Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano Tarehe 26 Machi 2014

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano Tarehe 26 Machi 2014

Ccm ni watu wa ovyo sana kama walijua haya yatatokea kwa nini kikwete aliruhusu huu mchakato?
au akujua kitakacho tokea ?ha ha nampa pole sana kikwete na ccm yake hakika hapa atoki mtu lazima UKAWA watusaidie kupata katiba tuliyo itaka sisi wananchi.

UKAWA ni nini? Kuuliza si ujinga.
 
Mkuu nimekugongea like na mbaya zaidi uoga wa wananchi umesambaa mpaka kwa viongozi wa upinzani ni waoga. Chadema kila siku wanasema maandamano nchi nzima na haijawahi kutokea japo kujaribu ushindwe hakuna ilka wakiongea waka kauli za kikamanda kweli ila uoga umewatawala


ila hata raia wa tz wamelala sana; kuna nchi huu ushenzi hauvumiliki kabbisa!
 
alishatoa ushauri aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya kenya wakati wanandika katiba mpya ya kenya kuwa
msiposikilizana na mkiendekeza itikadi za vyama mtaandika katiba mbovu na wananchi wataadhibu tu kwa kuikataa hapo ndipo mtajua ya kuwa mlikuwa mnapoteza muda kwa faida ya vyama vyenu na sio kuwatumikia wananchi kama wengi wa wana ccm wanavyojinadi
 
Watanzania tunapitia mchakato mgumu wa kuamua hatima ya taifa hili, tunatamani amani ibaki lakini tulikofika tunaogopa kama kweli tutakuwa na hatma nzuri tukitizama mchakato wa katiba unavyoenda.

Najua ramadhani bado lakini, hatunyimwi kutafuta muda maalumu kumuomba na
kumlilia Mwenyezi Mungu juu ya yote
yanayotusibu tukiomba msaada kwni yeye ndie mtoaji.

Watanzania tunaihitaji Katiba mpya na bora, lakini wapo baadhi ya watu ambao wapo mrengo wa CCM wanatia makwazo, hivyo tuombe Mungu atusaidie tuweze kufikia hatma njema.

Kama pakitokea wapo wanaoendelea kufanya maovu kwa lengo baya la kukwamisha katiba mpya tufikie mahala tuwasomee MUBAHALA, ili Mungu atoe hatma yake kwa wale woote wanaoonekana kuikandamiza nchi na watu wake.

Naomba Mashekh, wanazuoni, baraza la maulamar tutafakari hili jambo tufikie hatma.
 
wana ccm mpo?
msafara wa JK kwenda msoga tu gari 15 mpaka 20 za kazi gani hatujui eti analindwa
huku bungeni nako ni fujo tupu
 
Mkuu sixgates mbona tuna mchosha Mungu??

Ametupa Akili na Maarifa ili tuwe tofauti na wanyama..

Macho na masikio..

Uwezo wa kuamua nini tunataka na nini hatutaki..

Hivi bado tunahitaji tufanye Maombi badala ya kuwachukulia hatua?
 
Last edited by a moderator:
Hakuna ambalo Sitta ataweza kuliamua hapo bungeni bila ya kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na 'White House' kuona kama linawafaa au laa. Kiufupi, Samuel Sitta ana interests zake 'White House' na 'White House' ipo na interests zake kwa Samuel Sitta. Matokeo ya upuuzi huu ni nini? Ni kuiingiza nchi katika mtafaruku na balaa. Laitani hawa wanaojiita viongozi wangelisoma alama za nyakati na matokeo yaliyopata kutokea kwengineko wasingethubutu kuchezea kiberiti katika Dumu la petroli. Tusubiri tuone.
 
Lukuvi WAssira Werema Pinda mbona mpoo kimya wakati upuuzi wote huu nyie ndiyo ma engineer?
 
Mkuu sixgates mbona tuna mchosha Mungu??

Ametupa Akili na Maarifa ili tuwe tofauti na wanyama..

Macho na masikio..

Uwezo wa kuamua nini tunataka na nini hatutaki..

Hivi bado tunahitaji tufanye Maombi badala ya kuwachukulia hatua?

Mkuu umenena vyema, tumejaribu kadri ya uwezo wetu. Ndio naatoa wito tumrejee Mwenynz Mungu atutatulie hili linalotuchosha, sio vibaya na haijawahi kuwa vibaya.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: prs
Back
Top Bottom