Sidhani kama hili jambo linawezekana. Vinginevyo, angetajirika kwa kuwakamata wanaume wote wa Tanzania. Angebuni tu namba za simu na kujaribu kutuma fedha. Angelipata majina yote ya mhusika na angelimfanyizia mpaka apate hela. Huenda ni hofu tu ya ndugu yako.
Cha kujiuliza hapa ni kuwa, je nduguyo alikuwa anasimamisha? Kwa kiwango gani? Una uhakika gani? Au hiyo ni njia tu ya kufikisha ujumbe wake kuwa mashine haisimami? Jibu sahihi angetupa mkewe ambaye kwa bahati mbaya sana hayupo humu.
Anyway, tuchukulie kama yote uliyoyazungumza ni sahihi. Cha muhimu cha kutambua ni uwa mtu ambaye wala hakufahamu hawezi tu kukufanyizia. Bila shaka atakuwa anafahamika vema na mhusika.
Kwanza, aache mara moja kutuma fedha kwa mhusika. Na amkemee kuwa hatotuma tena sumni.
Pili, ajielekeze katika maombi kutokana na imani yake. Amuombe Mwenyezi Mungu amsitiri na kumponya maswaibu hayo.
Tatu, nduguyo afike hospital kwa ajili ya matibabu. Namshauri asimuelekeze daktari juu ya swal la huyo mpumbavu wa nyota. Amuambie tu nimeacha kusimamisha uume kuanzia siku za hivi karibuni.
Apime pia kisukari, kikiwa kinaanza mwanaume anapoteza nguvu za kusimamisha kabisa. Kuna ugonjwa mwingine wa Coronary artery disease, apimwe.
Nne, kama ni mtu wa gambe aache kwa muda. Pombe inapoteza uwezo wa kusimamisha ikitumika kwa muda mrefu.
Tano na la muhimu zaidi, aondoe hofu na mawazo. Hii ni ishu ya kisaikolojia zaidi. Kuwaza huko kulikojawa na hofu ya kulogwa, kunaendelea kupoteza uwezekano wa kusimamisha.
Mpe pole nduguyo.