Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

"
Pascal Mayalla, post: 34594309, member: 17813"]kitendo cha kukubali Chadema kutokuwa na media yake ni kosa kubwa la kiufundi, kutambua tuu hili ni plus, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa.
Ni makosa yaliyofanywa kuanzia enzi za Dr Slaa.
JF walishauri na hoja ikawa, nini kinachoshindikana ikiwa mtu binafsi anaweza kuwa na media?

Kushindwa kuwa na media siku za nyuma kunazaa tatizo jingine.

Katika zama hizi ambazo Taasisi za umma zimegeuka kuwa 'matawi ya chama chenye dola'' kwa mujibu wa kauli za Katibu mkuu wa CCM, Dr A.Bushiru, sijui media inaweza kutangaza zaidi ya saa 24 kabla katibu mkuu wa CCM hajaiagiza TCRA kufanya yake.Maria Sarungi anaweza kuwa shahidi wa hili.
NEC ni Tume huru ila sio Shirikishi. Kwa mujibu wa katiba na sheria iliyounda Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ni Tume huru, independent, ila sio Shirikishi in a sense that watendaji wote wanaweza kuwa ni makada hivyo kufumbia macho huu uwanja tenge wa ushindani wa kusiasa usio ushindani wa haki.
NEC si tume huru kwa vigezo vyovyote vile vya kitaifa na kimataifa.

Arguably,ni chombo halali kwa mujibu wa sheria. Kuwa chombo halali hakuifanyi NEC kuwa huru.

Kuna tofauti ya kuwa chombo huru na chombo halali. Unachozungumzia ni chombo halali kwa mujibu wa sheria.

Kutamkwa kikatiba kwa NEC kuwa chombo huru hakuifanyi NEC iwe huru.

Chief justice Heart alisema ''Not only justice must be done, but also seen done''

Msingi wa hoja hiyo ni kuwa sheria itendwe na kuonekana imetendwa bila kuacha chembe ya shaka.
Kwamba kusiwe na mazingira yanayotiliwa shaka na mtoaji wa haki ambaye ni ''Hakimu''

Maana yake ,NEC kuwa huru ni sehemu tu ya ''mtoa justice'' lakini uwepo wa mashaka juu ya uhuru wa tume unafanya 'ipoteze uhalali .Kuna mifano mingi ya kutilia shaka kuhusu NEC isiyopingika

1. NEC inateuliwa na mgombea wa CCM. Kwamba 'refa' wa mchezo wa Yanga na Simba anachaguliwa na Yanga. Tuliona Kikwete akibadilisha wajumbe wiki moja kabla ya uchaguzi.

2. Matukio kama ya kufutwa wagombea , mbinu za Wakurugenzi kjificha kupokea fomu uyaliyopelekea mauti ya Aqulina hayakukemewa na NEC kwasababu kuna ''collusion' na kwamba NEC ni tawi la chama tawala

3. Sanduku la kura la NEC linachukuliwa na Wahuni kisha kurudishwa, NEC na Polisi wakiwa wanatazama.

4. Muulize Maalim Seif na Jecha aliybanwa tumbo la kuhara kisha kupona akiwa TV Zanzibar

Ukiororedhesha makosa ya NEC ya mkusudi, hata mtu aliye kijijini anajua hii si tume huru kwa namna yoyote.
The political playground is not level, uchaguzi wetu ni mechi ya kugombea kisu cha makali kuwili, huku mgombea mmoja ameshika kwenye mpini akionyeshea kwenye makali ndipo waanze kuvutana.
Ndiyo maana nashwashanga akina Mbatia wanaokwenda kusimika Wagombea.

Hivi utashinda vipi ikiwa CCM wana Polisi, NEC, Usalama ,Wakurugenzi, DC n.k?
Hivi hili linahitaji certificate kulibaini ukweli huu. Nani anaweza kushindwa akiwa na msaada huo!

UVCCM wanasema ''fulani auawe'' hadharani, lini umemsikia Msajili wa vyama!
Msajili hawezi kukemea UVCCM halafu unatagemea utashinda uchaguzi!
Tunaingia kwenye uchaguzi Mkuu huru na wa haki huku chama kimoja ni chama dola, kina Tume, wasimamizi, polisi, jeshi, huku mgombea mmoja akizunguka kufanya kampeni kwa ving'ora, supported by state machinery, state cars, state media, state resources, akishindana na mgombea mwingine mwenye nothing!, halafu huyu mwenye nothing ategemee kushinda?!, angalau kama huyu mgombea with nothing angekuwa ame invest on people!, but he is not!, unategemea nini?, bora wanaojitambua, waacheni tuu waende!.
Halafu wanatafutwa kutiwa pingu kila siku.Imefika wakati DC anaamua Wapinzani waongee nini katika mikutano.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulionyesha nini kinafuata.
Kama kutakuwa na Wapinzani 3 bungeni, hao ni Lipumba, Mbatia na mwingine kutoka chama cha mfukoni.

Kwenda katika uchaguzi kwa NEC iliyopo ni kwenda kuhalalisha matokeo ya 99%

Na kwa kujua shinikizo la kimataifa , kususia uchaguzi kunatisha, sasa wanaitwa mmoja mmoja kivyake.

Hakuna uchaguzi , watu wasijidanganye. Bushiru Ally, Katibu mkuu wa CCM kasema wazi wao wanamsaada wa vyombo vya dola, hivi mnahitaji nani azungumze muamini?

tindo JokaKuu
 
" Ni makosa yaliyofanywa kuanzia enzi za Dr Slaa.
JF walishauri na hoja ikawa, nini kinachoshindikana ikiwa mtu binafsi anaweza kuwa na media?

Kushindwa kuwa na media siku za nyuma kunazaa tatizo jingine.

Katika zama hizi ambazo Taasisi za umma zimegeuka kuwa 'matawi ya chama chenye dola'' kwa mujibu wa kauli za Katibu mkuu wa CCM, Dr A.Bushiru, sijui media inaweza kutangaza zaidi ya saa 24 kabla katibu mkuu wa CCM hajaiagiza TCRA kufanya yake.Maria Sarungi anaweza kuwa shahidi wa hili. NEC si tume huru kwa vigezo vyovyote vile vya kitaifa na kimataifa.

Arguably,ni chombo halali kwa mujibu wa sheria. Kuwa chombo halali hakuifanyi NEC kuwa huru.

Kuna tofauti ya kuwa chombo huru na chombo halali. Unachozungumzia ni chombo halali kwa mujibu wa sheria.

Kutamkwa kikatiba kwa NEC kuwa chombo huru hakuifanyi NEC iwe huru.

Chief justice Heart alisema ''Not only justice must be done, but also seen done''

Msingi wa hoja hiyo ni kuwa sheria itendwe na kuonekana imetendwa bila kuacha chembe ya shaka.
Kwamba kusiwe na mazingira yanayotiliwa shaka na mtoaji wa haki ambaye ni ''Hakimu''

Maana yake ,NEC kuwa huru ni sehemu tu ya ''mtoa justice'' lakini uwepo wa mashaka juu ya uhuru wa tume unafanya 'ipoteze uhalali .Kuna mifano mingi ya kutilia shaka kuhusu NEC isiyopingika

1. NEC inateuliwa na mgombea wa CCM. Kwamba 'refa' wa mchezo wa Yanga na Simba anachaguliwa na Yanga. Tuliona Kikwete akibadilisha wajumbe wiki moja kabla ya uchaguzi.

2. Matukio kama ya kufutwa wagombea , mbinu za Wakurugenzi kjificha kupokea fomu uyaliyopelekea mauti ya Aqulina hayakukemewa na NEC kwasababu kuna ''collusion' na kwamba NEC ni tawi la chama tawala

3. Sanduku la kura la NEC linachukuliwa na Wahuni kisha kurudishwa, NEC na Polisi wakiwa wanatazama.

4. Muulize Maalim Seif na Jecha aliybanwa tumbo la kuhara kisha kupona akiwa TV Zanzibar

Ukiororedhesha makosa ya NEC ya mkusudi, hata mtu aliye kijijini anajua hii si tume huru kwa namna yoyote.
Ndiyo maana nashwashanga akina Mbatia wanaokwenda kusimika Wagombea.

Hivi utashinda vipi ikiwa CCM wana Polisi, NEC, Usalama ,Wakurugenzi, DC n.k?
Hivi hili linahitaji certificate kulibaini ukweli huu. Nani anaweza kushindwa akiwa na msaada huo!

UVCCM wanasema ''fulani auawe'' hadharani, lini umemsikia Msajili wa vyama!
Msajili hawezi kukemea UVCCM halafu unatagemea utashinda uchaguzi! Halafu wanatafutwa kutiwa pingu kila siku.Imefika wakati DC anaamua Wapinzani waongee nini katika mikutano.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulionyesha nini kinafuata.
Kama kutakuwa na Wapinzani 3 bungeni, hao ni Lipumba, Mbatia na mwingine kutoka chama cha mfukoni.

Kwenda katika uchaguzi kwa NEC iliyopo ni kwenda kuhalalisha matokeo ya 99%

Na kwa kujua shinikizo la kimataifa , kususia uchaguzi kunatisha, sasa wanaitwa mmoja mmoja kivyake.

Hakuna uchaguzi , watu wasijidanganye. Bushiru Ally, Katibu mkuu wa CCM kasema wazi wao wanamsaada wa vyombo vya dola, hivi mnahitaji nani azungumze muamini?

tindo JokaKuu

Nashukuru sana kwa huu ufafanuzi mujaribu kwa huyo Paskali anayedhani watu hatujui lolote.

Cc: GuDume
 
Mkuu J Mushi, nyomi nimeiona, na huu ni mwaka wa uchaguzi, nikidhani sasa Chadema watahutubia issues serious kuhusu a way forward, lakini naona bado Chadema wanaendelea na siasa zile zile za matukio.

Mwenyekiti Mbowe amezungumzua mambo makubwa matano.

Jambo la kwanza ni Ziara ya viongozi wa kisiasa Ikulu. Hili ni tukio.

Jambo la Pili, Mwenyekiti Mbowe amezungumzia Barua kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa kwenda kwa vyama vyote kuhakiki uhai wao ili kutambua vyama vinavyostahili kushiriki uchaguzi. Hii ni hoja ya kiutendaji.

Jambo la Tatu, Mwenyekiti Mbowe amelaani vikali Tabia inayoshamiri ya watu wachache kutaka kutumia Ukabila kuligawa Taifa. Hili ni tukio.

Jambo la nne, Mbowe amezungumzia ushirikiano wa vyama na kusema chana chake kinathamini sana ushirikiabo na kitakuwa tayari kushirikiana na chama chochote chenye nia thabiti ya kulikomboa Taifa- hapa pekee ndio hoja ya msingi na ya maana, lakini bila kusema how, pia ni empty!.

Jambo la tano, Mbowe alikemea vikali kauli ya hatari na ya kibabe iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally kwamba chama chake kitatumia Dola kushinda uchaguzi. Hili ni tukio.

Hizi siasa za matukio zitaifikisha wapi Chadema, wanawake ndilo kundi kubwa la wapiga kura, lini Chadema mtafanya mkutano na kuleta your own agendas na sio kuja kuhutubia kuhusu matukio, badala ya Chadema kuwa pro active kwa kutoa hoja zake, Chadema kazi yake ni kujibu tuu hoja za matukio.

Mtu anayezijua siasa za nchi hii kuelekea uchaguzi Mkuu akisikiliza hizo hoja 5 za Mwenyekiti, akisema Chadema hamna sera, mmeishiwa hoja, what are you standing for, ni hakuna, atakuwa anawaonea?.

Gap ya Chadema kutokuwa na watu ma strategists kama Zitto na Kitila, is very visibly seen!.

P
Unaposema “siasa za matukio”, ina maana haufahamu kuwa hayo matukio yana impact kwa wapiga kura? Au unadhani hayo matukio hayana madhara yoyote kwenye jamii yenye kufuata mfumo wa kidemokrasia?
 
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Ndani ya Chadema kuna makundi mawili, wako wanaojitambua, na wasio jitambua. Wanaojitambua wakiisha gundua Chadema ipo ipo tuu na haina mpango wowote wala uwezo wa kushika dola, wanajiongeza na kutimka zao kujiunga na chama dola. Wasio jitambua wanaendelea kuishi kwa matumaini ila baada tuu ya Bunge kuvunjwa, kutatokea mass exodus, waliobakia ni wale wagumu kama wewe ambao mnajitambua na mnajua kabisa kuwa Chadema hivi ilivyo, kamee haiwezi kuja kushika dola, ila mnaendelea kuwepo kuonyeshea msimamo usio yumba, baada ya 2020, mnakwenda nayo chini!.
P
Mengine ni vigumu kuyapita hivi hivi..
.
Unajichanganya.

Kuna makundi mangapi ya "Wanaojitambua" ndani ya CHADEMA?

Kundi hilo la mwisho pekee, ndio wanaojitambua.

CCM imefanya kazi nzuri sana ya kuisafisha CHADEMA iende mbele ikiwa imara zaidi.
 
Mungu Akubariki sana kwa ukweli huu ulioandika
 
" Ni makosa yaliyofanywa kuanzia enzi za Dr Slaa.
JF walishauri na hoja ikawa, nini kinachoshindikana ikiwa mtu binafsi anaweza kuwa na media?

Kushindwa kuwa na media siku za nyuma kunazaa tatizo jingine.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulionyesha nini kinafuata.
Kama kutakuwa na Wapinzani 3 bungeni, hao ni Lipumba, Mbatia na mwingine kutoka chama cha mfukoni.

Kwenda katika uchaguzi kwa NEC iliyopo ni kwenda kuhalalisha matokeo ya 99%

Na kwa kujua shinikizo la kimataifa , kususia uchaguzi kunatisha, sasa wanaitwa mmoja mmoja kivyake.

Hakuna uchaguzi , watu wasijidanganye. Bushiru Ally, Katibu mkuu wa CCM kasema wazi wao wanamsaada wa vyombo vya dola, hivi mnahitaji nani azungumze muamini?

tindo JokaKuu
Mkuu Nguruvi3, kwanza asante kwa hili bandiko, mimi naliita bandiko shule.
Naomba nitoe fursa tuendelee kupata nondo za siku ya wanawake duniani kwa wanawake wa Chadema.
Kwa upande wangu, matokeo ya uchaguzi Mkuu wa October, kwa mujibu wa Bashiru, tayari nayajua ni haya

Elections 2020 - Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!
P
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza asante kwa hili bandiko, mimi naliira bandiko shule.
Naomba nitoe fursa tuendelee kupata nondo za siku ya wanawake duniani kwa wanawake wa Chadema.
Kwa upande wangu, matokeo ya uchaguzi Mkuu wa October, kwa mujibu wa Bashiru, tayari nayajua ni haya

Elections 2020 - Kukubalika kwa Rais Magufuli/CCM: Kishindo cha asilimia 99.9% ni mawingu tu ya dalili, mvua ni 2020, ni lele tu, ngoma ni 2020!
P
Mkuu tuwapongeze wakina-mama duniani kwa kuadhimisha siku yao.

Pili, kama ulivyosema matokeo ni 99.99% CCM. Uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa ni prelude na rehearsal ya 2020.

Nina washangaa sana akina Mbatia na Maalimu Seif aliyesema ''kususa ni kumwachia nguruwe shamba la mihogo''
Kufanya jambo lile lile kwa namna zile zile na kutopata matokeo tofauti inaitwa ''insanity'

Katibu mkuu wa CCM kasema ''CCM inafaidika kwa kuwa chama chenye dola'' na tunajua dola inaundwa na nini.
Bushiru ni mkweli na muwazi kwamba itakuwa ujinga 'imbecile'' kushidwa uchaguzi wakiwa na kila msaada ikiwemo NEC

Nilipomshangaa Bushiru ni pale alipomjibu Membe kwamba kama tatizo ni Urais, basi aingie katika kinyangang'anyiro.
Yaani alitufanya Watanzania mazuzu kwamba tuna ''uchaguzi'' na kwamba hatujui CCM inashindaje uchaguzi.

Katika uwanja sawa wa CCM inaondoka. Hilo hata CCM wanalijua ndiyo maana wanatunia kila ''zana' waliyonayo.

CCM wanapokataa tume ya uchaguzi wanajua wazi kuifanyia marekebisho ni kukata mikono yao.

CCM wanapotumia Polisi wanajua wanafanya nini. CCM wana kila msaada wa dola (Bushiru)

Ni wazuri sana , baada ya kubanwa na wakubwa wameamua kuwaita ''Wapi-nzani'' mmoja mmoja kivyake.

Nina wasikia hao wapinzani wakijiandaa kwa uchaguzi, sijui wanajiandaa na nini ikiwa Bushiru keshawaeleza wazi
 
Mkuu Nguruvi3, Watanzania ni wazito kuelewa, hili mimi nimelieleza tangu ile 2014 nilisikia tuu kuwa mgombea wa CCM ni Magufuli, nilipandisha bandiko hili na humo nikaeleza what to expect from him
Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Na baada tuu ya uchaguzi, nilipandisha bandiko hili
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
nikizungumzia uchaguzi mkuu wa 2020.
Tuendelee na maandalizi ya Igizo la Uchaguzi!.
P
 
Mkuu J Mushi, nyomi nimeiona, na huu ni mwaka wa uchaguzi, nikidhani sasa Chadema watahutubia issues serious kuhusu a way forward, lakini naona bado Chadema wanaendelea na siasa zile zile za matukio.

Mwenyekiti Mbowe amezungumzua mambo makubwa matano.

Jambo la kwanza ni Ziara ya viongozi wa kisiasa Ikulu. Hili ni tukio.

Jambo la Pili, Mwenyekiti Mbowe amezungumzia Barua kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa kwenda kwa vyama vyote kuhakiki uhai wao ili kutambua vyama vinavyostahili kushiriki uchaguzi. Hii ni hoja ya kiutendaji.

Jambo la Tatu, Mwenyekiti Mbowe amelaani vikali Tabia inayoshamiri ya watu wachache kutaka kutumia Ukabila kuligawa Taifa. Hili ni tukio.

Jambo la nne, Mbowe amezungumzia ushirikiano wa vyama na kusema chana chake kinathamini sana ushirikiabo na kitakuwa tayari kushirikiana na chama chochote chenye nia thabiti ya kulikomboa Taifa- hapa pekee ndio hoja ya msingi na ya maana, lakini bila kusema how, pia ni empty!.

Jambo la tano, Mbowe alikemea vikali kauli ya hatari na ya kibabe iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally kwamba chama chake kitatumia Dola kushinda uchaguzi. Hili ni tukio.

Hizi siasa za matukio zitaifikisha wapi Chadema, wanawake ndilo kundi kubwa la wapiga kura, lini Chadema mtafanya mkutano na kuleta your own agendas na sio kuja kuhutubia kuhusu matukio, badala ya Chadema kuwa pro active kwa kutoa hoja zake, Chadema kazi yake ni kujibu tuu hoja za matukio.

Mtu anayezijua siasa za nchi hii kuelekea uchaguzi Mkuu akisikiliza hizo hoja 5 za Mwenyekiti, akisema Chadema hamna sera, mmeishiwa hoja, what are you standing for, ni hakuna, atakuwa anawaonea?.

Gap ya Chadema kutokuwa na watu ma strategists kama Zitto na Kitila, is very visibly seen!.

P

Paskali bila kupinga hoja zako maana kuna angalizo la msingi hilo unalosema siasa za matukio. Kwa kiasi fulani akitokea mtu anaweza kuamini usemacho maana kiko kisomi zaidi, bila kujali uhalisia.

Sasa twende taratibu nikuonyeshe kuwa ww ni mtu wa nadharia zaidi kuliko uhalisia. Kwanza kimsingi 70%+ ya wapiga kura wa nchi hii huwa hawachagui mgombea kwa sera bali huchagua kwa hamasa. Nitakupa mfano halisi wa kile ninachokiona, kwenye mikutano ya kampeni wangalau mkutano hupangwa kuanza saa 8 mchana au saa 9 alasiri mpaka saa 12 jioni. Wastani wa masaa matatu. Utakuta kwenye mkutano huo masaa mawili+ yote ni burudani, vijembe, kejeli na vioja. Lisaa limoja lililobakia nusu saa ni ya utambulisho na dakika chini ya 15 ndio za mgombea kunadi sera! Dakika 15 ni maswali ya kupanga na kuagana! Ukiangalia hapo dakika 15 ndio zimetumika kwenye mkutano wa masaa 3-4. Je dakika 15 kuna sera gani hapo?

Tuje tuangalie 30% iliyobaki inayotambua sera. Kwanza wengi wa hawa ni watu walioko busy, na kwa uzoefu wengi sio wapiga kura. Hata wao ukiacha kuwa ni watu wenye uelewa mpana, lakini sio watafiti au watu wanaopenda kusoma ili kujiongezea maarifa. Unakuta mtu toka amemaliza chuo hajawahi kusoma kitabu au kama kasoma ni vichache mno. Watu ambao ni wavivu kusoma, hawana hata muda wa kuchambua ubora au udhaifu wa sera, huo ndio uhalisia. Wangalau wakati wa JK tuliona bunge live, mikutano ya hadhara na midahalo iliyopandisha hamasa za wananchi kupata elimu ya uraia, na kuwa na uelewa mpana wa mambo. Toka amekuja Magufuli vyombo vya habari na wanahabari ikiwemo ww, mmeingia woga, wengine mmegeuka kuwa wanafiki na kuhubiri msichoamini. Wananchi wote sasa hivi kwenye media ukiacha hizi social media, wanalishwa anachotaka rais na wala sio sera. Katika jamii inayoishi kwa kulishwa atakacho rais kuna kuchagua kwa sera au ni kuchagua kwa hamasa? Kimsingi ukichaguliwa kuongoza nchi hii kwa hamasa, mabavu kama inavyofanyika sasa au vinginevyo, kikubwa ni kutoa huduma za kijamii kwa wananchi kama maji, barabara, afya, ajira nk.

Nifikie hitimisho ambalo ni la kanuni ya uumbaji, kitu chochote kikikaa muda mrefu watu huchoka, na kizazi chake hupita na kuja kizazi kingine kitakachohitaji jambo jipya. Ccm kama chama ni chama cha karne na kizazi kilichopita, kizazi cha sasa kimeichoka ccm, sio kwakuwa haijafanya kitu, la hasha ni kanuni tu ya uumbaji imefikia. Nadhani unakumbuka wakati mziki wa kizazi kipya ulipokuwa unaingia ilivyokuwa unapondwa na watu wa kizazi kinachoishia akina nyie kuwa hauna maadili, na watu wakawa wanasema nyimbo za kina Ottu, Sikinde nk ndio zenye maadili. Je leo hii kuna redio, tv au nyumba za burudani kusikopigwa miziki ya kizazi kipya? Kuna watu tena wanacheza muziki wa akina Sikinde ukiachia wazee? Magufuli ameingia kwa pupa bila kujua wala kuambiwa ukweli wa kanuni hii ya uimbaji, ndio maana anadhani akijenga barabara, reli, umeme nk watu wataipenda ccm hilo haliwezekani, na hapa sio suala la sera bali nature ndio ilivyo kuwa ccm ni outdated. Sasa hivi unaona ccm inatumia mabavu kwa maagizo ya Magufuli, inajisifu kujenga miundombinu kibao, lakini watu hawajitokezi kuipigia kura maana kanuni ya uimbaji haiko upande wao. Na kama hawatatokea watu wenye busara na kukimbia ukweli huu ccm, basi itaishia kukaa madarakani kwa hizo mbinu alizosema Bashiru Ally, lakini sio kwa ridhaa ya kura. Hivyo zile mbwembwe kuwa Magufuli na ccm wanakubalika ni propaganda mfu, ukweli ili ccm iendelee kukaa madarakani ni kwa mtindo ule wa uchaguzi uliopita wa SM.

tindo umemaliza yote. Atakuja kukupinga kwa vile ameshalishwa yamini kusifu na kuabudu binadamu mwenzake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Tindo, kwanza nakubaliana na wewe kwa yote na siku zote naiheshimu objectivity yako.
Hilo la CCM imechokwa na wanaiochagua CCM wanachagua nini, nimeieleza sana humu

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?

Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timamu, Anaweza Kuichagua Tena CCM?!. Kwa Lipi?!.

Elections 2015 - Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance?

Threads zinazidi 20!.

Pamoja na yote hayo, kwanini upinzani umeshindwa kwenda Ikulu?.
Sababu ni moja tuu, hatuna serious and credible opposition to oust CCM. Pale Wapinzani na watu objective kama nyinyi mtakapo waambia hao viongozi wenu makosa yao na kukubali kurekebisha, ndipo tutapata upinzani wa kweli.

Chadema ndilo lililokuwa tegemeo la upinzani huku bara, tumeishauri mpaka basi, sasa ni kusubiria tuu kifo baada ya 2020!.

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!.

Na ni kwa mtaji huu wa kukosekana kwa serious and credible opposition ndiko kunaifanya CCM itatawala milele!.

Naomba ufafanuzi wa serious na credible opposition. Niandikie kwa kifupi tu, sio ku copy na kupaste mabandiko yako ya zamani.

Amandla.....
 
Back
Top Bottom