magilapeak
Senior Member
- Aug 6, 2013
- 132
- 27
Wakuu leo majira ya saa sita na nusu mchana nilienda kulipa school fees ya kijana wangu benki ya stanbic tawi la kariakoo sokoni, nikampa cashier bundle la pesa akazitia kwenye mashine, moja ya noti za shs 10000 ikakwama, basi cashier akatabasamu, akaniambia ile noti ni fake,nikaichukua nikaiangalia,water marks zote zipo vizuri,na sio fake, nikamuomba staff mwenzake pale receiption aiangalie maana mteja ndani mle nilikuwa mimi tu, akaangalia akasema iko sawa, niliporudi kwa cashier nikakuta ndani ya teller counter vijana wawili wako nae ndani, nikamrudishia cashier aendelee, yeye akang'ang'ania kuwa ni feki na wale vijana nao wakaangalia wakawa wanam-support yule cashier lakini nikaona kabisa ni mchezo wa kuigiza, nikamwambia anirudishe ili nimpe noti nyingine. hapo ndipo shughuli ilipoanza,mmoja wa wale vijana kule ndani mweupe hivi akasema haiwezekani, lazima tuitoboe akimaanisha mi niondoke au anikabidhi kwa askari, akiwa kama anaenitisha, sasa mle ndani niko peke yangu, ikabidi nimpigie jamaa yangu alie jirani na eneo ili anisaidie, akasema anakuja, nilipokata simu tu, yule kijana mweupe akaniambia chukua hela yako zoezi la kunikabidhi kwa askari likaishia hapo, tafsiri yake walikuwa wanataka kunidhulumu elf kumi yangu.sasa nimebaki na swali benki sio sehemu salama tena?