Yametimia, ndege ya ATCL, Dash8-Q400 angani

Yametimia, ndege ya ATCL, Dash8-Q400 angani

Kama vitu hamvijui msiwe mnashabikia....Kwenye "Test Flight" kawaida landing gears zinakuwa nje tu.
mkuu, tayari lema keshadondoka presha iko juu kisa ndege,
 
barafu Tangu hii issue ya kufufuka kwa ATCL umekuwa ukijitahidi kufafanua mambo mengi sana licha ya kubezwa na watu wengi wasio na idea ya aviation industry.Hongera sana na usichoke kufafanua sisi Watanzania siasa imetufanya tumekuwa tunajua kila kitu
Tupo pamoja mkuu Belo ukinifuatilia humu michango yangu kwenye jukwaa la siasa,napingana sana na approach ya JPM juu ya upinzani na namna ya kuliingilia Bunge.Na huwa nakosoa kwa staha.

Lkn kwa hili la ATCL nipo pamoja na JPM kwa nguvu zangu zote.Ninaiona nia thabiti na uchaguzi sahihi wa ndege kutokana na ushindani wa soko.Hapa ninampa HEKO Rais
 
Mimi hofu yangu ni muda wa safari kuwa mrefu hivyo kushindwa kushindana na Fastest katika same root na hivyo kukosa faida na kushindwa kukua kibiashara. Sio mikoa yote ina idadi kubwa ya wananchi wanaweza kumudu kupanda ndege. Jamaa waumize kichwa na kufanya restructuring ya shirika sasa
Heko.
Ndiyo leo nimemsikia Waziri wa Uchukuzi akitetea ununuzi wa hizo ndege kwa kusema ni nzuri kwa mazingira ya Tanzania: zitatua katika viwanja vya changarawe (akatoa mfano kiwanja cha Musoma), viwanja vyenye runway fupi n.k.
Sasa nimejiuliza, hivi kwa soko na wateja gani hao wa kufanya shirika la ndege lipeleke ndege kila mahala Tanzania? Kwanini serikali isingenunua ndege za kuweza kushindana na FastJet (Airbus au Boeing) na kuanza na sehemu zenye soko na wateja wa ndege? Sasa kupeleka ndege Musoma (kama mfano) kuna ulazima gani?
 
Mimi hofu yangu ni muda wa safari kuwa mrefu hivyo kushindwa kushindana na Fastest katika same root na hivyo kukosa faida na kushindwa kukua kibiashara. Sio mikoa yote ina idadi kubwa ya wananchi wanaweza kumudu kupanda ndege. Jamaa waumize kichwa na kufanya restructuring ya shirika sasa

Hilo liko wazi kabisa, sidhani kama lita compete na Fastjet
 
mtaishia kusifia na kutoa mimacho lkn hampandi NG'OOOOOOOO
Mkuu mimi ndege kwangu sio "Chombo cha Usafiri" kama abiria anavyokuja kupanda.Hii kwangu ni ofisi,ninapoaga nyumbani kuwa naenda kazini...Ujuwe naenda angani kushinda huko.Nimeruka anga ya Tz nannikaamua kuja kuruka kwenye anga la nchi za watu.ATCL inarudi,nami nitarudi nyumbani kwa Mama Tanzania
 
Mkuu barafu kuna nyingine ina pangaboi mbele, hebu weka picha.
Pangaboi mbele?Hakuna kitu kama hicho,ndege yenye banga boi mbele ni zile ndogo single engine,ambazo ukubwa wake ni kubeba abiria13 au pungufu.

Bombardier ni double Engines…..jilidhishe kuona kuwa humu ndani kuna ndege ya ATCL iliyoletwa humu na single engine
 
Pangaboi mbele?Hakuna kitu kama hicho,ndege yenye banga boi mbele ni zile ndogo single engine,ambazo ukubwa wake ni kubeba abiria13 au pungufu.

Bombardier ni double Engines…..jilidhishe kuona kuwa humu ndani kuna ndege ya ATCL iliyoletwa humu na single engine
Mkuu tuliwekewa picha hapa jamii forums, ndege kama suzuki carry.
 
Mkuu barafu, binafsi nikupongeze sana kwa clarifications unazozitoa juu ya aviation industry. Pia naona ni jambo jema kwa serikali ya awamu ya 5 kujaribu kuifufua ATCL, hopefully shirika lita-excel.

Mimi nina mambo ambayo huwa sipati majibu:

Je, ATCL imewahi ku-lebel ndege zetu with 'KILIMANJARO' ? If NO, kwanini neno KILIMANJARO haliwekwi kwenye ndege zetu iwe kama njia mojawapo ya kujitangaza kiutalii?

Why tunashindwa kuutangaza Mlima wetu kwa kila namna iwezekanayo? Tuna matatizo gani sisi watanzania?

Natamani sana hapo nyuma karibu na picha ya Twiga, paandikwe neno 'KILIMANJARO'.

-Kaveli-
 
Hilo liko wazi kabisa, sidhani kama lita compete na Fastjet
Inapendeza sana kama mtu anajadili mada kama hizi,awe na ABC ya usafiri wa anga na changamoto zake.
Fastjet tunaenda kukimbiza sana sana.Kwa sbb yeye anatumia ndege aina ya A319 inayobeba abiria 156.
Sisi tunaenda kuwa na Dash8-400 abiria 78.Safari ya Mwanza to Dsm,ATCL inatumia saa 1.20 hadi 25 wakati Fastjet anatumia saa 1.10 hadi 15.ATCL anatumia tani 1.2 kwa safari hiyo,wakati fastjet anatumia tani 3.1 za mafuta JET A1 kwenda Mwanza.

ATCL anatuwa viwanja vyote Tz vyenye lami na vile vya vumbi,wakati Fastjet anatuwa viwanja vitano tu Tz kwa maana ya Mwanza,KIA,Dsm,Znz na Mbeya.Huku ATCL akituwa Kigoma,Tbr,Mbeya,Lindi,Mtwara,Arusha,Iringa,Songea,Musoma,Dodoma,Mpanda nk

Ili fastjet atuwe na kuruka,Runway ya kiwanja inatakiwa iwe km 2.3 wakati ATCL anatuwa kwenye kiwanja chenye 1.2 km,ambavyo ndo viwanja vingi vilivyopo Tanzania.

Kwa kulitambua hili,Fastjet ameamua kuanza kuuza ndege zake zooote,ili anunue walau E190 aendane na ushindani wa soko.Kuepuka ghalama za mafuta na vipuri.

Sasa hapo ni nani anamtishia mwenzake?Muwe mnafanya utafiti kabla ya kutoa mchango
 
karibu home kabajaj ketu ka taifa,wabongo wanaongea sana ujue watakuteta wakiwa humo humo umewabeba,usikasirike tu ukapitiliza kiwanja na kutua shambani km mwenzio yuleee wa zamani alivyofanya kigoma.
Ha ha haaa...so funny to be true!!
 
Back
Top Bottom