Yanayoendelea sasa CHADEMA ni mpango toka nje kuingiza nchi matatizoni. Serikali ina kazi ngumu huko mbele

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Chadema ni chama cha siasa chenye wanasiasa ambao si makini.

Ni chama kilichokusanya watu wanojiita wanasiasa lakini hawana mbinu za kuishi kwenye siasa.

Miaka mitano ilopita Chadema walipata shida na hawakuweza kujinafasi na serikali ambayo iliongozwa na raisi ambae hakuwa tayari kuvumilia vurugu iwe maneno au vitendo.

Sasa yupo raisi Samia Hassan huu ndo ulikuwa wakati wa Chadema kuketi chini na kupanga mikakati mipya ambayo itaendana na mwendo wa serikali ya sasa.

Nimewahi kusema mara nyingi kuwa Chadema haina wanasiasa makini ambao wanaweza kutofautisha siasa za vurugu na siasa makini za majibizano ya hoja kwa ustaarabu.

Pia nimewahi kusema kuwa Chadema imekosa wanamkakati au "strategists" ambao wataisaidia kuogelea kwenye bahari ambayo imejaa maji mengi ya CCM na vifaa vyake vyote bunge, mahakama, polisi, jeshi na mamlaka zingine.

Mwanamkakati kazi yake kubwa ni kutumia kampeni ambazo zitahakikisha wapiga kura wanabadili mawazo yao juu ya chama kingine na kuwa tayari kuwapa kura.

Kazi zingine ni kufanya kura za maoni kuona kama chama kinakubalika kwa wapiga kura na kwa asilimia ngapi, kutumia teknolojia na mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe halisi wa kisiasa na pia kuendesha harambaee za kuchangisha mifumo ya chama ili kupata fedha za kujiendesha.

Ni hili suala namba tatu ndilo lingeiwezesha Chadema kujenga ofisi yake maalum ya makao makuu ambayo ingekuwa inatambulika rasmi badala ya kajumba ka pale Ufipa Street.

Siasa ambazo Chadema inaendesha sasa hivi za kudai katiba mpya haziwezi kuiyumbisha CCM hata kwa dawa.

Sanasana ni kwa wanasiasa wa Chadema na wafuasi wao kuketi chini na kupanga mbinu mpya badala ya maandamano ambayo ni dhahiri yatapata taabu kuruhusiwa na polisi.

Katiba ndo msingi wa sheria na hutoa mwongozo namna serikali inavyotenda shughuli zake za kila siku.

Hivyo katiba ya nchi ni muhimu na pia utaratibu mzima wa kutaka kuibadili pia ni muhimu.

Bado Chadema haiweki wazi kuwa yataka katiba mpya au mabadiliko ya katiba tulio nayo.

Lakini Chadema ingeweza kuketi na kushawishi ili kupata washirika kutoka CCM kwa maslahi ya taifa na kutaka katiba ifanyiwe marekebisho kuwa wabunge wasijiongeze mishahara kiholela.

Serikali ya awamu ya sita yapaswa kusikiliza dai la tume huru, hili dai ndo msingi wa vurugu zinazoweza kujitokeza hapa nchi ama leo au siku za usoni.

Kuna dalili zote zionyeshazo kuwa nguvu kubwa kutoka nje ya nchi ipo nyuma ya hizi kelele za katiba mpya au tume huru.

Suala ni je ni kelele za msingi au ni nguvu tu ya kutaka kuhakikisha CCM inaondolewa madarakani?

Kabla ya uchaguzi wa 2015 CCM ilikuwa imefikiriwa katika majukwaa ya kimataifa kuwa ni chama kilichohitaji kuondoka kupisha chama kingine ambacho kingekuja na mawazo mapya.

Ni pale CCM ilipompata hayati John Magufuli na baada ya miezi sita ya kwanza ndipo majukwaa hayo yalipobaini kuwa CCM huenda imejigawa ila ni ileile.

Kelele za Katiba mpya au tume huru ya uchaguzi hazitaisha leo.

Ila katiba mpya si rahisi kuipata bila kuwepo kura ya maoni ambayo ndo itatoa mwanga kuwa wananchi wanataka nini.

Hivyo kwa maoni yangu naona Chadema na wanaharakati wote wanapaswa kupigania kuwepo kura ya maoni.

Pia kuhusu tume huru ni kwamba ni lazima wabunge wa upinzani bungeni wawe na ushawishi wa kuweza kuleta bungeni wazo la kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo ndo itasimamia zoezi la uchaguzi nchini na kuhakikisha vyama vyote vya siasa vinahakikiwa vyanzo vya0o vya fedha.

Ili zoezi la uchaguzi lipate heshima ni lazima kuwepo tume huru ya uchaguzi ambayo pia itasimamiwa na Bunge kupitia kamati ya siasa.

Katika hali ya sasa ni vigumu sana kupata tume huru ya uchaguzi endapo wabunge wa upinzani hawazidi theluthi mbili ya wabunge.

Idadi kadhaa ya wabunge wakija na hoja na wakazidi theluthi mbili hiyo huwa ni shida tayari na ni lazima wazo lao lisikilizwe.

Ndo maana mwaka 1993 Marehemu Njelu Kasaka ambae alikuwa mbunge wa jimbo la Lupa huko Chunya akiongoza kundi la wabunge 55 kudai serikali tatu na serikali ya Tanganyika alizimwa na hayati Mwalimu Nyerere kwa kuwa tu ndie alikuwa mlezi wa chama na hoja yake ya kupinga hoja ya serikali tatu ilikuwabaliwa tu kwa kilichoonekana ushawishi wa kisiasa badala ya hali halisi.

Hivyo kwa maoni yangu napendekeza Chadema wajikite katika kujiandaa kuchukua majimbo ambayo yatawasaidia kuongeza idadi ya wabunge kule bungeni ambao wanaweza kuweka hoja yenye nguvu.

Hivi ndivyo chama cha MCP cha Malawi kilivyojipanga kukitoa madarakani chama cha DPP na ikawa hivyo. MCP walihakikisha wanapata wabunge wengi zaidi ili kuweza kuunda serikali na bunge.

Serikali isipuuzie hizi harakati za CHADEMA maana hii ni mikakati ya muda mrefu katika kuhakikisha nchi inaingia kwenye matatizo endapo matakwa yao hayatatimizwa.

Watanzania tunasifika kwa woga na upole kiasi cha kushindwa kuhoji hata uhandisi jamii unoendelea hivi sasa wa kuhakikisha miradi ya maendeleo inadhurika na isiendelee.

Katika duru za usalama, uhandisi jamii waweza kutafsiriwa kuwa ni kitendo cha kumshawishi mtu kufanya kitendo ambacho kitanufaisha au kutonufaisha maslahi yake.

Mtu au watu hao ni pamoja na matarishi, makatibu muhtasi au mamesenja na maafisa masijala.

Nina imani serikali yetu itakuwa makini na itatumia busara katika kujadiliana na Chadema ambao sasa hivi wamekuja kwa kasi.

Pia sina shaka na mazee na mkuu wao Mabeyo na wanakamati wengi ambao bado wanatatizwa na kinachoendelea.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Umeandika insha ndeeefu isiyo na tija! Unapoandika Tena try to stick on main points! Ingependeza Kama ungesimama hapo kwenye kuvuruga ustawi na amani ya nchi na ungetaja jina la nchi inayoisaidia cdm ili hatua za kidiplomasia zichukuliwe! But you failed to mention that county! Pole Yako Kwa muda ulioupoteza hapa!
 
Ok Tutor.

The motion is brought forward by alien forces.

Your point noted.
 
Kaandika hadithi za pwagu na pwaguzi.

Mataifa ya nje yakitaka kukinukisha CCM, Tiss, Polisi na jeshi watafanya nini?
Mnatumia silaha ambazo wao walizitumia miaka ya nyuma Sana.
Wao ndio walimu wenu wa ulinzi na usalama, wanawajua nje na ndani, na uwezo wenu.
Msidanganye watu kuwa mnaweza lolote
 
Waufufua kwa vurugu mchakato uloletwa na CCM na ukazimwa na CCM?

Nimepitia bandiko lako, nilichoona ni uandishi mzuri usio na tatizo la kisarufi kwa mantiki ya herufi kubwa na ndogo, koma ama nukta. Lakini bandiko lako halisadifu ulichosema ndani. Imekuwa kama mtu anayeandika kila kinachomjia kichwani bila kujali muunganiko wa alichosema hapo kabla. Kwa maneno marahisi uzi wako ungezeweza kutoa nyuzi 5 tano tofauti maana ni mada tofauti.

Halafu ww inaonekana kama ni mtu uliyekaa muda mrefu kwenye mifumo ya nchi, lakini mtazamo ama weledi wako umetekwa na propaganda. Ni hivi, hakuna chochote nchi za nje wanachotaka ndani ya nchi hii wakakosa kwa ccm, iwe ile iliyokuwa ya JK, Magufuli ama huyu mama wa sasa. Kama wanaweza kupata chochote tena bila usumbufu kwa ccm, kwanini waingie gharama za kuwaingiza wapinzani madarakani kwa kitu wanachoweza kupata kupitia ccm?

Kwa taarifa yako ww na wenzako zungukeni mtakavyo, tengenezeni conspiracy theories mtakavyo Lakini mjue katiba mpya ni takwa la wakati. Mnachoweza ni kuchelewesha kwa muda mfupi tu, lakini taka msitake katiba mpya ni lazima.
 
Chadema ni chama cha siasa chenye wanasiasa ambao si makini.

Ni chama kilichokusanya watu wanojiita wanasiasa lakini hawana mbinu za kuishi kwenye siasa.

Miaka mitano ilopita Chadema walipata shida na hawakuweza kujinafasi na serikali ambayo iliongozwa na raisi ambae hakuwa tayari kuvumilia vurugu iwe maneno au vitendo.

Sasa yupo raisi Samia Hassan huu ndo ulikuwa wakati wa Chadema kuketi chini na kupanga mikakati mipya ambayo itaendana na mwendo wa serikali ya sasa.

Nimewahi kusema mara nyingi kuwa Chadema haina wanasiasa makini ambao wanaweza kutofautisha siasa za vurugu na siasa makini za majibizano ya hoja kwa ustaarabu.

Pia nimewahi kusema kuwa Chadema imekosa wanamkakati au "strategists" ambao wataisaidia kuogelea kwenye bahari ambayo imejaa maji mengi ya CCM na vifaa vyake vyote bunge, mahakama, polisi, jeshi na mamlaka zingine.

Mwanamkakati kazi yake kubwa ni kutumia kampeni ambazo zitahakikisha wapiga kura wanabadili mawaqzo yao juu ya chama kingine na kuwa tayari kuwapa kura.

Kazi zingine ni kufanya kura za maoni kuona kama chama kinakubalika kwa wapiga kura na kwa asilimia ngapi, kutumia teknolojia na mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe halisi wa kisiasa na pia kuendesha harambaee za kuchangisha mifumo ya chama ili kupata fedha za kujiendesha.

Ni hili suala namba tatu ndilo lingeiwezesha Chadema kujenga ofisi yake maalum ya makao makuu ambayo ingekuwa inatambulika rasmi badala ya kajumba ka pale Ufipa Street.

Siasa ambazo Chadema inaendesha sasa hivi za kudai katiba mpya haziwezi kuiyumbisha CCM hata kwa dawa.

Sanasana ni kwa wanasiasa wa Chadema na wafuasi wao kuketi chini na kupanga mbinu mpya badala ya maandamano ambayo ni dhahiri yatapata taabu kuruhusiwa na polisi.

ambao wanaweza kuweka hoja yenye nguvu.

Mungu ibariki Tanzania.
The fear of the unknown. Acha uoga wa kupazia nchi za nje. Matatizo ya kwetu wenyewe inabidi tudeal nayo wenyewe
 
Nimepitia bandiko lako, nilichoona ni uandishi mzuri usio na tatizo la kisarufi kwa mantiki ya herufi kubwa na ndogo, koma ama nukta. Lakini bandiko lako halisadifu ulichosema ndani. Imekuwa kama mtu anayeandika kila kinachomjia kichwani bila kujali muunganiko wa alichosema hapo kabla. Kwa maneno marahisi uzi wako ungezeweza kutoa nyuzi 5 tano tofauti maana ni mada tofauti.

Halafu ww inaonekana kama ni mtu uliyekaa muda mrefu kwenye mifumo ya nchi, lakini mtazamo ama weledi wako umetekwa na propaganda. Ni hivi, hakuna chochote nchi za nje wanachotaka ndani ya nchi hii wakakosa kwa ccm, iwe ile iliyokuwa ya JK, Magufuli ama huyu mama wa sasa. Kama wanaweza kupata chochote tena bila usumbufu kwa ccm, kwanini waingie gharama za kuwaingiza wapinzani madarakani kwa kitu wanachoweza kupata kupitia ccm?

Kwa taarifa yako ww na wenzako zungukeni mtakavyo, tengenezeni conspiracy theories mtakavyo Lakini mjue katiba mpya ni takwa la wakati. Mnachoweza ni kuchelewesha kwa muda mfupi tu, lakini taka msitake katiba mpya ni lazima.
Dah! nimetekwa na propaganda sio?

Mwenzio hapa Dodoma nipo makini.
 
Mataifa ya nje yakitaka kukinukisha CCM, Tiss, Polisi na jeshi watafanya nini?
Mnatumia silaha ambazo wao walizitumia miaka ya nyuma Sana.
Wao ndio walimu wenu wa ulinzi na usalama, wanawajua nje na ndani, na uwezo wenu.
Msidanganye watu kuwa mnaweza lolote
Sisi tunajimwambafwai tu ila angalau katika ukanda wote wa maziwa makuu tunaheshimika.

Tishio nnalolizungumzia si silaha wala mabomu ni mbinu za kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom