Kwanini baadhi ya taasisi na mashirika ya umma ajira zao hazipitii Sekretariet ya Utumishi?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,

Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake(Kama taarifa zitakuwa ni sahihi).

Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.

Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.

Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.

Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.

Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.

Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TAPE,TBA TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100

TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.

Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.

Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.

Nini kifanyike:

Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.

Mungu ibariki Tanzania
 

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Feb 1, 2015
1,695
2,000
Hata hiyo sekretarieti ya ajira ina loop holes nyingi pia. Hakuna mfumo rasmi unaonyesha ulinganisho wa waomba ajira.

Nikupe mfano TRA wametangaza kazi huko. Mara ya pili mfululizo lakini shortlisting inasuasua wakisubiri maelekezo Toka TRA. Kumbe happy tatizo lile la wachaga kubebana Bado halijaondoka.Sent using Jamii Forums mobile app
 

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Hata hiyo sekretarieti ya ajira ina loop holes nyingi pia. Hakuna mfumo rasmi unaonyesha ulinganisho wa waomba ajira.

Nikupe mfano TRA wametangaza kazi huko. Mara ya pili mfululizo lakini shortlisting inasuasua wakisubiri maelekezo Toka TRA. Kumbe happy tatizo lile la wachaga kubebana Bado halijaondoka.Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu ndo maana nimekuambia nitaleta uzi kuhusu urasimu pale psrs japo huwa inafanyika kwenye mashirika yanayolipa vizuri.
Lakini zile taasisi taabani hawana shida, nafasi za TPA mpka Leo hamna mtu aliyeitwa kuanza kazi ikiwa now psrs inatakiwa itumie siku 52 tangu tangazo linapotoka mpka mtu anapoitwa kuanza kazi
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,587
2,000
haya mambo ya urasimu ndiyo yanasababisha Tanzania tuendelee pole pole...

hivi TBC watake mtangazaji.. au mtu creative.. Mirald Ayo aombe .. mumzungushe kwa taratibu ndefuuu..
 

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,365
2,000
Kwa tabia za kibinadamu sio rahisi kumpa shavu mtu usiyemjua na hata wewe ukipewa opportunity ya kuajiri lazima uwaweke jamaa zako sema tunahitaji utaratibu mzuri tu
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
20,279
2,000
Hahaha nacheka kama mazuri ila jobseekers tunaweza kufa bila kuwahi kuajiriwa.
 

Jitu jeusi

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
1,698
2,000
Ila kwa upande wa PSRP sidhani kama tatizo lao n kubwa sana.

Mimi naona chakuboresha ni namna ya kufanya Mtihani usivuje tu.Sent from my GT-N7000 using Tapatalk
 

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Kwa tabia za kibinadamu sio rahisi kumpa shavu mtu usiyemjua na hata wewe ukipewa opportunity ya kuajiri lazima uwaweke jamaa zako sema tunahitaji utaratibu mzuri tu
Ndgu hizi issue zinatakiwa zifanyike taasisi Binafsi sio taasisi na mashirika ya umma au serikali kuu..
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,587
2,000
Unayafahamu madhara yake?

hata trump kampa vyeo mwanae, shemeji yake,....

hata toyota.. imejaa watu wanaitwa toyota surname kibao...

yule mama chief financial officer wa huawei aliekamatwa canada sijui marekani.. baba yake ndiye mwenye huawei...

museven kawapa vyeo ndugu zake kibao

hata rais wa wanyonge nae amewakumbuka ndugu zake na wapwa na marafiki zake...

hiyo ipo kila sehemu..

ndio maana wale wanaojijua wakali huwa hawalalamiki lalamiki.. wanakomaa wenyewe kwa kujiajiri au kwa kulazimisha mpaka wanapenya wanapopataka
 

okyo

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
2,006
2,000
Ni kweli mkuu ndo maana nimekuambia nitaleta uzi kuhusu urasimu pale psrs japo huwa inafanyika kwenye mashirika yanayolipa vizuri.
Lakini zile taasisi taabani hawana shida, nafasi za TPA mpka Leo hamna mtu aliyeitwa kuanza kazi ikiwa now psrs inatakiwa itumie siku 52 tangu tangazo linapotoka mpka mtu anapoitwa kuanza kazi
Mkuu kwanini TPA wamechelewesha hivo?

Inawezekana wamekusikia usishangae kesho wakatoa majibu hivo uvumilivu unatakiwa..

Kingine sidhan kama Ni rahisi kuweka watu wao maana majina ya walionde kwa oral interview yapo Na watakaokuwa selected majina pia tutayaona hivo Ni rahisi jua kama kuna udanganyifu maana sio rahisi nafasi zote jazwa Na watu waliopo kwenye kanzidata

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Hivi unajua unachoogeaa? Wewe unazunzungumzia nafasi za kisiasa.
Tofautisha nafasi za kisiasa na kitaaluma, halafu unachanganya kampuni au taasisi Binafsi na nafasi za kazi za taasisi na mashirika ya umma.
Fikirisha ubongo wako mkuu
hata trump kampa vyeo mwanae, shemeji yake,....

hata toyota.. imejaa watu wanaitwa toyota surname kibao...

yule mama chief financial officer wa huawei aliekamatwa canada sijui marekani.. baba yake ndiye mwenye huawei...

museven kawapa vyeo ndugu zake kibao

hata rais wa wanyonge nae amewakumbuka ndugu zake na wapwa na marafiki zake...

hiyo ipo kila sehemu..

ndio maana wale wanaojijua wakali huwa hawalalamiki lalamiki.. wanakomaa wenyewe kwa kujiajiri au kwa kulazimisha mpaka wanapenya wanapopataka
 

okyo

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
2,006
2,000
Kwenye udanganyifu kuhusu Secretariat ya ajira sidhan mana utaratibu wao uko wazi sana kama upo mdogo mno kwa hili nawapongeza Hawa jamaa kwa kweli wanatenda haki sana wasiojua tu ndo wanaweza sema kuna udanganyifu ila magufuli apa ameweka mambo sawa kabisa tumpongeze amewazuia wale walanguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,268
2,000
Wanafanyakazi kazi kwa kweli na wamepunguza urasimu kwa asilimia kubwa, tofauti na taasisi zikiachwa ziajiri zenyewe
But udanganyifu upo, nitaleta thread humu siku moja.
Kwenye udanganyifu kuhusu Secretariat ya ajira sidhan mana utaratibu wao uko wazi sana kama upo mdogo mno kwa hili nawapongeza Hawa jamaa kwa kweli wanatenda haki sana wasiojua tu ndo wanaweza sema kuna udanganyifu ila magufuli apa ameweka mambo sawa kabisa tumpongeze amewazuia wale walanguzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom