Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu ya CDM 30.04.2011

Mimi nawasubiri Dr Slaa na Zitto watujuze maana wao ni members humu....huyu Jini Brain mzushi mtupu
 
Mkuu hili sio kweli kwani masharti ya ununuzi wa vifaa chakavu ni katiba ya Taifa, haizuii vyombo vingine nje ya serikali kutofanya hivyo. Na hakuna mahala popote ktk katiba ya chama inazuia chama kutonunua vitu chakavu iwe ya CCM,CUF,TLP au CDM. nenda maofisi mwao utakuta vitu chakavu na mkuu wangu unajikuna pale unapoweza.

Swala la Zitto kupinga ununuzi huo ni wazo lake kupinga ununuzi huo na haihusiani na sababu za kitaifa kutonunua vitu chakavu, ila ni ushauri ambao hutokea ktk vikao vyovyote vile. Hata mimi naweza pinga magari kununuliwa toka India, haina maana maamuzi ya CDM kununua magari India ni Ufisadi bali napinga wazo hilo unless nitaonyesha ufisadi umefanyika vipi..

Mkuu tunachosema ndicho tukitende , na mara nyingi CDM wao wamesema watatenda watakacho sema. Hili la ununuzi wa magari chakavu lina harufu ya rushwa ndani yake na ndio maana wakina Prof. baregu, Dr. Kitila , Zitto waliliona hilo. Ni aibu kubwa kwa cdm kusema , halafu dhamira waliyo nayo moyoni mwao sio hicho wanacho sema mkuu
 
Mimi nawasubiri Dr Slaa na Zitto watujuze maana wao ni members humu....huyu Jini Brain mzushi mtupu

Mkuu kubali ukweli tujivue magamba, ukiona na wao wako kimya ujue ni ukweli mtupu mie huwa sibahatishi na ninayo yasema. Silence means YES !
 
Huwezi elewa kwani umeisha ziba masikio na macho. Tofautisha ununuzi wa gari lako na mkeo, na wa chama cha siasa. Kama chama cha siasa inabidi uonyeshe kwa vitendo kile mnacho hubiri, sio nyie na wabunge wenu mnahubiri vitu chakavu visinunuliwe serikalini na kwenye halmashauri kwani kufanya hivyo mtaruhusu mwanya wa ufisadi ? sasa nyie mnataka kununua vitu chakavu huo kwenu sio ufisadi ? au ufisadi ni kwa serikali tu ? jivue gamba !
Samahani nilikuwa nimetoka kidogo hivi unaweza kuniambia ni magari mangapi hadi sasa yameshanunuliwa na Chadema kuthibitisha huo ufisadi.
 
Mkuu kubali ukweli tujivue magamba, ukiona na wao wako kimya ujue ni ukweli mtupu mie huwa sibahatishi na ninayo yasema. Silence means YES !

Tatizo ni kukataa kwako kuelewa......serikali inabanwa na PPA kama sheria lakini taasisi zilizo nje ya mfumo wa kiserikali hazizuiwi kununua mali chakavu ikiwemo hata CCM ina magari ya mtumba...na hii PPA ni directive ya World Bank....wewe unahusiha CDM...kwa hiyo unataka turudi kununuwa Dowans just kwa sababu CDM wanataka kununua magari mtumba?...wewe unaendesha gari mpya?
 
Samahani nilikuwa nimetoka kidogo hivi unaweza kuniambia ni magari mangapi hadi sasa yameshanunuliwa na Chadema kuthibitisha huo ufisadi.

Slaa si yumo humu mwambieni ajibu hili, kama yeye ni mkweli kweli. Na akipindisha tutamuumbua kwani taarifa zote tunazo
 
Tatizo ni kukataa kwako kuelewa......serikali inabanwa na PPA kama sheria lakini taasisi zilizo nje ya mfumo wa kiserikali hazizuiwi kununua mali chakavu ikiwemo hata CCM ina magari ya mtumba...na hii PPA ni directive ya World Bank....wewe unahusiha CDM...kwa hiyo unataka turudi kununuwa Dowans just kwa sababu CDM wanataka kununua magari mtumba?...wewe unaendesha gari mpya?

Nashangaa uelewa wako kwa nini ni mdogo kiasi hiki, unataka kufananisha ununuzi wa gari lako la familia (private use) na la chama (public use), ni vitu viwili tofauti. Na hata CCM wao hawajawahi kununua magari mitumba, wakati wa uchaguzi waliingiza magari mapya ya Landcruiser hardtop (mkonga) 110 yote mapya, ww hiyo ya kusema magari chakavu walinunua uliipata wapi? toa data. Sasa nyie hii rushwa ya kununua vitu chakavu itawaponza wakuu jirekebisheni bana
 
Slaa si yumo humu mwambieni ajibu hili, kama yeye ni mkweli kweli. Na akipindisha tutamuumbua kwani taarifa zote tunazo
Wewe ndiye umeanzisha thread nafikiri una taarifa zaidi ni magari mangapi yamenunuliwa ili tuwabane zaidi.
 
Wewe ndiye umeanzisha thread nafikiri una taarifa zaidi ni magari mangapi yamenunuliwa ili tuwabane zaidi.

Yeye mwache ajibu hili, ila nampa dokezo tu hizi gari chakavu za Maraj za india , kwani mpaka aina tunaijua !
 
Nashangaa uelewa wako kwa nini ni mdogo kiasi hiki, unataka kufananisha ununuzi wa gari lako la familia (private use) na la chama (public use), ni vitu viwili tofauti. Na hata CCM wao hawajawahi kununua magari mitumba, wakati wa uchaguzi waliingiza magari mapya ya Landcruiser hardtop (mkonga) 110 yote mapya, ww hiyo ya kusema magari chakavu walinunua uliipata wapi? toa data. Sasa nyie hii rushwa ya kununua vitu chakavu itawaponza wakuu jirekebisheni bana

Ha ha haa.......nadhani wana JF wengine wameshaongelea uelewa wako mdogo kuhusu sheria ya manunuzi....nimekupa mfano mdogo hujaelewa...kwa heri...na utabakia kama yule fisi aliyekuwa anasubiri mkono uanguke....mimi nimeyaona magari mengi to ya CCM ya mtumba....hatuhitaji kutoa data
 
Mnatuchanganya wanachadema wachanga,tumekimbia ccm mambo kama haya sa mnataka kutupeleka kulekule.

Tafadhali chondechonde cdm msiondoe ile imani tuliyowapa
 
Mkuu kubali ukweli tujivue magamba, ukiona na wao wako kimya ujue ni ukweli mtupu mie huwa sibahatishi na ninayo yasema. Silence means YES !

Mkuu hapa unabahatisha, na unatumia nguvu nyingi bila sababu. Twambie magari hayo yamesha nunuliwa? kama swala lipo kwenye mjadala kabla ya kununuliwa hapo ufisadi uko wapi? Kama kikao hakijaisha na wewe unatangaza ufisadi kwa nguvu zote tukueleweje? unachuki na CDM, ufisadi au magari mitumba? Umeweka thread wacha tuijadili bila mwongozo wako, labda utuambie nia yako ilikuwa kupandikiza chuki. Mbona magari mabovu aina ya Korando yaliletwa na CCM kutoka India yakafa yote baada ya muda mfupi hujayasema hapa!
 
Hili suala la magari chakavu limemuumbua sana Slaa kama mtendaji mkuu wa chama, kwa kusema asivyotenda ! Slaa ni ndugu na mapacha 3

Hoja ya kununua magari chakavu ni kwa ajili ya matumizi ya serikali, taasisi za serikali na mashirika ya umma ambayo huratibiwa na kusimamiwa na serikali. Serikali ina uwezo wa kununua magari mapya kwa kuwa ina uwezo kifedha.

Vyama vya siasa vina uhuru wa kupima uwezo wao na hivyo kununua magari yake kadiri wanavyoona uchumi unawaruhusu. Kuna magari mengi yaliyotumika kwa bei nafuu na ni ya kiwango cha magari mapya, bora hayo kwa vile pesa zilizopo zinaweza nunua magari kiasi hicho na kama wataamua kununua mapya kiwango cha pesa kilichopo hakitatosha.

Hoja ya manunuzi vyombo vilivyotumika inaihusu serikali, taasisi za serikali na mashirika ya umma, hivyo hoja hiyo haina nguvu kwa vyama vya siasa na hakuna sheria ya nchi inayovibana vyama vya siasa kununua magari mapya.
 
All politicians are the same... Especially linapokuja suala la fedha!

Mkuu nilishawaambia kuwa vyama nimikusanyiko ya wasaka tonge. Hakuna chama chenye uchungu na nchi hii, maslahi binafsi mbele. Ila la kununua magari mitumba inategemea pesa zinatoka wapi kama ni Government Funds wanatakiwa wafuate the Public Procurement Act, 2004 (and its regulations) ambayo inakataza kununua vitu chakavu, lakini kama ni za kwao basi itategemea sera zao walizojiwekea juu ya manunuzi ya vitu/vifaa ndani ya chama chao. Kununua magari mitumba hakuwezi kuwa ufisadi ila kama kuna msukumo mwingine nyuma yake kama alivyosema mmoja wetu hapo kwamba kulikuwa na 50m ya bakshishi!!
 
Geniusbrain.
Mkuu labda iweke hapa sheria ya SERIKALI ya manunuzi, isome tena vizuri labda utaelewa. Unachosema ndicho tukitende sii lazima iwe hivyo kwa sababu wapo marafiki zangu wakristu huandaa chakula halali ktk maswala ya Jumuiya (harusi au misiba) lakini wao wenyewe majumbani mwao hula hata nguruwe na hawana uharamu. Na wala sii jambo la ajabu kwa baadhi yao kusema hawataki kula nguruwe..
 
Mkuu hapa unabahatisha, na unatumia nguvu nyingi bila sababu. Twambie magari hayo yamesha nunuliwa? kama swala lipo kwenye mjadala kabla ya kununuliwa hapo ufisadi uko wapi? Kama kikao hakijaisha na wewe unatangaza ufisadi kwa nguvu zote tukueleweje? unachuki na CDM, ufisadi au magari mitumba? Umeweka thread wacha tuijadili bila mwongozo wako, labda utuambie nia yako ilikuwa kupandikiza chuki. Mbona magari mabovu aina ya Korando yaliletwa na CCM kutoka India yakafa yote baada ya muda mfupi hujayasema hapa!

Mkuu kwenye uchaguzi wa 2005 CCM walinunua Double Cabin aina ya Mahndra toka India na Agent wa Mahndra hapa Tanzania ni Noble Azania (Jeetu Patel). Sina hakikakama walinunua au walipewa msaada! Ila yote yako kwenye mawe!!
 
Genuiabrain, pole sana kwa kupoteza muda wako, hapa jamvini kuna greater thinker, Leo umekula? Chukua panadol kisha meza ili kesho tena teoa
 
Kwani katika chadema kuna sera ya manunuzi? Kama ipo inasemaje? Kama haipo kuna ubaya gani kushindanisha hoja juu ya huo mpango?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom