Yanayojiri mkutano wa NCCR - Disemba 17, 2011

Yanayojiri mkutano wa NCCR - Disemba 17, 2011

Status
Not open for further replies.
Kama Mbatia Kapenya kenye kihunzi hiki na anaendelea kuongoza kikao, naamini wakini kafulila watajuta kumfahamu kibaraka huyu wa CCM. Ni fainali butu kati ya Kibaraka wa CCM (MBATIA) na Kibaraka wa ZITTO (Kafulila)
 
Kama hawafai timulia mbali ruzuku kitu gani? Msikubali kuwa after money kama ccm
 
Wanafiki wakifungiwa chumba kimoja lazima Wanafikiane! Ingawa unafiki wao una malengo tofauti wote Mbatia na Kafulila ni wanafiki tu! Wanafikiana sasa!
 
awajachapana mapanga
kama mpaka sasa wanapiga swaha auwezi kuwa mkutano huo
tusubiri wa cuf
 
watakuwa walishea wanawake wanaombana radhi awana jipya hao
 
Huyu Mwanalugali ni pandikizi la magamba kwa ajili ya kubomoa upinzani. Jina lake sahihi nalijua kabisa.

Mkuu may u give us his/her name? this is the time to deal with these people effectively...even by using mafias ways such of Dr***********
 
Watumie hekima na busara ili wafikie maamuzi yatakayokinufaisha na kukijenga chama chao.
 
Watumie hekima na busara ili wafikie maamuzi yatakayokinufaisha na kukijenga chama chao.
Hekima iliyotumika ni kumfukuza, ameshafukuzwa
Chama cha NCCR mageuzi kimemfukuza uanachama mbunge wake David Kafulila. Kwa uamuzi huo uliofikiwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho muda mfupi uliopita huenda akapoteza kiti cha Ubunge. Salama ya Kafulila kuendelea kuwa mbunge ni kwenda mahakamani au kukata rufaa ngazi ya juu ya chama hicho. Hatua hiyo itategemea uharaka wa chama chake kutoa taarifa rasmi kwa Spika wa Bunge, msajili wa vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi kutangaza kiti hicho kuwa wazi.
Habari kutoka ndani ya mkutano huo kinaeleza kwamba pande zote mbili kwa sasa kila mmoja unapanga mikakati ya kuwahi mahakamani jumatatu asubuhi. Upande wa chama hicho kinachoongozwa na James Mbatia wanakusudia kufungua kesi ya kumzuia Kafulila kuendelea kukishambulia chama hicho baada ya kufukuzwa uanachama pamoja na kumtaka atumie taratibu za kikatiba za chama hicho ikiwapo anataka kukata rufaa. Upande wa Kafulila unaelezwa kuwa umedhamiria kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa uanachama ikihoji uhalali wa mkutano huo na taratibu zilizotumika kumuondoa uanachama.
Awali mkutano huo ulitawaliwa na vuta nikuvute kuhusu taarifa ya mkutano huo, huku upande wa Kafulila ukiwakilishwa na Hashim Rungwe ukikutana na Msajili wa Vyama vya siasa kupinga mkutano huo kuitishwa kwa dharura na kutaka makabrasha ya mkutano kufika majumbani kwa wajumbe kabla ya mkutano. Hata hivyo, baada ya kupitia katiba ya chama hicho msajili hakuona msingi wa kuzuia mkutano huo wa dharura kufanyika.
Kabla ya mkutano huo kuendelea mwakilishi mwingine wa Kafulila ambaye ni mbunge mwenzake toka Kigoma wa Jimbo la Muhambwe Felix Mkosamali aliweka pingamizi lingine kuhusu wajumbe ambao walielezwa kuwa pandikizi. Hata hivyo, msajili wa vyama vya siasa alitoa orodha ya wajumbe waliopo katika ofisi yake yake ambao ilikuwa na majina ya wajumbe hao. Vyanzo kutoka makao makuu ya NCCR Mageuzi vinaeleza kwamba baada ya mgogoro kuanza Mbatia alitumia mamlaka yake ya katiba kuteua wajumbe hao na kutoa taarifa kwa msajili wa vyama vya siasa. Hata hivyo upande wa Kafulila haukuwa unafahamu kuhusu wajumbe hao wapya hali ambayo ilileta mzozo katika ukumbi huo.
Katika eneo la ukumbi walionekana walinzi wa chama hicho wakivinjari, lakini kutokana na mzozo huo Hashim Rungwe alitoa taarifa polisi ambao walifika kwa wingi na kukuta tayari walinzi hao wamewatuliza wajumbe wa mkutano na kikao kinaendelea.
Habari ndani ya ukumbi wa mkutano huo zinaeleza kwamba mara baada ya ufunguzi wajumbe walijadili taarifa ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tuhuma zinazomkabili Mbatia. Kutokana na barua ya kumtaka ajiuzulu iliyosainiwa na kundi la Kafulila ilibidi halmashauri kuu ya NCCR Mageuzi impe nafasi mwenyekiti ajieleze. Kutokana utetezi huo wajumbe walipiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti ambao wajumbe 42 walipiga kura ya kuwa na imani wakati wajumbe 9 walipiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti.
Baada ya wajumbe wengi kuonyesha kuwa na imani na mwenyekiti mkutano uliamua kujadili kuhusu waliowasilisha tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti wa kiongozwa na Kafulila. Kila mjumbe aliulizwa msimamo wake baada ya kura hizo na Kafulila alieleza kwamba naye ana imani kubwa na mwenyekiti. Kutokana na kauli hiyo kutofautiana na barua aliyoandika kwa wajumbe pamoja na ushahidi wa magazeti mkutano ulimuhoji kufafanua na alisisitiza kwamba ana imani na mwenyekiti isipokuwa magazeti yamekuwa yakimnukuu vibaya. Aidha Kafulila asisitiza kwamba barua ya kujiuzulu mwenyekiti haikuwa ya madai ya kutokuwa na imani naye bali ni changamoto kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
Mkutano uliamua kuwatoa wajumbe wenye tuhuma mbalimbali kwa ajili ya kuwajili ambao wajumbe kwa kauli moja waliona kwamba ipo haja ya kuwapa adhabu ya kuwavua nafasi mbalimbali za uongozi. Hata hivyo, wakati kikao kikiendelea likaja kundi lingine la askari polisi ambao walieleza kwamba wamepigiwa simu na Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzuia vurugu zilizokuwa zikiendelea katika mkutano huo. Kutokana na madai hayo, mkutano huo ulilazimika kumuita tena Kafulila na Hashim Rungwe ambao walitajwa kuwapokea askari hao kueleza msingi wa kuhusisha vyombo vya dola na watu wa nje wa chama hicho katika mkutano wa ndani wa chama hicho.
Baada ya kuitwa kwa mara ya pili mbunge wa Kasulu Aggripina Buyogela aliwaomba radhi wajumbe kuhusu uasi huo kutoka katika mkoa wa Kigoma kwa kuwa Kafulila, Rungwe, Mkosomali na Machali wote wanatoka katika mkoa mmoja na yeye. Aggripina aliwaomba wajumbe kutoa adhabu inayostahili bila kutazama mkoa kwa kuwa si watu wote wa mkoa ni wakosaji ili kudumisha nidhamu katika chama.
Kufuatia kauli hiyo Kafulila akaongezewa mashtaka mengine ya kutoa tuhuma kwa viongozi wenzake na chama kupitia vyombo vya habari badala ya vikao vya chama. Kafulila alidaiwa kufanya vitendo hivyo hata baada ya kuonywa na katibu mkuu wa chama hicho. Baada ya kusikiliza utetezi wake ndipo wajumbe walipiga kura ya kumfukuza uanachama kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama hicho huku wajumbe 8 wakiacha kupiga kura.
Kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyu kumeendeleza wimbi la wabunge kufukuzwa na vyama vyao toka mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Miaka michache iliyopita walifukuzwa wabunge wa viti maalum wa CUF ambao hata hivyo walishinda kesi na kuendelea kuwa wabunge kwa amri ya mahakama kutokana na chama hicho kutokufuata taratibu. Wabunge wengine waliofukuzwa ni wa majimbo wa chama cha UDP ambao kutokana na katiba ya chama hicho kufuatwa walipoteza nafasi za ubunge wao licha ya kwenda mahakamani.
Kafulila alihamia NCCR Mageuzi baada ya kuvuliwa cheo cha uafisa habari wa CHADEMA. Kufuatia hali hiyo aliamua kujivua uanachama na kujiunga na CHADEMA na kuungwa mkono na Zitto Kabwe na hatimaye kushinda uchaguzi wa Kigoma Kusini. Wakati wa uchaguzi na mara baada ya uchaguzi gazeti la Mwanahalisi limekuwa likitoa mfululizo wa habari zikinukuu mawasiliano ya barua pepe baina ya wanasiasa hao vijana machachari zikieleza mpango wa kuichukua NCCR Mageuzi ili kujenga chama kitakachokuwa makini zaidi ya CHADEMA kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani mwaka 2015. Kutokana na habari hiyo vyombo vingine vya habari vimekuwa vihusisha mgogoro wa NCCR Mageuzi na suala hilo hali iliyopelekea wanasiasa hao kukanusha. Hata hivyo, Mbunge mwingine wa NCCR Mageuzi Machali alijitokeza karibuni na kuthibitisha madai hayo huku akidai kuwa ana ushahidi wa mawasiliano yake na Kafulila yenye kuonyesha kwamba alimshawishi kushiriki katika mpango huo.
PM
 
Jamani nilisema anayemuweza MBATIA ni Halima Mdee binti Chadema peke yake lakini hakuna mwingine. Pamoja na kwamba Mbatia ni sumu katika mabadilko ya Tanzania lakini Kafulila ni kirusi klibaya sana. Alijisemea Dr. Slaa kuwa huyu ni sisimizi Mbatia akaona amepata jembe kweli kweli.

Sasa Kafulila na washirika wake waliokua nje ya NCCR waangalie jinsi ya kuiibua DP ya mtikila ama UDP ya Cheyo vinginevyo safari ya siasa kwao kushneyi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom