Bijou
JF-Expert Member
- Feb 25, 2011
- 1,249
- 360
Hawa watumishi wa benk waboreshewe maslahi yao waache tamaa,sisi wateja pia tuna shida zetu.
Mtanzania hata aboreshewe maslahi vipi, wizi umekuwa jadi kuanzia juu hadi chini kila mtu ajitafakari
Hawa watumishi wa benk waboreshewe maslahi yao waache tamaa,sisi wateja pia tuna shida zetu.
Kuna tawi moja la CRDB ilikua kila nikienda kutoa viburungutu nakuta 10, 20 au 30 imepungua. Kurudi siwezi na kuanza kuhesabia pale pale a bundle of 6m plus is a waste of time. Halaf very frequently ilikua nakutana na binti wa2 haohao. Ni sehemu ya kupanga foleni sio kwa namba. Vikaanza na kunichekea chekea kiasi kwamba hata wangekua wanatoa kilo nahisi ningechekelea tu! (ila namba ningechukua!)
Siku moja nikamgusia meneja swala hili kama bytheway wakati tunaongea maswala mengine. Akaniambia alishasikia na anashukuru mimi kumwambia tena. 2 weeks later dada mmoja nikamkuta customer care mwingine sijui alienda wapi?
Siitaji branch sababu swala lilishatatuliwa, hivyo ni vyema kuripoti!
Ww inaonekana ni mfanyakazi wa stanbic unauliza nguo alizovaa mteja ili iweje. Mchezo wenu umeshagundulika kawaambie staff wenzako waache.
Mchezo huo upo sana na Bandarini pale long room...kuna siku nilikua nalipia ushuru wa gari jamaa akaniliza 30,000 akasingizia zimepungua wakati pesa nilikuwa nimetoka kuzitoa bank muda huo huo na sijatoa hata sent. Nilikasirika na nilizua timbwili kubwa sana pale...yaani wezi sana bank tellers...kuna haja ya kutoa mimacho uangalie kila anachofanya hasa unapoweka pesa nyingi....
kuna mama alitaka kutapeliwa mil 1 na maTELLER wa crdb k'koo. Walidai hajahesabu vizuri badala ya mil 5 wakasema zipo mil 4. Akawauliza kuna mabunda mangapi? Akajibiwa manne, yule mama alimwomba waende kwa meneja wakacheki kwenye cctv zao maana amempatia mabunda matano, ikabidi kaunta ifungwe kwa muda . Waanze mahesabu, ikagundulika yule teller alipokea mil 5. Yule mama aliwaka sana akiwambia ni wezi..
Unaulizia nguo za nini badala ya kuwafundisha hao tellers wenzako customer care nzuri. Hivi mnajua kuwa sisi wateja ndio tunawawezesha kupata kazi hapo benki.ulikuwa umevaa nguo gani?
mkuu kwani kamera za CCTV hamna?ulikuwa umevaa nguo gani?