepata kiasi cha Shilingi 270 Milioni kama mauzo ya staa huyo. Sio haba.

Mama hata kama angewaamuru Yanga wamuachie Fei bure basi ingewezekana. Hata hivyo kwa dili lilivyokwenda ni kwamba na wao wameambulia kitu. Kitu ambacho naamini kinawastahili. Vinginevyo labda ni kwamba walikuwa wanataka kumkomoa Fei tu.

Mkataba wa Fei umebakiza mwaka mmoja tu. Ni ngumu kumuuza mchezaji wa Kitanzania anayecheza nchini kwenda katika klabu nyingine nchini kwa dau la Dola 200,000. Sio sawa. Sio haki. Kadri mkataba unavyobakiza muda mfupi ndivyo bei inaposhuka.

Leandro Trossard katika umri wake wa miaka 28 na ubora wake alionao, ameuzwa kwa dau la pauni 25 milioni kwa sababu mkataba wake ulikuwa unaelekea mwisho pale Brighton and Hove. Kama angekuwa na mkataba mrefu angeuzwa kwa zaidi ya pauni 60 milioni.

Upande wa tatu ulionufaika ni Azam. wamempata mmoja kati ya viungo bora kuwahi kutokea nchini. Ingawa imegundulika kwamba Azam walikuwa nyuma ya mpango huu kwa muda mrefu lakini njia ambazo walizitumia hazikuwa sahihi. Hata hivyo wamempata mtu wao.Ni kwa sababu tu Azam ni matajiri lakini naweza kusema kwamba wametumia nguvu nyingi kumpata Fei ingawa wangeweza kutumia msuli mdogo tu. wangeweza kumsubiri Fei mpaka amalize mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao na aondoke bure.

Wangeweza kuingia naye mkataba wa awali na kisha wakamnasa Fei bure. Hata hivyo, wenye pesa huwa hawachaguliwi cha kufanya. kutumia kiasi cha shilingi 270 milioni kwa mchezaji aliyebakiza miezi kumi tu ndani ya soka letu ni jambo lisiloeleweka.

Mwisho wa filamu hii ya Fei tunajifunza kwamba pande hizi zote tatu zimetupotezea muda. Walipaswa kulifanya hili walilofanya mapema zaidi bila ya kusubiri kauli ya Mama. Na inawezekana hata wangekwenda CAS bado wangeweza kurudishwa hapa hapa nchini wauziane mchezaji mwenyewe.

Muda mrefu wazo lilikuwa ni Fei kwenda Jangwani na kuomba kuuzwa. Sijui kwanini alikuwa hafanyi hivi. Labda alikuwa anahofia kwamba Yanga wangepanga dau la kumkomoa. Hata hivyo ukweli ni kwamba angekwenda kwanza halafu Yanga wakapanda dau la kumkomoa hili wote tusimame upande wake dhidi ya Yanga. Hata hivyo kitu cha msingi ni kwamba jambo lenyewe limekwisha na kila upande umepata ulichotaka.

CREDIT: MWANANCHI
Kama kweli kauzwa kwa 270M inayotajwa basi hapo tunaongelea 110M ya kuvunja mkataba na faini ya kutoitumikia timu kwa miezi 6. Ila binafsi nadhani ameondoka bure au wamelipa around 160M ikijumuisha gharama za kuvunja mkataba 110M na hiyo faini kama 50M.
 
Back
Top Bottom