Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Yanayojiri bungeni: Tarehe 20 Machi, 2014

Huku seneta A. Wako akieleza Kenya ilivyopata Katiba Mpya, Rev. C. Mtikila aibua tena 'Muungano,' ataka kanuni "zisiwatishie" wale wanaoupinga mtikila amesema watu wamekuwa wakitishwa na kama hali hiyo ikiendelea yupo tayari kuondoka dodoma.huko nchi za nje wapo watu wanampiga rais kwa mayai sisi tumeanza kutishwa tusimuhoji kesho atakapokua hapa yule amesjiriwa na wananchi.alisema mtikila mumini mzuri wa Tanganyika.
Kanifurahisha jinsi alivyofafanua suala la mahakama ya kadhi kuwekwa kwenye katiba ya Kenya,amesema Mombasa ilikuwa chini ya Sultani wa Zanzibar,Waingereza walipoitaka kwa ajili ya Bandari,walifanya makubaliano na Sultani akawapatia kwa Masharti kuwa kamwe wasifute mahakama ya kadhi,hivyo kaonya wanaotaka mahakama hiyo kwa Tanzania kwa kutolea mfano katiba ya Kenya waijue kwanza historia kwani kwa Tanzani ni ngumu kwani Waromani nao watadai mahakama ya canon laws ambayo nayo ikikubaliwa ni ngumu kwa Tanzania kwani rufaa za kesi ni kwa Papa huko Vatican,pia na dini nyingine zote nazo zinaweza kudai mahakama zao,hivyo ameshauri ilo suala lisiwepo kwenye katiba.
 
So kumbe mombasa nayo ilikua chini ya sultan wa zanzibar na ndo sababu kenya wakalazimika kukubali mahakama ya kadhi kama mbinu ya kumpoza sultan.
Huku bara wao walijaribu kuimeza zanzibar kimyakimya bila kuaddress ishu ya kilomita 16 za ukanda wa pwani kuwa under the territory of the sultan of zanzibar.
No wonder serikali inang'ang'ania serikali mbili kwa kujua kuwa siku zanzibar ikijitenga wanaweza kudai dar es salaam,tanga,pwani,kilwa.
No wonder pia just in case nyerere aliamua kuhamisha mji mkuu uwe Dodoma badala ya dar,kwani alijua siku yoyote linaweza kubumbuluka.
WE REALLY ARE STUCK BETWEEN A ROCK AND A HARD PLACE.

Wala, hawana ubavu wa kudai kwani hicho kipande kilinunuliwa na mjerumani kihalali.
Pili muarabu nae alikuwa mkoloni kama alivyokuwa mjerumani na muingerea sasa wakidai kama nani au wakoloni wakiarabu koko?.
Tatu wajaribu waone.
Wakitaka warudi arabuni kwao.
 
Katika namna ya kipekee leo Mch C. Mtikila amemuonya mwenyekiti kuhusu kauli kuwa watu wasiotaka muungano watashughulikiwa. Ameuliza jee watashughulikiwa kama Kolimba? Au Dr Mvungi, Ulimboka au kwa namna gani. Ameweka wazi kuwa kwa vile yeye yuko wazi kuwa haungi mkono muungano huu uliopo sasa wa kuipoteza Tanganyika hivyo tishio hilo la kushughulikiwa ni wazi ni kwake yeye. Kama mawazo ya wengine hayasikilizwi bali ya kikundi cha watu wachache (CCM) anafikiria kufungasha virago na kurudi Dar ili kuendelea na shughuli zingine kuliko kushiriki Bunge linaloburuzwa kwa maslahi ya watu wachache. Pamoja na Sitta kuipoza hoja hiyo kwa kusema Mtikila asiwe na wasiwasi, lakini maelezo ya Mtikila yameleta damage kubwa katika uhuru wa uendeshaji wa bunge hilo.
Jee kama kuna kutishana kushughulikiwa inakuwaje kwa wale wajumbe legelege wasio na msimamo thabiti kama Mtikila? Watawezakufanya kazi tuliyowatuma?

Sent from my iPad using JamiiForums
Sitta alisema kuwa wasio utaka muungano watashughulikiwa.!
 
nimefurahi namna mwenyekiti wa bunge alivohandle utoaji wa hoja kwa mchungaji mtikila. Yaani roho ilikuwa ikilipuka kwani nilikuwa najaribu kufikiria kama mwenyekiti akijaribu kumzuia asitoe neno mchungaji mtikila kingetokea nini

Unajua pale Mtikila alikuwa anampa Sitta za uso bila aibu. Na kama Sitta angejifanya refa na kusimamisha pambano ingekuwa ni Technical knock out. Mtikila amefungua mjadala wa uwazi bila woga,na ndilo tunalotaka wote hayo mambo ya kushughulikiana wakashughulikiane kwenye vikao vyao vya ndani hao walioamua pamoja na kuacha familia zao kwa siku nyingi kuja kuwa mazezeta ya watawala. AIBU KWAO.
Wito kwa wana JF, wale wajumbe wenye mwelekeo wa kufanya maamuzi kwa kujikomba na woga wa watawala kila anayefahamika jina lake liwekwe wazi tuwajue kuwa ni wasaliti na familia na ndugu zao na marafiki wawafahamu ili heshima yao ishuke kwenye jamii yote. Katiba ni yetu wote si yao wachache. Na kama huna msimamo wa kutetea wananchi usingeenda.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mi nadhani ipo haja ifanyike Campaign maalum ya kuhamasisha watz tuhudhurie masomo ya kiingereza, hata kwa muda wa jioni baada ya majukumu mengine ya kusaka maisha......hii lugha inafanya tunabaki nyuma kwa mambo mengi tukubali au tukatae..........ngoja nianze kutafuta wataalamu wa kimombo hapa jf tuandae vipindi vya luninga kila jioni, naamini kuliko kuangalia upuuzi wa baadhi ya vipindi kwenye TV hichi cha masomo ya kingereza kinaweza kuwa na manufaa zaidi.
 
Huyu jamaa anasema ukweli mtupu, tstizo ushabiki na kuwa na viongozi wanao fikiri kwa kutumia t.u.mbo ndo sababu humu kuna watu wanajadili huku povu likiwatoka wakitaka serikali mbili kwani wanaishi kwa kupigia debe uozo. Hakuna mtu anaye jitegemea kwa chakula na kuishi kwa kuendesha maisha yake mwenye akili timamu akaunga mkono serikali mbili.
 
Na alivyoingia profesa Safari, kuna mjumbe nasikia aliropoka akasema Mtikila namba 2 huyu
 
Nikiwa naangalia kipindi cha semina ya Bunge maalumu la katiba nimeshituka baada ya Mh.Mch.C.R.Mtikila akiwa anatahadharisha wabunge juu ya vitisho vya baadhi ya wabunge kama vile Prof.Mwandosya,Mtikila amesema ameshaambiwa eti kabla jk hajahutubia bunge la katiba hapo kesho aondoke kidogo aende dar ili kupisha hali ya hewa isichafuke.

Akiendelea na maelezo yake amesema baadhi ya wanaccm wanasema atakaeenda kinyume na msimamo wa serikali tatu atashughulikiwa.ndipo akauliza
..je watatushughulikia kama Ulimboka,,Dr Mvungi au Kolomba!
Ameonesha wazi kuwa dr mvungi kwa makusudi ameuliwa.

Je unadhani christopher ana mengi juu ya hayo!!

R.i.p Dr Mvungi.
 
Namshauri ndugu Mtikila asiondoke Dodoma maaana kususa ni kuwapa manyan'gau urahisi wa kutuburuza, japo tunajua watampuuza kama wanavyofanyaga lkn historia haitaandika uongo,itakuwa heri yeye alisema kuliko kina wengine wanavumilia maumivu kimya kimya bila kufungua midomo..........
Hongera Mch Mtikila, asikutishe mtu hapo,tangu wameanza kutoa roho za watu nini wamepata zaidi ya laana tu Nchi haisongi mbele zaidi ya umaskini kuongezeka, aibu yao.

Jembe Mbowe si yupo au haaminik
 
Wala, hawana ubavu wa kudai kwani hicho kipande kilinunuliwa na mjerumani kihalali.
Pili muarabu nae alikuwa mkoloni kama alivyokuwa mjerumani na muingerea sasa wakidai kama nani au wakoloni wakiarabu koko?.
Tatu wajaribu waone.
Wakitaka warudi arabuni kwao.
mkuu hakikununuliwa,wajerumani wali LEASE mpaka mwaka 1948,bahati mbaya ikatokea vita wakaondolewa baada ya vita vya pili vya dunia mwaka 1945.

Mikataba hii ya kimaifa huwaga inastick,ndo maana leo tuna matatizo na malawi.
Waingereza huko kenya walifanya kuingia makubaliano na sultan.
Hizo km 16 za ukanda wote wa pwani zilikua zinajumuisha pwani yote,ikijumuisha na pwani ya kenya na tanganyika.
That is why wako ametoa jicho na kusema hiyo issue ni VERY HOT.
Hivi unadhani kwanini nyerere aling'ang'ania sana huu muungano?
 
Mtikila ameongea point sana!!! Kuna watu walitishiwa awali kabisa kuwa ni lazima wapige kura kufuata matakwa ya CCM kati ya wale wajumbe 201!!!! Pia kwa CCM inaeleweka tena kabisa kuwa wanalazimishana kupigia kura yale ambayo wanaona yanafaa kwao katika kuendeleza udikteta.
 
Kiingereza ni lugha ya pili ya Taifa, lakini watanzania wengi hawajui kiingereza kwa sababu ili ujue kiingereza tz mara nyingi lazima uwe umepita shule angalau sekondari ambapo elimu inatolewa kwa kiingereza, sasa kwetu sisi watz ambao wengi hawajapata fursa ya kuhudhuia shule ambao pia ni wengi,hawajui kiingereza. Tunatengeneza katiba ambayo inayowaathiri wengi wasiojua na wanaojua kiingereza ni vema itumike lugha ambayo kila mmoja wetu anaielewa(Kiswahili) hata kama muda utakuwa mrefu. kimsingi wabongo hatupaswi kuona aibu ya kutokujua kiingereza vizuri maana hakuna taifa hapa duniani ambalo watu wake wanatumia lugha za taifa mbili na wanazimudu zote kwa ufasaha. na wala kujua lugha yakigeni vizuri hakiwezi kuwa kipimo cha ujinga au uelewa wa Watanzania hapa hakuna sababu ya kuona aibu, kama ndivyo basi naomba tumuone huyo Wacko na Wakenya kuwa ndio wanatia aibu maana hawajui Kiswahili na Kiingereza vizuri.
 
Na alivyoingia profesa Safari, kuna mjumbe nasikia aliropoka akasema Mtikila namba 2 huyu

Hiyo ni kuonyesha wazi kuwa mle ndani hata viti vina thamani kuliko baadhi ya walio vikalia. Ndio maana nakusudia kuanzisha thread itakao wataja wazi wajumbe watakao gundulika kuwa ni sawa na mizigo ili tuwataje na wake/waume zao wajue wanakosa chakula cha usiku pasipo sababu za maana. Maana kama mjumbe anaendekeza ujinga sii bora angebaki kwake akaendelea kumpa mke/mume haki yake ya usiku kuliko kupoteza muda Dodoma.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Kanifurahisha jinsi alivyofafanua suala la mahakama ya kadhi kuwekwa kwenye katiba ya Kenya,amesema Mombasa ilikuwa chini ya Sultani wa Zanzibar,Waingereza walipoitaka kwa ajili ya Bandari,walifanya makubaliano na Sultani akawapatia kwa Masharti kuwa kamwe wasifute mahakama ya kadhi,hivyo kaonya wanaotaka mahakama hiyo kwa Tanzania kwa kutolea mfano katiba ya Kenya waijue kwanza historia kwani kwa Tanzani ni ngumu kwani Waromani nao watadai mahakama ya canon laws ambayo nayo ikikubaliwa ni ngumu kwa Tanzania kwani rufaa za kesi ni kwa Papa huko Vatican,pia na dini nyingine zote nazo zinaweza kudai mahakama zao,hivyo ameshauri ilo suala lisiwepo kwenye katiba.

hajahitimisha vizuri ktk hili, ni kama anatuamulia vitu vya kuwepo kwenye katiba japo mimi si muumini wa hiyo mahakama!
 
Nikiwa naangalia kipindi cha semina ya Bunge maalumu la katiba nimeshituka baada ya Mh.Mch.C.R.Mtikila akiwa anatahadharisha wabunge juu ya vitisho vya baadhi ya wabunge kama vile Prof.Mwandosya,Mtikila amesema ameshaambiwa eti kabla jk hajahutubia bunge la katiba hapo kesho aondoke kidogo aende dar ili kupisha hali ya hewa isichafuke.

Akiendelea na maelezo yake amesema baadhi ya wanaccm wanasema atakaeenda kinyume na msimamo wa serikali tatu atashughulikiwa.ndipo akauliza
..je watatushughulikia kama Ulimboka,,Dr Mvungi au Kolomba!
Ameonesha wazi kuwa dr mvungi kwa makusudi ameuliwa.

Je unadhani christopher ana mengi juu ya hayo!!

R.i.p Dr Mvungi.

Mkuu hapo kwenye redi sijui ni typing aero (nahisi ulikuwa unamaanisha Serekali mbili)

Kwa serekali hii no wonder on what mtikila said
 
Hana. Hayo aliyosema sio mapya masikioni kwetu. Labda akiyathibitisha kwa vielelezo vinginevyo ni hadithi tu.
 
Back
Top Bottom