Narubongo
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 2,768
- 2,750
kuendelea kuimarika kwa CHADEMA kwa kiasi fulani kutategemea matokeo ya kikao cha NCCR leo!!
- James Mbatia akishindwa na kuondolewa kwenye nafasi yake ya Uenyekiti, kutafanya CHADEMA kuyumba maana Kafulira atakuwa ameshinda. Huyu akishinda, atakuwa amedhihirisha uimara wake kisiasa na ataendeleza chokochoko zake kwenye CHAMA alichotoka na ataendelea kumshawishi Zitto Kabwe ajiunge naye apewe uenyekiti.
- Nafasi ya Uenyekiti NCCR ikiwa wazi; itatumika kama kishawishi cha kuiumbisha CHADEMA hasa Zitto ambaye atashawishiwa kujiunga na NCCR ili mkoa wa Kigoma ugeuzwe kuwa ni Kanda inayomilikiwa na NCCR.
- James Mbatia akishinda katika mgogoro huu na kufanikiwa kuwafukuza baadhi ya wanachama wake, kutakifanya CHADEMA kuvuna wanachama wengi wa NCCR ambao hawatakubaliana na maamuzi. Uwezekano utakuwa ni mkubwa Mkosamali na Kafulira watarudi CHADEMA na kudhaminiwa na chama hicho ktk uchaguzi mdogo ambao bila shaka utawarudisha bungeni kwa tiketi ya CHADEMA na kukifanya chama hicho kuongeza idadi ya Wabunge.
umeandika nini?