Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, January 27, 2015

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, January 27, 2015

mahakama ya kadhi ni kuhalalisha serikali ya kiislam nchini
 
Hakuna chama kitashika madaraka Tanzania bila kura za Waislam walio wengi, hilo kumbuka.

Na sasa Waislam tutatumia nguvu yetu ya kura kushinikiza tuyatakayo. Atependa haya asiyependa haya, Waislam tukipiga kura ya NO usahau madaraka. Kumbuka hilo.

Huo ndo mtaji wako na siyo mambo ya tuchague mtu uliyoleta siku zile.
siku hizi hao waislamu wanajua kusoma na kuandika na kuhesabu? ie KKK.
 
Hawa jamaa wa sheria la utangazaji la Taifa mbona ni vilaza, inakuwaje zaidi ya saa nzima sasa hawajui kuwa watazamaji hawasikii kitu kwenye matangazo yao wanayoyarusha. Na hii nimeiona leo tu, tokea tamthiliya yao ya kichina mpaka sasa hivi bunge limeanza hakuna sauti. Tunaachaje kufikiria kuwa huu ni mchezo mwingine mchafu, hili ya kufanya wananchi wasijue kinachoendelea?

hebu sema na ww labda watasikia,maana hapa tbc 1 ni full utumbo,alafu nashanga mbona star tv hai oneshi wakati ilitangaza itaonesha mbuge,mbona kimya,alafu tbc 1 mmbunge akiwa anauliza swali hasikiki,mpaka waziri akiwa ana jibu.
 
Bigurube serikali ina dini na hapa ndipo unaposikia Mfumokristo katika uendeshaji wa nchi...
 
Mkutano wa 18 wa Bunge unaanza leo mjini Dodoma, lakini hoja nzito ambazo zinatarajia kuibua mijadala mizito ni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Jumla ya miswada mitatu itawasilishwa kwenye mkutano huo, lakini tayari kuna dalili kuwa muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali, ambao unagusa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, unaweza kuibua mjadala mzito bungeni, kutokana na suala hilo kila linapoibuka wabunge wamekuwa wanagawanyika.

Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza wa Bunge, bila kuwepo kwa vigogo ambao wameondolewa au kujiuzulu, kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow. Vigogo hao ni Mwanasheria Mkuu wa zamani, Jaji Frederick Werema, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospeter Muhongo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge hilo, katika mkutano huo moja ya shughuli ambazo zitafanywa na Bunge ni kujadili taarifa za CAG zilizowasilishwa katika Mkutano wa 15.

Miongoni mwa madudu ambayo Ripoti ya CAG ilibaini serikalini ni malipo ya mishahara hewa, kupotea kwa stakabadhi kwenye halmashauri, uwindaji haramu unavyoongezeka na kandarasi tata ndani ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).

Wenyeviti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), watawasilisha ripoti zao na serikali itajibu taarifa hizo, ambazo ni hesabu za mwaka 2012/13.

Pia, katika mkutano huo, Kamati za Bunge nazo zitapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa za mwaka za shughuli za Kamati; na zitapangiwa muda wa kujadiliwa, kwa kadri Spika atakavyoelekeza.

Hali kadhalika, Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi, itapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa yake, na taarifa hiyo itajadiliwa bungeni hapo.

Taarifa hiyo ya Bunge ilisema miongoni mwa shughuli za leo bungeni ni kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ambaye amejaza nafasi ya Jaji Werema.

Taarifa hiyo ilitaja miswada itakayowasilishwa na kupitishwa katika vikao vya Bunge ni Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 ambao utapigiwa kura tu, Muswada wa Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 na Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 2 wa mwaka 2014.

Wakati huo huo, Jukwaa la Wakristo limetoa tamko ambalo linaishauri Serikali kuuondoa bungeni Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa kile linachodai kuwa ni kuepusha kuvunja misingi ya taifa, ambalo halina ubaguzi na lisilo na dini yoyote.
Muswada unaopingwa na jukwaa hilo ni ule ambao unapendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964, ambao unapendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.

Tamko hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana kwenye taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Jukwaa hilo, ambao ni Askofu Dk Alex Malasusa wa Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT) , Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu Daniel Awet kutoka Umoja wa Makanisa ya Pentekoste (CPCT) baada ya mkutano uliowakutanisha Januari 20 mwaka huu.

Kwenye tamko hilo, viongozi hao walieleza kuwa mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa, yatakayokuwa na athari kubwa na nzito, yakihoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini.

Tamko hilo lilieleza kuwa kwa sababu hiyo, mapendekezo hayo yanaibua mambo mazito ya kikatiba, ambayo hayawezi kuamuliwa na muswada huo.

Tamko hilo lilibainisha kuwa sababu zilizowezesha kufutwa kwa mahakama hizo mwaka 1963, ilikuwa kujenga umoja wa kitaifa, kuondoa ubaguzi katika mfumo wa kisheria na utoaji haki sawa, jambo ambalo bado ni halali na la msingi kwa sasa.


Kipindi cha maswali na majibu:


Swali- Ezeckiel wenje
: Kuhusu makazi ya walimu.

Majibu- Naibu waziri: Mahitaji ya nyumba ni kmakubwa, serikali inajiandaa kufanya ukarabati, Walimu wanatakiwa kuishi kwenye nyumba za serikali bila kutozwa kodi

Majibu ya swali la nyongeza: Walimu wanapaswa kuishi kwenye nyumba za serikali bure.

Swali- Zitto Kabwe: Anauliza kuhusu fedha wanazokatwa walimu kwaajili ya makazi.

Majibu- Naibu waziri: Swala la watumishi kukatwa fedha lilitokana na kanuni za utumishi ambazo zilirekebishwa, na sasa walimu waliokatwa wanatakiwa kurejeshewa fedha zao.



upande wanapokaa ukawa sauti haisikiki.
 
Sumbai suala la wingi wa wafuasi katika Uislam na Ukristo ni suala linalowatisha sana wale walohodhi madaraka. Jiulize ni nani aliyekuwa hataki kipengele cha dini katika sensa utapata jibu. Ukiona serikali inapinga jambo linalotakiwa na Waislam jua hilo halina maslahi na Ukristo...mifano ni mingi...ukipenda fungua uzi wa mada hii utajulishwa mengi...
 
Kwa kweli hii ni aibu sana kwa sababu ya uoga tu wa serikali nd'o wanafika mahala wanafanya hivi?
 
Mkuu bado unaangalia huu upuuzi wa tbccm?Tupa kule tune star tv!

star tv haioneshi ndugu yangu.!naona weme kuja na staly nyingine wa kufanya wananchi wasijue kinacho endelea,TBCCM SHAME ON YOU..!ACHANE UKIRITIMBA NYIE.
 
Chenge kiboko yao kama kawaida ndani ya nyumba
 
And vice versa is true,kwa nn waslam wamekuwa n watu wa kudai tu?
Sumbai suala la wingi wa wafuasi katika Uislam na Ukristo ni suala linalowatisha sana wale walohodhi madaraka. Jiulize ni nani aliyekuwa hataki kipengele cha dini katika sensa utapata jibu. Ukiona serikali inapinga jambo linalotakiwa na Waislam jua hilo halina maslahi na Ukristo...mifano ni mingi...ukipenda fungua uzi wa mada hii utajulishwa mengi...
 
Hakuna chama kitashika madaraka Tanzania bila kura za Waislam walio wengi, hilo kumbuka.

Na sasa Waislam tutatumia nguvu yetu ya kura kushinikiza tuyatakayo. Atependa haya asiyependa haya, Waislam tukipiga kura ya NO usahau madaraka. Kumbuka hilo.

imebidi nikupende tu mana hakuna jinc NIKUPENDE TU
 
Bigurube serikali ina dini na hapa ndipo unaposikia Mfumokristo katika uendeshaji wa nchi...

kwa hiyo mnapambana kuupata mfumo Mohamed? mnaupakazia ukristo tu maana mwenyewe alisha tenganisha kanisa na serikali. aliuluzwa swali ni halali kwa wafuasi wake kulipa kodi ya serikali?

aliwajibu, ya kaisari mpeni yaliyo yake na mungu mpeni yake. ndio maana mkristo hayuko tayari kuchanganya dini na siasa
 
Chakaza unataka kusema Wakatoliki si wamoja kwa kuwa kuna Wanamaombi?
Mohamed Said wewe ni zaidi ya hapo. Ukweli unaujua dhahiri ndio kuhusu mgongano uliopo katika waumini wa kiislamu tofauti na hiyo ya wana maombi. Mfano mzuri ni mgogoro wa sheikh Ponda na kundi lake na msimamo wa Bakwata juu ya jambo hilo. Imefika mahali wengi wenu mmekataa kabisa kulitambua hilo baraza kama chombo chenu cha uwakilishi.
 
Last edited by a moderator:
Nikukumbushe labda nikukumbushe...unapomtukana mama wa mwenzio ni sawa ya kumtukana mama yako alokuzaa...hayo matusi kabla hujayatoa ungemuwaza mama yako na fikra ikakujia kuwa mamio kaumbwa kama alivyoumbwa FF...labda ungesita...hapa si mahala pa matusi humu ni mahala pa mijadala itakayosaidia watu kuelewana ili nchi yetu isonge mbele kwa amani...
 
Back
Top Bottom