Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Wewe siyo mungu u
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Ndani ya Chadema kuna makundi mawili, wako wanaojitambua, na wasio jitambua. Wanaojitambua wakiisha gundua Chadema ipo ipo tuu na haina mpango wowote wala uwezo wa kushika dola, wanajiongeza na kutimka zao kujiunga na chama dola. Wasio jitambua wanaendelea kuishi kwa matumaini ila baada tuu ya Bunge kuvunjwa, kutatokea mass exodus, waliobakia ni wale wagumu kama wewe ambao mnajitambua na mnajua kabisa kuwa Chadema hivi ilivyo, kamee haiwezi kuja kushika dola, ila mnaendelea kuwepo kuonyeshea msimamo usio yumba, baada ya 2020, mnakwenda nayo chini!.
P
Pascal unazi wa ccm umekumaliza kabisa!
 
Asante Mkuu Yohane Mbatizaji, ukiwaambia ukweli mchungu hawa jamaa zetu wanaoishi kwenye ndoto za mchana za kuiota Ikulu, ukiwaambia hizi ni ndoto tuu za mchana kweupe, wanakasirika.
Ukweli ni kuwa NEC, ni Tume huru ila sio Shirikishi.
P
Ikitokea wameshika dola itakuaje
 
Kwenye hoja hii
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Sikumzungumzia kisiasa, nilizungumzia matumizi ya ukwasi wake to Chadema advantage, very unfortunately it didn't work out.

2015 ilikuwa Chadema ichukue nchi, ikakwamishwa na kitu kimoja tuu kidogo, reaching out mechanisms to the grassroots movement kutokana na Chadema kutokuwa na media zake. Sasa ni 2020, uchaguzi mwingine ndio huo just around the corner, matukio ya mass mobilization ndio haya, na media yenyewe ndio hawa kina Molemo wanafanya kusaidia tuu, unategemea nini?!.
P
Hovyo; mbona uhalali wa matokeo ya uchaguzi 2015 haujawekwa wazi?
 
Wewe siyo Mungu
Pascal unazi wa ccm umekumaliza kabisa!
Mungu ni Mungu na binadamu ni binadamu, hakuna mtu yoyote anayejifanya Mungu, na ninachofanya mimi ni kuwasomea tuu political trends za kuelekea 2020 zinaonyesha Chadema ikielekea ukingoni.

Hili la unazi wa CCM ni maoni yako na nayaheshimu.
P
 
Usiwe watovu wa shukrani, naamini Lowassa alikuja Chedema kwa nia njema ya kusaidia na kiukweli amewasaidia sana!, mgombea gani wa Chadema angeweza kupata kura zaidi ya milioni 6?.

Hoja ya binaadamu yoyote atakufaje, iko nje ya uwezo wetu, sio mimi, sio wewe wa kusema, ni Mungu tuu pekee!.
P

Lowasa ni kweli alipeleka hamasa kubwa ndani ya Chadema lakini ni naamini Dr. Slaa alikuwa anauwezo wa kuvunja hiyo record ya Lowasa ya kura 6m
 
Katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, nahisi hii itakuwa "photo shop" si bure.
tapatalk_1583684591807.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ukuta wa Saka, kwanza naheshimu mawazo yako kuhusu shallow analysis ya ujio wa Lowassa Chadema. Mtu asiye na shukrani kwa madogo, hawezi kubarikiwa makubwa. Nimeuliza bila Lowassa, Chadema ingepata kura zaidi ya milioni 6!. Unajua Chadema imepata wabunge wangapi kwa ujio wa Lowassa?. Unajua hao wabunge wanaingiza ruzuku kiasi gani Chadema?.

Politics is a science and a game yenye malengo. Japo Lowassa aliingia Chadema kuitafuta fursa ya kuingia Ikulu, baada ya kukosekana, it was his right kurejea, ila alipokuja, hakuja mikono mitupu, he brought something, Chadema aliyoikuta sio Chadema aliyoiacha!. Mimi nimehudhuria mkutano Mkuu wa Chadema enzi hizo unafanyikia ukumbi wa Kiramuu, hadi sasa Chadema wanakodi ukumbi Mlimani City!. Nyinyi manazi wa Chadema ndio hamna shukrani na Lowassa lakini Mbowe anamheshimu na anamshukuru mpaka kesho!.
P

Kwa hili uko yawezekana uko sahihi lakini pia sio uhalali wa kukufanya uamini kuwa ndiyo ilikuwa hali halisi..ukumbuke katika kipindi ambacho lowasa anajiunga cdm tayari ccm ilikuwa imeshapoteza Imani na mbili kwa wananchi kwa hiyo kwa namna yoyote ile lazima Chadema walikuwa wanavuna kura nyingi sana na sio ni kwa sababu ya ujio wa lowasa,na pia kitu ambacho haujaribu kukiwaza ni kwamba kwa ujio wa lowasa cdm na kumtosa dr.slaa kumewapunguzia cdm kura nyingi sana kutokana na kwamba tayari cdm kupitia dr slaa watu walipata kuhamasika sana na hivyo alivyoshuka lowasa ilimnufaisha sana magufuli kutokana na ukweli kwamba lowasa alikuwa ameshachafuka sna.
 
Mkuu J Mushi, nyomi nimeiona, na huu ni mwaka wa uchaguzi, nikidhani sasa Chadema watahutubia issues serious kuhusu a way forward, lakini naona bado Chadema wanaendelea na siasa zile zile za matukio.

Mtu anayezijua siasa za nchi hii kuelekea uchaguzi Mkuu akisikiliza hizo hoja 5 za Mwenyekiti, akisema Chadema hamna sera, mmeishiwa hoja, what are you standing for, ni hakuna, atakuwa anawaonea?.

Gap ya Chadema kutokuwa na watu ma strategists kama Zitto na Kitila, is very visibly seen!.



..hotuba ya Mh.Halima Mdee inatoa mwanga zaidi kuhusu dhima nzima ya mkutano wa bawacha.

..sikiliza hotuba ya Mh.Mdee hapa.



cc tindo
 
Kwenye mahesabu ya chama itaonekana vimenunuliwa vitenge 1000 kwa ajili ya sare za kina mama wa Bavicha!
Chadema hakuna mambo ya kijinga kwa level hiyo kama CCM.
Vitenge kila MTU kajinunulia kwa mapenzi yake na nauli kajilipia sio kuletwa na malori.
Ukiangalia picha hii utajua mengi tofauti ya UWT na Bavicha, kama unajuwa kusoma picha
mdudechadema___B9PDMorgfY2___.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine ya kijinga sana. Yaani wakati ule wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA walikodi huo ukumbi kwa siku 11 kwa shilingi milioni 110 leo kwa siku moja wanakodije kwa shilingi milioni 230!!?

Hivi nyie watu ni nani aliyewaloga hadi kuamini kila mnachoambiwa na CCM?
Kama katibu mkuu wao ana PhD lakini hamnazo, unadhani hawa mavuvuzela watakuwaje?
Nikuwaacha tuu bila kuwajibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom