Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3: Shahidi wa 13, Tumaini Swila ashindwa kufika mahakamani. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Habari Wakuu,

Leo 10/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3. Shahidi Tumaini Swila jana Februari 9, 2022 aliomba ahirisho kwakuwa alikuwa hajisikii vizuri.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Swila aomba ahirisho kuwa hajisikii vizuri; kuendelea na ushahidi 10/02/2022

Baki nami.

Updates:

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Wakili wa Serikali, Nasorro Katuga: Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha Mawakili
  • Pius Hilla
  • Esther Martin
  • Jenitreza Kitali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha Mawakili
  • Jeremiah Mtobesya
  • Fredrick Kihwelo
  • Sisty Aloyce
  • Iddi Msawanga
  • Michael Mwangasa
  • Edward Heche
  • Gaston Garubindi
  • Hadija Aron
Wakili wa Serikali Nasorro Katuga: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameshauriwa na Daktari Kupumzika na sisi hatuwezi Kwenda Kinyume na Ushauri wa Daktari Pia tungeweza Kutafuta Shahidi Mwingine wa Kuendelea naye ila Kwa Muda wa Jana na leo isingetosha Kutafuta Shahidi Mwingine

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tuhairishe Kesi Mpaka Jumatatu, Kama atakuwa bado hajapona tunaweza Kutafuta Shahidi Mwingine Pia Mheshimiwa Jaji Kwa kutii Agizo la Mahakama Shahidi ameweza Kumtumia Ndugu yake aweze Kuja na Cheti cha Hospitali, lakini Original yake anaweza Kuja nayo yeye Mwenyewe pale atakapo pona

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba kama Dakika Moja na sisi tuweze Kuangalia Cheti cha Hospitali.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tumesikia Hoja ya Ndugu yangu Nassoro Katuga Nikianza na Hoja yenyewe ya Nyaraka Kutoka Hospitali, Nakumbuka Wakati natoa Hoja Jana, Tuliomba Shahidi atuletee Karatasi Kutoka Hospitali ya Serikali ambapo pia nafahamu Kwamba Askari Polisi anapopatwa na Ugonjwa anatakiwa kwenda huko, Nyaraka Walio leta Wenzetu Inatoka TMJ Super Polyclinic hii siyo Hospitali Ya Serikali Nyaraka hii inazidi Kuweka Wasiwasi zaidi Kwa Nini Mtu aende Kwenye Hospitali ambayo Haifahamiki

Nafikiri Jana tulikubaliana kuwa aje na Uthibitisho kutoka Hospitali ya Serikali Naomba Mahakama Ione kuwa sababu haina Logic wala hazipo Kama Mahakama itaona tofauti Basi Wenzetu Wasisitizwe

Kwa Mujibu Sheria Kesi katika Mahakama hii inatakiwa iishe ndani ya Miezi 9 Tukienda Kwa Mwenendo huu tutalazimika Kuomba Muda wa Nyongeza Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Jaji: Hoja ya Kuhusu airisho Sijaona kama Umezungumzia Kuhusu Muda wa airisho

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Jumatatu ni Mbali sana, Kwa Vyovyote itakayokuwa, Sasa ni saa Nne, Mpka Kesho Saa Nne ni Zaidi ya Masaa 24 Wana akiba ya Mashahidi 11 zaidi. Basi tutafute kati hao Mashahidi 11 angalau tuairishe Kwa Leo tuweze Kuja Kuendelea Kesho

Wakili wa Serikali Nasorro Katuga: Mheshimiwa Jaji Tumesikia Hoja ya Wenzetu Kutoka kwa Wakili Peter Kibatala Wenzetu Wanasema Kwamba Shaeria na Tangazo la Serikali namba 259 inataka Kumaliza shauri hili ndani ya Miezi 9 tunalifahamu na tumelichukua

Suala la tukishindwa Kuleta Shahidi huyu, tulete shahidi Mwingine nalo tumelichukua Suala la Shahidi Kuleta Cheti cha Hospitali ya Serikali, Shahidi Tulikuwa tunaona hapa tangu Mwanzo Kila Muda alikuwa anaomba Kwenda Msalani Huko Ndipo alipo kuwa anatibiwa kupitia Daktari Wake

Kupata tiba kutoka kwa Daktari Wake ni Nusu ya tiba, Kuhusu Wasiwasi Wa hapo anapotibiwa wanaweza Kwenda Kuuliza na Kuonana na Daktari Wake. Tunasisitiza Sisi Ka Maafisa wa Mahakama hatufurahishwi na airisho Lolote Pasipo Sababu.

Kuhusu Kuairisha Mpaka Kesho na Sitakukubali Kwamba tuje Kesho halafu tukaja na Hadithi ya Kukosa Shahidi. Ndiyo Maana tukaomba tuahirishe Mpaka Jumatatu ili kama Shahidi hata Kama anatakiwa Kusafiri atakuwa amefika

Sisi tunaona Kuwa ni Busara Kuairisha Mpaka Kesho halafu tukaja na story, Mahakama Yako itachoka Kutusikiliza. Sisi tunaomba tupewe airisho Mpaka Jumatatu. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Mahakama ipo kimya kusubiri uamuzi mdogo wa Mheshimiwa Jaji (10:15 AM)

Bado Mahakama ipo kimya (10:27 AM)

Jaji: nimesikia Hoja zilizotolewa na pande zote mbili Kama ambavyo Imetolewa na Upande Wa Mashtaka Mahakama hii imekuwa na Spirit ya Kutaka Shauri liishe kwa Haraka nimekuwa nikisisitiza Mawakili wa pande zote Mbili kuzingatia Spirit hii

Ila jana Wakati Shahidi anatoa Ushahidi wake, Shahidi Aliomba Kusitisha Kutoa Ushahidi Na Kwenda Kupata Matibabu Maombi hayo Kwa kuwa yalikuwa ya Msingi, Mahakama Ilielekeza Kuwa Shahidi atakapo rudi Mahakamani Hapa atalazimika kululetea Uthibitisho

Mahakama Haikusema Uthibitisho huo lazima utoke Hospitali ya Serikali, Kwa sababu suala la Matibabu ni la Mtu Binafsi Mahakama ilisita Kutoa Maelekezo hayo Ingekuwa inaingilia Mambo Mengine

Nyaraka iliyokuja hapa Shahidi amepata Uthibitisho Kuanzia Tarehe 9 Mpaka 11 February

Kwa Maana hiyo Shahidi Kwa Kesho Hawezi Kuwepo Upande wa Mashtaka Wanasema Kwamba hawawezi Kuomba airisho Mpaka Kesho Sababu wanaogopa Kuja Kesho bila Shahidi.

Kwa sababu hiyo ni Busara Ya Mahakama Inaona ni Vizuri Kuairisha Mpaka Siku ambayo Shahidi ataweza Kuja Mahakamani

Kwa sababu Hiyo naairisha Mpaka Jumatatu na Kuelekea Upande wa Mashtaka Kuhakikisha Kuwa Jumatatu wanakuja na Shahidi hata Kama yule atakuwa bado hajapona Waje na Mwingine

Kwa Maana hiyo na airisha Shauri Mpaka Jumatatu Saa 3 Asubuhi na Washtakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Siku hiyo

Jaji anatoka
 
Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Zamani wakati wa mtihani tulikuwa tunakwenda kusoma " nyenzo" chooni.

Baadae chooni akawekwa mlinzi ili kutia hofu wapiga chabo.

Labda vyoo vya mahakama zifungwe camera ili kesi hii iende haraka na iishe.
Katika historia ya JF umekuwa mkweli. Leo na kesi hii UCHAWA WA CCM umeuweka pembeni, umeangalia Haki (Kama huna hidden ill motive anyway)
 
Back
Top Bottom