Mambo 15 ya kufanya ili usipigwe bei kwenye biashara

Davidmmarista

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2024
Posts
3,088
Reaction score
6,267
Habari Wana JF!

Mambo vipi ndugu zangu wa Jamiiforums? Leo nimeamua kuwaletea somo la biashara ambalo naamini wengi wetu tumewahi kulia machozi kwa kulipia bidhaa au huduma kwa bei isiyo halali.

Kama kuna siku nilipigwa hadi nikatamani nisirudi nyumbani, basi ni ile siku niliyoenda Kariakoo kununua power bank. Jamaa alinibebesha moja kubwa, yenye maandishi "20,000mAh Super Fast Charge" huku akinishawishi, "Hii ukiichaji mara moja, wiki nzima hujashika chaja!" Kwa furaha nikalipa bila hata kuuliza maswali. Siku ya kwanza nikaiweka chaji, ndani ya masaa mawili ikaisha. Nilipoifungua ndani, nikakuta betri ndogo ndogo za AAA zimejaa na mchanga kidogo juu. Hapo ndipo nilijua kuwa Kariakoo ina mafunzo ya maisha!
Kwa hiyo, ndugu zangu, kabla hujajiingiza sokoni na kuachia hela yako, chukua hizi mambo 15 ya kufanya ili usipigwe bei kwenye biashara, hasa hapa Tanzania.
1. Fanya Utafiti wa Bei Kabla ya Kununua

Usiwe na haraka ya kununua bidhaa bila kulinganisha bei kutoka kwa wauzaji tofauti.

Mfano: Ukiwa unataka kununua TV, duka la kwanza linaweza kukuambia "Bei ni 750,000", duka jingine likakwambia "Hii hii tunauza 580,000". Hapo ukikurupuka kununua kwenye duka la kwanza, umepigwa zaidi ya laki moja bila sababu.

2. Epuka Kushiriki Hamasa ya Kundi (Peer Pressure)
Unapokwenda kununua kitu na marafiki wanaokusukuma ufanye maamuzi ya haraka, unakuwa kwenye hatari ya kupigwa bei.

Mfano: Unakwenda kununua viatu, rafiki yako anasema,"Bro, hivi viatu vipo moto! Usikose hii dili!" Bila hata kuuliza bei kwenye maduka mengine, unalipa 120,000, kumbe dukani jingine bei halisi ni 75,000.

3. Chunguza Ubora wa Bidhaa kwa Makini
Usiamini maneno ya muuzaji tu, hakikisha umeichunguza bidhaa kwa macho na kuijaribu kabla ya kununua.

Mfano: Unanunua simu na muuzaji anakwambia ni mpya. Ukiona kioo kina mikwaruzo midogo na kipo loose, hiyo ni simu ya mtumba iliyoshafanyiwa 'refurbish'.

4. Jifunze Sanaa ya Kupatana (Bargaining Skills)
Usikubali bei ya kwanza unayoambiwa, jifunze kupunguza bei kwa kuongea kwa ustaarabu.

Mfano: Unakwenda sokoni, muuzaji anasema "Gauni hii ni 60,000," ukimwambia "Nina 30,000," anaweza kusema "Basi toa 40,000 tu uondoke nayo".

5. Epuka Kununua kwa Watu Wasiokuwa na Maduka Rasmi
Watu wanaouza mitaani au kwa njia za haraka mara nyingi wanakupiga.

Mfano: Umeenda Posta na unakutana na mtu anasema, "Simu original Samsung A52, bei ni 250,000, huku madukani ni 650,000!" Ukikubali, utarudi na simu ya mchina yenye rangi ya bluu ya ajabu!

6. Usiamini Ofa za "Bei Poa kwa Dakika Chache Tu"
Wauzaji hutumia mbinu ya kukulazimisha ukanunue haraka kwa hofu ya kupoteza fursa.

Mfano: Jamaa anakuambia "Mkuu, hii TV tunauza 450,000 kwa sasa hivi tu, kesho inarudi 600,000!" Ukikimbilia kununua bila kuuliza maduka mengine, unajikuta umepigwa.

7. Epuka Kulipa Kabla ya Kupewa Bidhaa
Kamwe usilipe hela kabla ya kupata bidhaa mkononi.

Mfano: Unataka kununua sofa na fundi anakwambia ulipe kwanza, atakutengenezea. Ukikubali, wiki inapita, mwezi unapita, mwisho wa siku unapigiwa simu "Nipo safarini, nirudi nitakutengenezea!"

8. Tumia Wataalamu Unaponunua Bidhaa za Bei Ghali
Kama hujui kitu, tafuta mtaalamu wa kukusaidia kufanya maamuzi bora.

Mfano: Unataka kununua gari, badala ya kwenda peke yako, tafuta fundi uliye na uhakika naye akague injini na mfumo wa gari.

9. Angalia Rekodi za Wauzaji kwenye Mitandao ya Kijamii
Kabla hujanunua kitu kwa muuzaji mtandaoni, angalia reviews na maoni ya watu wengine au njoo JF waungwana watakusaidia.

Mfano: Unataka kununua bidhaa kutoka kwa mtu Instagram, ukiona comment za wateja wa zamani zinasema "Huyu mtu ni tapeli, nililipia mzigo sijawahi kupata!" jua kuna hatari kubwa.

10. Usiamini Wauzaji Wanaotaka Ulipie kwa "Tigo Pesa" kwa Jina la Mtu
Unapotaka kununua bidhaa kutoka kwa kampuni, hakikisha unalipa kwa akaunti rasmi.

Mfano: Kampuni inaitwa "Smart Electronics," lakini unashangaa wanakwambia "Tuma kwa jina la Juma Fundi," hapo jua kuna kitu hakiko sawa.

11. Usikubali "Pesa haipo, utaletewa Bidhaa Kesho"
Kamwe usikubali ahadi za maneno matupu, hakikisha bidhaa iko tayari kabla ya kulipa.

12. Epuka Wauzaji Wanaosema "Unibebee Tu hii Pesa Nipate Nafuu"
Hii ni mbinu ya kukufanya ulipie kitu ambacho hukupanga kununua.

13. Angalia Sheria za Kurudisha Bidhaa Kabla ya Kununua
Wauzaji wengi hawakubali kurudisha bidhaa ukishalipa.

Mfano: Umenunua nguo na ukaona haikutoshi, ukirudi dukani, muuzaji anasema, "Hatupokei bidhaa zilizotoka dukani!"

14. Tumia Google na YouTube Kuelewa Bidhaa Kabla ya Kununua
Kama hujui bidhaa unayotaka kununua, angalia mapitio yake kwanza mtandaoni.

Mfano: Unataka kununua laptop, angalia YouTube kujua specs halisi, usije ukauziwa "Core i7" kumbe ni "Pentium 4"!

15. Usiwe Mrahisi Kuamini "Dili ya Ndani"
Dili zinazosemwa kuwa "za ndani" zinaweza kuwa mitego ya kukupiga bei zaidi.

Mfano: Unataka kununua kiwanja, mtu anakuambia "Nina connection ya mtu wa manispaa, nitakusaidia upate kiwanja cha bei poa." Unalipa, baadaye unagundua kiwanja hakipo kwenye ramani ya serikali.

Sasa ndugu zanguni wa JF, kama umewahi kupigwa, usijali sisi sote tumejifunza kwa njia ngumu. Lakini ukitumia mbinu hizi, hakika hutapigwa tena.
Nb.
Biashara ni uwanja wa vita, na mshindi ni yule anayejua mbinu za kuepuka mtego wa kupigwa. Kama umefika hapa, basi unajua jinsi ya kuwa mjanja sokoni. Nimekupiga nyundo 15 kichwani, sasa kazi ni kwako kuzitumia. Kama unajua mbinu nyingine za kuepuka kupigwa kwenye biashara, drop comment hapa JF!
 
Biashara ni uwanja wa vita, na mshindi ni yule anayejua mbinu za kuepuka mtego wa kupigwa. Kama umefika hapa, basi unajua jinsi ya kuwa mjanja sokoni. Nimekupiga nyundo 15 kichwani, sasa kazi ni kwako kuzitumia. Kama unajua mbinu nyingine za kuepuka kupigwa kwenye biashara, drop comment hapa JF!📌🔨
 
Unacho zungumzia ni utapeli Katika biashara. Aisee utapeli ni issue pana sana. Sio rahisi kuepuka.
Kikubwa ni kuwa makini Kila mahali.
 
Hii ni dalili kwamba wafanyabiashara hawajui kuwa uongo(hata katika biashara) ni chukizo kwa Bwana. Wafanyabiashara wanatakiwa kuwavuta wateja kwa maneno ya kweli, sio kwa kuwadanganya.

Vijana mnaomcha Mungu, tengenezeni T-Shirt zenye ujumbe huu:
Mungu
anachukia
UONGO
Mit 12:22

Mkizivaa na kutembea nazo mitaani, wafanyabiashara wenye hofu ya Mungu wanaweza kuacha "kuwapiga wateja" kwa maneno ya uongo.
Mungu Anachukia Uongo.jpg

Mithali 12:22
Mwenyezi Mungu anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
 
View attachment 3272718
Mithali 12:22
Mwenyezi Mungu anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh
 
NAMBA 5 hao ni mawinga duka moja wako 7-9.
Nitarudi
KAZI ni kipimo cha utu
 
Ukosefu wa ufahamu wa bei rasmi za bidhaa ndio hutumiwa na mawinga kuwapiga wateja bei
 
Machale muhimu sana kwenye pesa hata kama unafanya biashara na baba yako.
 
Unaweza kujikuta mjanja na ukajaa kwenye mfumo
Mfumo upi tena? Watu wanapigwa sababu ya kutojua,leo wanajuzwa mbinu za kujikwamua kutoka kwenye mtego wa wapigaji,wewe unasema watajaa kwenye mfumo,ninao wasiwasi kwamba na wewe ni mmoja wa wale wanaoitwa mawinga wa Kariakoo.
 
Back
Top Bottom