Serikali rekebisheni za chaguzi vizuri twende mbele kama nchi!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Ukiangalia vizuri mapendekezo ya marekebisho ambayo vyama na wadau wanapigia kelele yarekebishwe ni ya msingi. Lakini sioni faida yeyeote ya maana kwa chama tawala cha CCM wala serikali kwa kuweka sheria nusu nusu na kuendeleza majibizano, maandamano na fikra kwamba chaguzi sio huru. Raisi samia ajiulize sana. Faida za kuweka mabadiliko ni chaguzi huru sasa Raisi samia ajiulize je hasara ni zipi? Hasara kwa nchi ni kubwa sana kuliko utakachopata.

1. CCM ikishinda kwa kuiba iba hamtajisaidia kwasababu hamtaweza kujipima na kujuwa wananchi wako wapi kwenye kuwaunga mkono. Ni bora 51% yako kuliko 80% ya wizi. Angalieni legacy ya Magufuli ilivyo haribiwa na chaguzi.
2. Sheria nzuri zitasaidia nchi iende mbele na kuacha kulumbana na vyama na wadau kila siku. Hii nchi inatakiwa kushindana na nchi nyingine na sio kila siku tulalamikie demokrasia ambayo hata ndani ya CCM inafaidisha watu ambao sio wazalendo tu. Hakuna mzalendo ambaye hataki demokrasia ya kweli.

Kama nchi hapa ndani tunatakiwa kushindana kwenye sera za maendeleo. Na demokrasia ni muhimu. Kama wananchi wanachagua mpinzani kwasababu ya kumuona mtu huyo anafaa zaidi ndiyo ubora wa hii system ya kibepari.

Raisi Samia usikofanya hivi kwanza wananchi watakosa imani na umuhimu wa kupiga kura. Lakini kibaya zaidi si vizuri wananchi kuishi na kusubiri mtu mmoja ndiye aje kubasilisha nchi nadala yake tuweke mifumo bora na ni kwa katiba bora.
 
Chama cha majambazi hakiwezi kubadili sheria za uchaguzi na kuweka tume huru, wanajua wakifanya hivyo asubuhi na mapema watatoka madarakani
 
Back
Top Bottom