Barua ya wazi kwa Waziri wa Utumishi na PSRS. Msiturudishe nyuma kipindi cha giza kuu mkamgombanisha Rais Samia na wapiga kura

Upside Down

Member
May 6, 2023
14
29
Awali ya yote nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa juhudi kubwa iliyofanywa kuondoa au kupunguza upendeleo katika nafasi za kazi serikalini kwa kuunda chombo kimoja kitakacho simamia ajira za umma (PSRS) iliyo chini ya ofisi ya Raisi.

Ni kweli kuna mapungufu kadhaa ndani ya hiki chombo ambayo naamini yanarekebishika ikiwapo watu wanaongia hatua ya usaili wa mahojiano matokeo yao kuwekwa wazi(UWAZI KWA KANZI DATA), pia swala la PSRS kushindwa simamia kanuni na sheria zake ikiwapo baadhi ya taasisi na mashirika kugomea watahiniwa waliofaulu na kuwekwa kwa kanzi data wakati ni suala la kikanuni na sheria.

Suala kubwa lilonifanya niandike wakala huu ni baada ya kuona juhudi za wazi zinazofanywa kwa juhudi kubwa na wakuu wa taasisi kadhaa na mashirika wakisaidiwa na wanasiasa wenye maslahi binafsi kuhakiksha mashirika yao yanajitoa kwenye hiki chombo kwa madai rahis kama kucheleweshewa watu pia kupelekewa watu wasio na sifa(Uwezo).

Naomba ni tuleweshane jambo hapa,
Hao wanaoitwa hawana uwezo walichaguliwa kwa mujibu wa tangazo la kazi ambapo sehemu kubwa ya masharti/Requirements walizitoa taasisi husika, pia michakato yote muhimu ikwapo utungaji wa maswali mpaka usaili wa mahojiano wanashirikishwa.

Hao wanaosemwa hawana uwezo kuna muda wa matazamio wamepewa wa mwaka mzima wa kuwa tathimini kabla ya kuwapa mikataba ya kudumu ya kazi pia baadhi ya taasis kama TRA na nyingne zina muda wa kuwapika wahitimu wao kabla ya kuanza kazi na hata baada ya kuwa kazini.

Suala la kucheleweshewa watu ni swala ambalo taasisi husika zinaweza kuwa zinajitakia ili wapate hoja za kuharalishiwa matakwa yao binafsi sababu kanuni inasema kuna Kanzi Data tena unakuta ya usahili wa taasisi hiyo hiyo uliofanyika miezi michache nyuma yaani ndani ya ile valued time ya Data base na ndani yake kuna Candidate waliofanya vizuri taasis husika inagoma inataka usaili mwingine hapo lazima kuwe na delay kidogo ambayo isingekuwepo kama wangechukuliwa walifaulu kwa usaili uliopita wa taasisi lakini wakakosa nafasi.

Katika hili nampongeza Katibu Mkuu utumishi kwa jitihada alizoanza chukua tumeona hili kwa halmshauri kadhaa ikiwapo ya Misenyi kwa kusitisha saili sababu kuna watu kwa data base waliofanya vizuri, Sema Katibu Mkuu una full power and authority kwa mujibu wa sheria wa hata hizi baadhi ya taasisi zinazogomea Kanzi data kuzikatalia.

JAMBO JINGINE NI HILI
Inaonekana baada ya kuona harakati za kujindoa utumishi pengine ni ngumu ili kutimiza tamaa na matakwa yao Binafsi wamekuja na mbinu ya kuwapa ajira wanaojitolea ambalo kwa mujibu wa Naibu waziri Ridhwani Kikwete vikao vyake vimeanza toka Tareh 5 mwezi huu.

Ukweli njia ya kujitolea kutenda haki ya ajira ni ngumu sana kwa sababu hizi, Kazi za kujitolea kwenye hizi taasisi na mashirika zimekuwa za upendeleo mkubwa mno kuanzia taasisi binafsi moja kwa moja au Hata Taesa na mfano 1 ulio hai kipindi nipo chuo mwaka wa kwanza hata field nilikosa kabisa pakufanyia kila taasisi ambayo ningeweza fanya field kulingna na kozi yangu niliambiwa hakuna nafasi wakati kuna wengine walipata hata bila barua sababu ya connection.

Mwaka wa pili nijaribu peleka barua yangu Bandarini kulikuwa na barua nyingi za watu wa kuomba field mara kadhaa nilipokuwa naenda jibu niliambiwa njoo baada ya wiki mbili nilienda zaid ya mara 3 hizo wiki mbili mbili mara ya 4 dada mmoja aliyekuwa kwa mkataba ofisi ya HR alinionea huruma akanipa namba yake ya simu nilivyomtafuta alijibu atanisadia kupata yeye kama yeye lakini bila mtu kila siku utambiwa njoo baada ya wiki 2, nilipata kwa style hii, kitu cha ajabu nikiwa naendelea na field kuna siku Dada mmoja muajiriwa wa mkataba akaniuliza connection yako ni nani nikamwambia mimi sina connection ni Mungu alinipigania kupata, alikata katu hili jambo, mara kadhaa siku tofauti aliendelea niuliza mpaka nikamjibu fulan akasema huyo dada sawa fulan ni Mjomba wake ndo maana basi sisi sote humu hakuna alikuja bahati mbaya ndo maana nilikuwa nakuliza.

Nimetumia mfano wangu halisi wa nilivyo pambama kupata field kuna wengine mpaka wana maliza hawakuahi fanya field hizo intern au kazi mkisema mtoe kwa wanao jitolewa mnakosea sana wapo wengi wanatamani kujitolea lakini wanakosa hizo nafasi.

Pendokezo langu PSRS iendelee kujengewa uwezo na hata hizo nafasi za mikataba ikibidi wapewe kipaumbele Candidate walifanya usaili wa taasisi walio kwa kanzi data, baadala ya kuzichia taasisi husika au Taesa pia vikao anavyoendela navyo naibu waziri vya kujaribu kuwapa kazi wanajitolea kwa taasis visitishwe vinaturudisha nyuma kipindi cha GIZA KUU.

JOBLESS WERE WALKING DEAD.
 
Sidhani kama wanaweza ruhusu hili, la taasisi kujitoa sababu kuna mpango mkubwa wa kuifanya psrs kuwa chombo imara na siku zijazo hata zile taasisi ambazo bado zina ajili zenyewe nazo zipitie PSRS.Kuna ujenzi wa ofisi zao unaendelea unaogharimu bilion kadhaa kama sehemu ya mpango wa kuimarisha ofisi pia bajeti yao imeongezwa karibu mara 2

Jambo muhimu hapa ni Naibu waziri kusitisha vikao vya kutoa ajira kwa kigezo cha kujitolea itaturudisha tulipo toka
 
Back
Top Bottom