Yameanza kwa TRA yatafata kwengine, TRA kusimamia wenyewe ajira badala ya utumishi tunarudi kule kule kwenye ajira za ukoo na kujuana

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Mke: Mume wangu, mdogo wangu kile kipindi utumishi wanasimamia ajira hakupata kabisa.

Mme: Ni kweli utumishi walikuwa pasua kichwa, walituharibia sana, mambo ya connection yalipigwa panga.

Mke: Sasa Mama karuhusu Mashirika mjisimamie msaidie basi mdogo wangu.

Mme: Ondoa shaka, mdogo wako aombe tu, mengine ntamalizia

Nikiri kwamba kulikuwa na malalamiko ya utumishi kuchelewa kuita watu kazini ila ni vema hayo malalamiko yangefanyiwa kazi kuliko Rais kuruhusu taasisi ziajiri zenyewe,

Unadhani mabosi wataruhusu watoto wao ama ndugu zao wabaki mtaani kisha wewe usie na connection hata uwe na cheti kizuri upenye ? Ni ngumu sana hio!! Na ndio maana kulikuwa na utumishi ili kukabiliana na hili maana hata hao mabosi pamoja na elimu zao ni binadamu tena waafrika wenye utamaduni wa kuweka mbele watoto, ndugu, marafiki, watu wa kabila lao, dini yao, n.k.

Utumuishi pamoja na changamoto zake wengi tulijionea mambo ya connection yalipungua sana, watu hata waliotoka familia za chini ilikuwa kawaida sana wanapenya.

Ghafla mwezi wa pili Mama akatoa speech kwamba taasisi nazo waanze kujisimamia ajira, Balaa ndipo lilipoanzia hapa sasa linaloenda kuleta ubaguzi kwenye ajira.

Nimeona pia mitihani haifanywi sehemu moja ni mikoa tofauti tofauti, zamani wote mlikuwa mnaenda Dodoma ila kwa utaratibu huu mpya ni rahisi kuvuja mtihani.

Source"

Kuruhusu mashirika yajisimamie kwenye ajira badala ya utumishi

TRA Tangazo la kuitwa wenye Usaili
 
Mama hapo alikurupuka, kuna vigogo ndani ya TRA na nje ya tra waliotengeneza tatizo ili ionekane utumishi kuna shida. Mimi binafsi nimefanya kazi kwenye taasisi za serikali zinazoajiri zenyewe na zile zinazoajiri kupitia utumishi, nimeshuhudia undugunization wa hatari kwenye taasisi zinazoajiri wenyewe, kwa watoto wa mama ntilie nawataarifu tu kazi za TRA mtaishia kuziona kwenye matangazo tu, wale intake ya mwisho iliyobahatika kupenya kupitia utumishi ndio ilikuwa intake ya wasakatonge waliofunga mlango.

Mama samia nakuomba hili ulitizame kwa upana wake. Hapo TRA kuanzia mchakato wa kununua mfumo wa Ajira (takribani milion 700 imetumika) umegubikwa na ufisadi wa hali ya juu, fairness kwenye mchakato wa ajira kwa watanzania wasiokuwa na connection inakwenda kutoweka.

Suala la ajira kwenye taasisi/mashirika ya umma lisimamiwe na utumishi, inawezekana kuna mapungufu madogo madogo yapo utumishi nashauri ni vyema yangetatuliwa hayo luliko kuondoa kabisa mandate ya wao kufanya mchakato wa ajira kwa mashirika/taasisi za umma. Ni matumaini yangu utayasikiliza na kuyafanyia kazi haya. Bado haujachelewa.
 
Kweli kabisa ndugu, Ajira zingebaki utumishi, hii ya kuruhusu taasisi ziajiri ndio unakuta Taasisi imejaza watu wa Kabila moja au dini moja kisa Mtendaji Mkuu alikuwa wa Kabila Hilo au dino hiyo, yalishatokea
 
Hivi nini chema kwenu aisee. Yaani pamoja na malalamiko yote yale ya utumishi kweli mnalaumu Tena jamani
 
Hao utumishi walituhujumu sana wasabato kila usaili wanapanga jumamosi licha ya malalamiko walitia pamba masikioni bora ilivyorudi hivi na shida kubwa ni kutaka kuwafanyisha watu wote sehemu moja tu hivyo kuwa ngumu kupata venue kuwaaccomodate wote kwa hiyo inabidi kuweka siku isiyo na kazi na hivyo kuiweka jmosi huu uamuzi upo sawa kbs utaondoa hiyo shida
 
Hoja ya kipuuzi sana, Kwanza sahili nyingi huwa ni siku za kazi jumatatu hadi ijumaa, Pili hata ikifanyika jumamosi kwa wasabato huwa kuna ibada ya mchana.

ANYWAY!!

NImegusia mambo mazito yanayohusu mustakabali wa raia asiye na connection kupata ajira..na si siku gani usaili ufanyike.

Unaweza kufanya Huo usaili siku tofauti na ya sabato lakini bado ukakumbana na ukiritimba wa mfumo.
 
Hao utumishi walituhujumu sana wasabato kila usaili wanapanga jumamosi licha ya malalamiko walitia pamba masikioni bora ilivyorudi hivi na shida kubwa ni kutaka kuwafanyisha watu wote sehemu moja tu hivyo kuwa ngumu kupata venue kuwaaccomodate wote kwa hiyo inabidi kuweka siku isiyo na kazi na hivyo kuiweka jmosi huu uamuzi upo sawa kbs utaondoa hiyo shida
Una akili za kipuuzi puuzi sana. Ni matumaini yangu haupo kwenye utumishi wa umma.
 
Mke: Mume wangu, mdogo wangu kile kipindi utumishi wanasimamia ajira hakupata kabisa.

Mme: Ni kweli utumishi walikuwa pasua kichwa, walituharibia sana, mambo ya connection yalipigwa panga.

Mke: Sasa Mama karuhusu Mashirika mjisimamie msaidie basi mdogo wangu.

Mme: Ondoa shaka, mdogo wako aombe tu, mengine ntamalizia

Kulikuwa na malalamiko ya utumishi ila ni vema hayo malalamiko yangefanyiwa kazi kuliko Rais kuruhusu taasisi ziajiri zenyewe,

Unadhani mabosi wataruhusu watoto wao ama ndugu zao wabaki mtaani kisha wewe usie na connection hata uwe na cheti kizuri upenye ? Ni ngumu sana hio!! Na ndio maana kulikuwa na utumishi ili kukabiliana na hili maana hata hao mabosi pamoja na elimu zao ni binadamu tena waafrika wenye utamaduni wa kuweka mbele watoto, ndugu, marafiki, watu wa kabila lao, dini yao, n.k.

Utumuishi pamoja na changamoto zake wengi tulijionea mambo ya connection yalipungua sana,

Ghafla mwezi wa pili Mama akatoa speech kwamba mashirikika nayo yanaweza kujisimamia ajira, Balaa ndipo lilipoanzia hapa sasa.

Kwa sasa watoto wasio na connection itakuwa ngumu sana.

Nimeona pia mitihani haifanywi sehemu moja ni mikoa tofauti tofauti, hapa possibility za kuvuja mtihani nazo zimekuwa kubwa sana,

Source"

Kuruhusu mashirika yajisimamie kwenye ajira badala ya utumishi

TRA Tangazo la kuitwa wenye Usaili
Hapa tusubiri Zanzibar yote kuajiriwa
 
Nadhani labda ulizaliwa miaka ya 1996 umeanza kuomba ajira miaka ambayo kulikuwa na utumishi.

Subiri sasa uone hizo ajira ambazo taasisi zitajisimamia zitakuwaje, Mtajifunza kwa uchungu kwamba Taasisi zikiachiwa zenyewe ziajiri, mabosi wanaajiri watu wao wa karibu tu, nafasi zikibaki baki huko ndio wengine wanajazia jazia.

Utumishi kulikuwa na malalamiko ila ilibidi yarekebishwe tu na bodi ivunjwe iiingie nyingine, hauwezi kusema wti kisa nyumba ina ufa basi mhame, cha kufanya ni kuziba ufa.
Hiki kigezo si sahihi...kwani nani aliyekuhakikishia kuwa hizo taasisi hazitopanga usaili jumamosi?

Swala linalogusiwa hapa ni pana kuliko hoja yako. Though haki ya kuabudu ni ya msingi sana.

Mtoa Mada amegusia mambo mazito yanayohusu mustakabali wa raia asiye na connection kupata ajira..na si siku gani usaili ufanyike. Hizi ni hoja mbili tofauti.

Unaweza kufanya Huo usaili siku tofauti na ya sabato lakini bado ukakumbana na ukiritimba wa mfumo.
 
Hao utumishi walituhujumu sana wasabato kila usaili wanapanga jumamosi licha ya malalamiko walitia pamba masikioni bora ilivyorudi hivi na shida kubwa ni kutaka kuwafanyisha watu wote sehemu moja tu hivyo kuwa ngumu kupata venue kuwaaccomodate wote kwa hiyo inabidi kuweka siku isiyo na kazi na hivyo kuiweka jmosi huu uamuzi upo sawa kbs utaondoa hiyo shida
Hoja ya kipuuzi sana hii.

wasabato mmeanza shida zenu za vyuoni kwenye inshu za msingi kama izii za hatima ya ajira za wasomi wasio na connection za ajira

Ifike mahali mbadilike.
 
Utumishi naona wanenda kubaki kusimamia ajira za central government huku kwenye mashirika ya uma wanaenda kujisimamia naona na Tanzania Airports Authority (TAA) walitangaza ajira zao wenyewe means the processing wanafanya wenyewe watafuta kazi kazi tunayo
 
Hoja ya kipuuzi sana hii.

wasabato mmeanza shida zenu za vyuoni kwenye inshu za msingi kama izii za hatima ya ajira za wasomi wasio na connection za ajira

Ifike mahali mbadilike.
Hoja yake ya kipuuzi sana, kwanza sahili nyingi huwa zinafanyika siku za kwenda kazini jumatatu hadi ijumaa.
 
Back
Top Bottom