View attachment 390212 View attachment 390213 View attachment 390214 j
Mkuu
Ndikusyaganya twende pamoja na kwa utaratibu,tutaelewena na mjadala utanoga.
Kwanza kumbuka sina haja ya kupotosha hapa jukwaani...Maana JF sio jukwaa la watu mbumbumbu.
Ni kweli unachanganya madesa,ama kwa kutokujua au kwa kuwa na taarifa nusunusu.
Bombardier ni Kampuni inayotendegeza ndege,kumbe Dash8 ni aina moja wapo ya ndege zinazotengenezwa na Bombardier.
Hivyo si mimi wala Gazeti ulilolisoma limepotosha,maana kama walisema Bombaridier Q400,maanake walifupisha tu wakijuwa wote wasomaji wataelewa,lkn kwa anayejuwa akiona "Bombardier Q400" anajuaa tu ni Dash8-Q400.
Hawa Bombardier wanatengeneza ndege za aina tofauti,Jet Engines na Turboprop Engines,ndege hizi zina matoleo tofautitofauti.Mfano mpaka ukafikie kwenye Dash8-Q400,maanake kuna Dash8-Q100,Dash8-Q200,Dash8-Q300 na sasa latest ni Dash8-Q400 ya kisasa na ndio Tanznia imenunua.
Kampuni hii pia hutengeneza ndege za Jet engines,ambazo zinatumiwa sana na Shirika la Delta la US na lile la Ujerumani.Ndge nzuri,ndefu kama mshare na za kisasa sana.Ndio Rwanda anamiliki kwa sasa baada ya kununua Dash8-Q400.Hizi za Jet engine zinaitwa Bombardier CRJ-900 Next Generation.
Kwa hiyo mtu akisema Bombardier S900(series) inajulikana tu ni CRJ-900,maana hizi CRJ nazo zina "series" ,ipo 700,800 hadi 900 ambayo ni latest kabisa.Kwa hiyo mkuu wangu Bombardier Q400 ndio hiyohiyo Dash8-Q400.
Ni sawa na kusema Toyota Mark II,Toyota Carina,Toyota Pick up,hizi zote ni Toyota lkn aina tofauti.
Angalia hapo kiwandani Bombardier,Mteja mzuri Rwanda...kanunua mwanzo Turboprop,alipoimarika akavuta CRJ jet engines.Na sisi ndio tumeanza.Tunavuta Turboprop kwa cash....Baadae tutavuta Jet hata kwa installment
Ni kweli wewe husafiri sana na ndege,ungekuwa unasafiri ungejuwa hayo maeneo yalivyo na abairia wengi.Kigoma,Tabora hadi Musoma Precision anaenda na abiria bado ni wengi