Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 700
Mkutano wa 18 wa Bunge unaanza leo mjini Dodoma, lakini hoja nzito ambazo zinatarajia kuibua mijadala mizito ni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Jumla ya miswada mitatu itawasilishwa kwenye mkutano huo, lakini tayari kuna dalili kuwa muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali, ambao unagusa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, unaweza kuibua mjadala mzito bungeni, kutokana na suala hilo kila linapoibuka wabunge wamekuwa wanagawanyika.
Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza wa Bunge, bila kuwepo kwa vigogo ambao wameondolewa au kujiuzulu, kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow. Vigogo hao ni Mwanasheria Mkuu wa zamani, Jaji Frederick Werema, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospeter Muhongo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge hilo, katika mkutano huo moja ya shughuli ambazo zitafanywa na Bunge ni kujadili taarifa za CAG zilizowasilishwa katika Mkutano wa 15.
Miongoni mwa madudu ambayo Ripoti ya CAG ilibaini serikalini ni malipo ya mishahara hewa, kupotea kwa stakabadhi kwenye halmashauri, uwindaji haramu unavyoongezeka na kandarasi tata ndani ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).
Wenyeviti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), watawasilisha ripoti zao na serikali itajibu taarifa hizo, ambazo ni hesabu za mwaka 2012/13.
Pia, katika mkutano huo, Kamati za Bunge nazo zitapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa za mwaka za shughuli za Kamati; na zitapangiwa muda wa kujadiliwa, kwa kadri Spika atakavyoelekeza.
Hali kadhalika, Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi, itapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa yake, na taarifa hiyo itajadiliwa bungeni hapo.
Taarifa hiyo ya Bunge ilisema miongoni mwa shughuli za leo bungeni ni kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju ambaye amejaza nafasi ya Jaji Werema.
Taarifa hiyo ilitaja miswada itakayowasilishwa na kupitishwa katika vikao vya Bunge ni Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 ambao utapigiwa kura tu, Muswada wa Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 na Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 2 wa mwaka 2014.
Wakati huo huo, Jukwaa la Wakristo limetoa tamko ambalo linaishauri Serikali kuuondoa bungeni Muswada huo wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa kile linachodai kuwa ni kuepusha kuvunja misingi ya taifa, ambalo halina ubaguzi na lisilo na dini yoyote.
Muswada unaopingwa na jukwaa hilo ni ule ambao unapendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964, ambao unapendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Tamko hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana kwenye taarifa iliyosainiwa na viongozi wa Jukwaa hilo, ambao ni Askofu Dk Alex Malasusa wa Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT) , Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu Daniel Awet kutoka Umoja wa Makanisa ya Pentekoste (CPCT) baada ya mkutano uliowakutanisha Januari 20 mwaka huu.
Kwenye tamko hilo, viongozi hao walieleza kuwa mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa, yatakayokuwa na athari kubwa na nzito, yakihoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini.
Tamko hilo lilieleza kuwa kwa sababu hiyo, mapendekezo hayo yanaibua mambo mazito ya kikatiba, ambayo hayawezi kuamuliwa na muswada huo.
Tamko hilo lilibainisha kuwa sababu zilizowezesha kufutwa kwa mahakama hizo mwaka 1963, ilikuwa kujenga umoja wa kitaifa, kuondoa ubaguzi katika mfumo wa kisheria na utoaji haki sawa, jambo ambalo bado ni halali na la msingi kwa sasa.
Kipindi cha maswali na majibu:
Swali- Ezeckiel wenje: Kuhusu makazi ya walimu.
Majibu- Naibu waziri: Mahitaji ya nyumba ni kmakubwa, serikali inajiandaa kufanya ukarabati, Walimu wanatakiwa kuishi kwenye nyumba za serikali bila kutozwa kodi
Majibu ya swali la nyongeza: Walimu wanapaswa kuishi kwenye nyumba za serikali bure.
Swali- Zitto Kabwe: Anauliza kuhusu fedha wanazokatwa walimu kwaajili ya makazi.
Majibu- Naibu waziri: Swala la watumishi kukatwa fedha lilitokana na kanuni za utumishi ambazo zilirekebishwa, na sasa walimu waliokatwa wanatakiwa kurejeshewa fedha zao.
Majibu- Waziri : Ni kweli bado shule binafsi zinaenda kinyume na maagizo ya serikali, Shule zisizotekeleza taratibu za serikali zitafutwa.
Swali- Dk Dhakifu: Wazazi hawana uwezo wa kulipa ada, Lini serikali itatamka kutoa elimu ya bure.
Majibu - Waziri: Serikali imeadhimia kila mtoto anapata elimu ya msingi na sekondary na Mheshimiwa raisi ametangaza adhma ya serikali ya kutoa elimu ya sekondary.
Ahmedi mwidau Swali- Uhaba wa walimu kwenye shule za serikali
Majibu- Waziri wa elimu: Wizara imeanzisha mafunzo ya stashada ya juu ya masomo ya uwalimu. Serikali inamkakati wa kuendelea kuajiri walimu wa sayansi na hisabati, imeajiri mwaka jana na mwaka huu itaajiri walimu wengine. Serikali inamkakati wa kukarabati vyuo vya uwalimu.
Swali la nyongeza:
Majibu- Waziri: Vivutio kwa walimu wa Hesabu na Sayansi, Serikali inapenda kuweka vivutio kwa walimu wote hususan walimu wa sayansi na hesabu, Serikali inajiandaa kuboresha Mishahara na mazingira ya kufundishia.
Kuhusu TEHAMA na umeme katika shule, Kwenye miradi ya umeme almashauri zimeelekezwa kufikisha umeme kwenye mashule.
Swali- Mh Msola: Chuo cha sanaa cha Mkwawa, kwanini kisitumike kufundisha masomo ya Sayansi pekee badala ya kuwa chuo cha sanaa kama ilivyo hivi sasa ?
Majibu- waziri: Wazo la proffesa ni zuri na serikali ipo karika mchakato wa kulitekeleza hilo. na sasa inaboresha maabara ya chuo hicho.
WIZARA YA MAWASILIANO:
Swali Mh Mwanausi: Ni lini wananchi wa mpakani mwa Tanzania na msumbiji watapatiwa mawasiliano.
Majibu: Maeneo ya mpakani na maeneo yake yamewekewa mpango maalumu na kufikia July mwaka huu yatakuwa yamepatiwa mawasiliano.
Note: Wabunge wanapouliza maswali Sauti inakata kwahiyo inakuwa kazi kupata maswali yanayoulizwa na pia majibu yanashindwa kueleweka.
Kwenye majibu ya nyongeza: Kampuni ya simu ya VIATEL itakuwa kampuni yenye ubora wa hali ya juu kwasababu inaanza na mtandao wa 3g moja kwa moja tofauti na makampuni mengine.
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Swali la nyongeza- Mh Mangungu:
Majibu- Naibu Waziri : Sio kwamba serikali inachukuwa muda mrefu lakini mahitaji yamekuwa mengi. Sio kwamba kila eneo la kijijini linatoza hizo pesa, kinacholipwa elfu 27 ni VAT tu, maeneo ambayo mradi wa lea haujafika wananchi wanaendelea kulipa.
Swali- la Mh Magdalena Hamisi Sakaya: ikuhusu mradi wa REA.
Majibu: Jumla ya vijiji 41 vipo kwenye mpango wa REA. Mradi unawaunganisha wateja 1550, kazi inaendelea na utekelezaji umefikia zaidi ya asilimia 50. mradi unatarajiwa kukamilika mwaka 2015.
Swali la nyongeza- Mh Masudi:
Majibu: Wananchi wa kaliua watapata umeme, kuandaa mipando na kuagiza vifaa inachukuwa muda mrefu sana, lakini vifaa vikifika utekelezaji unachukuwa muda mfupi.
Swali- Mh kapuya: Naishukuru sana wizara ya nishati na madini kwa kufikisha umeme kwenye kijiji cha Kawira.
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Swali: kuhusu Shilingi m250 zilizotengwa kwa ajili ya kukarabati majengo ya wazee .
Majibu naibu waziri wa Afya: Wizara inafanya tathmini ili kuangalia jinsi ya kuboresha zaidi makazi ya wazee
Swali la nyongeza: Makazi ya Kiilima ni mabovu sana nyumba hazina madirisha wala milango, hakuna vyoo wala chakula cha uhakika, Waziri anasema kunampango wa kufanya ushirikiano na DANIDA, saa ni lini serikali itakamilisha mpango huo. Je kunampango gani wa kutoa chakula cha uhakika kwa wazee hao.
Majibu- Naibu waziri: Katika mwaka unaokuja wa fedaha serikali itaingiza vituo hivi kwenye bajeti kwa awamu . Serikali inampango wa kupunguza makazi haya ili kuongeza udhibiti.
Swali la nyongeza - Mh Rweikiza: wazee wanaishi kwa kutegemea wafadhili, kwanini serikali iseweke bajeti kwa ajili yao
Majibu: Wafadhili wanaojitokeza ni walioguswa na sio njia kuu ya kuwatunza wazee hao, serikali inatenga bajeti
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Swali- Rajabu Mbaruku Mohammed: Tatizo la tembo kuzaliwa bila meno serikali inachukua hatua gani ?
Majibu: Tembo wote huzaliwa bila meno lakini meno huota baadaye, kuna taarifa za kuongezeka kwa tembo wasiokuwa na meno, seriali inafanya utafiti ambao umelenga kuthibitisha taarifa hizi, utafiti huu haukuwa wa kina na haukulenga kuleta ufumbuzi.
Swali la nyongeza :
Majibu : Ni kweli nilikiri kwenye vyombo vya habari kuwa Idadi ya tembo wasiokuwa na meno inaongezeka na sababu ni kwamba tembo wasiokuwa na meno sio waathirika wakubwa wa ujangili.
Swali- Mh Mbatia:
Jibu: Ni kweli wizara ya maliasili inachangia 19% kwenye pato la taifa na tunampango wa kuongeza mpaka asilimia 30, bado tunahimiza utalii wa ndani.
WIZARA YA UJENZI
Swali- Bwanausi: kuhusu baranara ya masasi na daraja la ukama.
Majibu- Naibu waziri wa Ujenzi : Serikali imekubali na imejicomit kukamilisha ujenzi wa barabara hii, kuhusu daraja serikali italifatilia kuona kitu gani inaweza kufanya.
Swali la nyongeza la Mh Mkapa:
Majibu: Ujenzi wa daraja unaendelea kuhusu ukamilifu wake serikali itamfatilia mkandarasi ili kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi na wakati.
Swali la nyongeza- Dk Chami:
Majibu- Naibu waziri wa ujenzi: Ni kweli swala hili lipo ndani ya ilani ya chama cha mapinduzi na kazi hii imeshafanyika kwa awamu. Tunapozungumzia ujenzi wa barabara inajumuisha na daraja.
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Swali- Mh Mashishanga (Viti maalumu): Kuhusu kiwanda cha kusindika nyama Shinyanga kilichokuwa kinamilikiwa na Tanganyia Pekas
Majibu- Naibu waziri: Kampuni inayosimamia ipokwenye mchakato wa kutafuta mbia mwingine atakaewekeza kwenye mitambo mizuri zaidi ya kuchinja na kusindika nyama.
Majibu ya swali la nyongeza: Sasa tufike mahali tusaidiane tutafute mbia mwingine.
Swali- Mch Mwanjari: Hata mbeya kuna kiwanda hakifanyi kazi serikali inasema nini juu ya swala hili.
Majibu: Hili nalo tunaliunganisha na jibu lililotangulia.
WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Swali- Kwanini serikali isiondoe kodi kwenye mashirika ya kidini
Jibu- Naibu waziri: Kodi ambayo mashirika haya yanatozwa ni tsh 8000 ambayo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na kodi zinazotozwa kwenye asasi zingine, hivyo serikali haina mpango wa kuondoa kodi hiyo kwa sasa ili mashirika hayo yachangie hata kidogo.
Swali lanyongeza- Mh Ragge: Serikali inatoa kauli gani kwa manispaa zinazotoza kodi zaidi ya tsh 8000?
Majibu - Naibu Waziri: Serikali inakemea vikali Manispaa zote zinazotoza zaidi kinyume na maagizo ya serikali.
Matangazo
Mswada wa Twakimu unaondolewa kwenye orodha ya shughuri za bunge, Serikali inataka kuurekebisha zaidi. Mswada wa kodi
Mh Wenje: amesimama lakini Sauti imekatika.
Spika anasitisha shughuri za bunge hadi Kesho saa tatu Asubuhi