Kwenye Mgogoro huu inaonekana dhahiri kuwa Wajumbe wamegawanyika sana, hivi karibuni Msaidizi wa Mwenyekiti Danda Juju ameonekana akimukandia sana Mbatia na Moses Machali kwasababu , MBATIA alimushawishi DANDA amuunge mkono ili amupitishe Kwenye nafasi ya kugombea Ubunge Afrika Mashariki.
Taarifa zinaonyesha kuwa Mbatia aliambiwa na CCM baada ya kushindwa Ubunge Kawe kuwa amufungulie kesi Halima Mdee wa Chadema ili ushindi wa Halima Mdee Utengiuliwe na ukirudiwa CCM itatumia Nguvu zote na kunyakua Jimbo hilo.
Mkataba huo ulikuwa CCM wamupe Ubunge Jemus Mbatia kupitia Afrika Mashariki Kwa hiyo Mbatia anajua kuwa yeye ni Mbunge tayari kupitia Afrika Mashariki, lakini ni lazima ashinde kesi ya Kawe. Gharama zote za kuendesha Kesi hiyo zinatoka CCM na sio NCCR!
Ndani ya NCCR Danda Juju ana jina kubwa Kugombea Ubunge Afrika Mashariki lakini Hawezi kupita kama Mbatia hamuungi Mkono!!!
Danda alifanya Kampeni Mbaya dhidi ya Mbatia kuwambia Wajumbe wa NEC kuwa endapo Mbatia ambaye ni mwenyekiti wa NCCR atakuwa Mbunge kupita Afrika mashariki basi NCCR itakufa kwakuwa watu watasema ni CCM-B.
Mbatia aliposikia njama hizo akakaa kikao na Dr Mvungi wakapatana kwamba ni bora Dr Mvungi au katibu Mkuu Samuel Ruhuza Wakagombea Ubunge Afrika Mashariki na si Danda JUJU.
Huu ndio umafia wa Mbatia na kundi lake na Danda juju anajua hivyo amenoa upanga kumukata Mbatia leo!!!
Hapa ndipo mahali palipo mfanya Mbatia kuagiza watu wanaoitwa Mabonce Kutoka CCM Jeshi ambalo halipo kwenye katiba ya NCCR.
Ndani ya Katiba ya CUF kuna kitengo cha Blue Guard, na Katiba ya CDM kuna kitengo cha Red Brigade na CCM wana Green Gud lakini Ndani ya NCCR hakuna kitengo cha Mabounce lakini kuna kitengo cha VIBARAKA wa CCM wanaofahamika na kulipwa na MBATIA.
Ma-bouncer hao wanalipwa na Mbatia na si NCCR na pesa zote zinatoka CCM.
Sasa kama Kafulila wamevunja katiba kwa kuongea nje ya vikao iweje mtu ambaye amevunja katiba na kuitisha jeshi kutisha mkutano wa Halmashauri kuu?
Hivi unaweza kuwa na Uhuru kulindwa na mtu usiyemjua? Hapa hoja hii naacha kwenu!
Kwa nini asiite polisi?