Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,388
2,000

Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.

Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa

Rais wa Zanzibar,Dr. Ally Mohamed Shein,ndiye anayewasili uwanjani.

Jecha S. Jecha naye yupo uwanjani

Sasa anawasili Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan

Kumekucha sasa,Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,anawasili sasa uwanjani tayari kuanza kwa maadhimisho haya.

Rais Magufuli yuko kwenye gari maalum kuzunguka uwanjani na kuwasalimu wananchi. Katika gari hilo,yupo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Rais sasa amepanda jukwaa maalum kupokea salamu toka kwa jeshi. Gwaride liko chini ya Kamanda Luteni Kanali Makanya Eras. Wimbo wa Taifa na mizinga 21 vinarindima.

Rais sasa anakagua gwaride

Ukaguzi umemalizika. Rais anarejea jukwaa kuu. Vikundi vya jeshi vitapita mbele yake kwa heshima,kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka

Sasa vikosi vinapita mbele ya Rais kwa kutoa heshima

Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.

Sasa Makomando wanaonyesha uzoefu wao

Komando wanakunja nondo kwa mikono

Komando wanapigana kwa fito hadi kuvunjika

Sasa ni zoezi la kuvuja tofali kifuani na kichwani mwa komando

Komando analalia misumari mgongo wazi

Komando wanasukuma gari lililoharibika hadi kutembea

Kwata ya kimyakimya

Sasa vinafuta vikundi vitatu vya ngoma za asili

Sasa rais Magufuli anahutubia umati uliofika katika viwanja vya uhuru.
Rais anaanza kwa kutoa salamu huku itifaki ikiwa imezingatiwa.

Rais Magufuli: Niliamua kusitisha sherehe za mwaka jana kwa sababu kuu mbili; kwanza Sherehe za mwaka jana zingefanyika kabla sijaapishwa, pili sherehe zingegharimu shiling bilioni 4. Nilielekeza hizo bilioni 4 zitumike kujenga barabara.

Rais Magufuli:
Sherehe za miaka 55 ya uhuru nimeamua zifanyike hapa kwani zitakuwa ndo sherehe za mwisho kufanyika Dar es salaam, Sherehe nyingine zote zitafanyika Makao makuu Dodoma.

Rais anawapongeza wapigania uhuru na marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wote wastaafu.

Rais Magufuli:
Ndugu zangu watanzania katika bajeti ya mwaka 2016/17 tumetenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tumeanza miradi mbalimbali ikiwemo kinyerezi I,II na III.

Mpaka sasa tumeshanunua ndege sita kwa ajili ya kujenga uchumi na utalii wa nchi yetu.
Bajeti ya afya imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi bilioni 131.
Makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 850 mpaka wastani wa trilioni 1.2

Rais Magufuli: Tutaendelea kuchukua hatua kali ktk masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa. Tumepanga kuondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge
Ombi langu kwenu, tuendelee kudumisha amani yetu. Tudumishe pia umoja na mshikamano wetu tusisahau kuulinda muungano wetu. watanznia pia tuendelee kufanya kazi tuzingatia kauli ya hapa kazi Tuu.

Rais Magufuli: Tutajihidi kutatua kero zenu kwa uwezo wetu wote bila kubagua mtu kwa dini yake, kabila lake au chama chake.

Asanteni sana na Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru
 

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,288
2,000
Hicho Ni Chombo Cha Umma Hata Salary Huwa Hawapewi Kwa Kuombewa. Mkulu Kakwambia Kila Kitu Kipo Sawa,Ukweli Hao Wanaoshiriki Zoezi Wana Posho Zao Siyo Kuwaombea Chochote Kwa Matajiri
Posho zipi zilizositishwa?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,521
2,000
Unakuja kuwaombea hela kwa matajiri wakati bado watu wanaugulia maumivu ya hela za wahanga wa kagera? Nadhani katika taasisi zinazopata upendeleo hapa nchini ni pamoja na jeshi. Nenda kwenye maduka ya jeshi uone bei ya bidhaa. Hilo halitoshi bado? Mikopo kwao iko njenje. Anyway sio wazo baya kwa kile walichokifanya.
 
May 20, 2014
92
125
Nazungumzia kikosi cha komando ambacho kimeonyesha sarakasi na karate uchwara
Ndg waamini makomando wetu, usifikiri kwamba ni legevu wale jamaa.Km U.S.A na Italy zinawakubali makomandoo wetu Wa JWTZ na kifanya nao mazoezi ya pamoja, Kwa nini wewe uwadharau ? Wale jamaa in hatari sana , sana !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom