Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Ila kama Fidel Castro atafufuka leo, anaweza akafa tena kama atamuona yule Komando wetu mwenye Kitambi.

Komando unakuaje na Kitambi???
 
Jamani kama heading inavyosema, leo kwenye uwanja wa Uhuru kuna maonyesho yanafanyika, yanajumuisha gwaride la majeshi jwtz, polisi na magereza.

Niende kwenye kiini, Mimi leo katika maonyesho haya nimevutiwa sana na kikundi cha guard ya kimyakimya( silent guard)

Sio siri wamefanya vizuri sana hasa katika mambo yafuatayo:
1. Mageuko(turning), Mara zote wamegeuka kikakamavu sana na wanakata upepo balaaa
2. Jinsi ya kukondamachi( yaani msitari mmoja unaingia kwenye mistari mingine ili kupanga guard kuendana na urefu yaani watu wa mbele wabakie walewale na right marker abakie yuleyule, safi sanaaaa

3. Namna ya kubadilishana silaha, wamefanya kitendo hiki kwa uharaka na ukakamavu na bila kukosea(accuracy)

4.kwenye kunyoosha mistari wamefanya wonders, hongeraaaaa
5. Kiongozi wao Lt. Kilawe yule Dada mwenye kitala ameonesha ukakamavu safi sanaaaa

Hongera zao silent guard ya jwtz (infantry soldiers)
Najua kuna mengine umeyaona mwana jf karibu uyaweke hapa
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeniii

Interested na hii kitu for sure
 
Back
Top Bottom