Mkuu
Kaveli raha ya JF ni kujadiliana,haimaniishi mi najuwa sana kuhusu Aviation Industry ila na-share tu na wadau.
Kiukweli miaka ya nyuma tulikuwa na ndege zenye majina tofautitofauti sana,Kulikuwa na Boeing737 yetu iliitwa Kilimanjaro,kulikuwa na Serengeti,Ngorongoro,Tarangire nk.Hizi ndege zilipaa kote duniani na kuitangaza nchi yetu.
Yalikuja "manyang'au" fulani yakitajirisha na kuliibia shirika mpaka sisi wengine tukaikimbia nchi na kutoa michango yetu ktk nchi jirani.Tulikuwa na Boeing ya kwenda Addis Ababa kupitia Entebe mara mbili kwa week.Tulikuwa na moja ya kwenda London-Heathrow!!Mpaka kuna wakati tulikuwa tunaenda hadi Ulaya Mashariki.Hii anga dunia ilitambua Call Sign yetu kama "Tango Charlie".
Wahuni fulani wakalila shirika,tunaojuwa tunaona juhudi za kurirudisha,hatukumpigia kura JPM...ila kwa hili tunampa pomgezi....Tunaiona heshima ya "Tango Charlie" katika anga ya dunia ikirudi.
Kwa swali zuri uliloniuliza,nakuzawadia picha ya BOEING737 iliyopewa jina la "KILIMANJARO" tazama katika picha(Kutoka maktaba ya kumbukumbu zangu) mali yetu sisi Watanzania miaka hiyo sisi tukiwa Vijana.Iwe kumbukumbu kwako na wengine,kuwa Taifa hili la Tanzania liliwahi kuwa ni Taifa la watu wenye akili sana na mawazo mapana...Lakini walikatishwa tamaa na wanasiasa,kama watapewa nafasi basi nchi hii itakuwa kimbilio la masikini wooooote wa Afrika na Dunia
Nakupa picha hii kukupa uthibitisho kuwa "SIBAHATISHI" ktk maelezo yangu(NA KULA SIKUMPA MAGUFULI NA CCM KUANZIA NGAZI YA UDIWANI HADI URAIS)
Cc
eddy MOTOCHINI UncleBen Belo Adharusi Papa Mopao View attachment 390180