Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,935
- 30,280
Kwa hakika kipindi cha utawala wa Mwinyi hakupungukiwa na watu waliokuwa wanaona raha kumshambulia.
Ilisikitisha kuwa kulikuwa na magazeti yalimpa nafasi Reverend Mtikila kumshambulia Rais.
Kuna baadhi ya vijana wa wakati ule waliona wana wajibu na dhima kubwa ya kumtetea Rais pale ilipodhihiri kuwa hakuwa na mtetezi.
Nilikuwa mmojawapo wa vijana walioamua kumtetea Rais Mwinyi.
Namsoma Rais Mwinyi, ''Mzee Rukhsa Historia ya Maisha Yangu,'' na natingisha kichwa kwa mengi ninayokutananayo.
Natingisha kichwa kwa kuwa baadhi ya matukio na mambo yaliyomo kitabuni mimi na wenzangu tuliyafahamu kwa undani na tuliyaandika kwa yale yaliyostahili kuandikwa na mengine tuliyanyamazia.
Hapo chini kuna "Memories" post niliyoandika baada ya kutoka kumbukumbu za Rais Ali Hassan Mwinyi.
Ukiwa umesoma kitabu cha Mzee Mwinyi na ukawa umesoma kitabu cha Abdul Sykes (1998) utaona kuna mambo muhimu na mazito yamepishana kwa kiasi kikubwa.
Nilipata kumpa kitabu hicho Mzee Mwinyi nikiwa na nia akisome na ajue mchango wa Waislam katika kupambana na wakoloni kuanzia enzi za Vita Vya Maji Maji 1905.
Picha yangu hiyo hapo chini nikimkabidhi Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kitabu cha Abdul Sykes.