kuendelea kuimarika kwa CHADEMA kwa kiasi fulani kutategemea matokeo ya kikao cha NCCR leo!!
- James Mbatia akishindwa na kuondolewa kwenye nafasi yake ya Uenyekiti, kutafanya CHADEMA kuyumba maana Kafulira atakuwa ameshinda. Huyu akishinda, atakuwa amedhihirisha uimara wake kisiasa na ataendeleza chokochoko zake kwenye CHAMA alichotoka na ataendelea kumshawishi Zitto Kabwe ajiunge naye apewe uenyekiti.
- Nafasi ya Uenyekiti NCCR ikiwa wazi; itatumika kama kishawishi cha kuiumbisha CHADEMA hasa Zitto ambaye atashawishiwa kujiunga na NCCR ili mkoa wa Kigoma ugeuzwe kuwa ni Kanda inayomilikiwa na NCCR.
- James Mbatia akishinda katika mgogoro huu na kufanikiwa kuwafukuza baadhi ya wanachama wake, kutakifanya CHADEMA kuvuna wanachama wengi wa NCCR ambao hawatakubaliana na maamuzi. Uwezekano utakuwa ni mkubwa Mkosamali na Kafulira watarudi CHADEMA na kudhaminiwa na chama hicho ktk uchaguzi mdogo ambao bila shaka utawarudisha bungeni kwa tiketi ya CHADEMA na kukifanya chama hicho kuongeza idadi ya Wabunge.
Mbatia ameshinda kwa nguvu za Mabounce waliopo nje!!!
Ukiona Mkutano wa NCCR unaongozwa na Mabonce ujue hapo Mbatia anabakia katika nafasi ya Uenyekiti kwa nguvu za Mabounce ambao ni Majambazi !!!
Hapa hakuna deomokrasia ya kweli na wala Mbatia hawezi kudai Tume huru na katiba mpya kwa kuwa uchaguzi unao muweka madarakani sio huru!!!
Kura ya mtu ni siri kwa nini amelazimisha kuweka wazi???
Kushinda Kwa Mbatia katika nafasi ya Uenyekiti hakumaanishi anakubalika.!!!
Kumbuka Jakaya Kikwete ameingizwa madarakani kwa Nguvu za vyombo vya dola , lakini unaona anavyo yumba???
Leo Kikwete akigombea Ubunge jimbo la Ubungo , John Mnyika anaweza kumushinda Kwa asilimia 90!!!
Hapa ukweli ni kwamba Mbatia hana Uhalali wa kuitwa Mpinzani na wala hawezi kuungana na CHADEMA kuzunguzan kama mpinzani!!!
Mbowe amewafukuza Wabunge wa NCCR kwenye kambi ya Upinzani kwa sababu ya Mbati kuwa Kibaraka wa CCM!!!
Hivi nini hatima ya NCCR na MBATIA???