Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu ya CDM 30.04.2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu ya CDM 30.04.2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, May 2, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kilichojiri kikao cha kamati kuu ya CHADEMA siku ya Jumamosi tarehe 30.04.2011
  Ø Zitto apinga mpango wa ununuzi wa magari ya Chama ya mitumba kutoka India yenye thamani ya Tshs 480 milioni. Ambapo Prof. Baregu ,Dr. Mkumbo na Mnyika nao wanaunga mkono hoja hiyo
  Ø Lema ataka Zitto ang’olewe kutokana na kupinga wazo hilo la ununuzi wa magari ya mitumba (chakavu), na kumshutumu kuwa anamtetea Shibuda
  Ø Zitto amwambia Mbowe mpango wake wa kujenga makundi ya mtandao utakuja mletea matatizo
  Ø Kamati kuu yatengua uteuzi wa Shibuda wa kukaimu uenyekiti wa chama Shinyanga , na kundi linalo mpinga Zitto kumshutumu kuwa akikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao
  Ø Wakati wa mvutano huo Dr. Slaa alikuwa kimyaa na hakusema lolote
  Ø Shibuda akiri kusikia taarifa hizo na anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vya maamuzi

  Source : Mwananchi 02.05.2011

  My note :
  1. CDM wanahubiri wasicho kitenda kwani mpango wa kununua vitu chakavu wao wanajifanya kuvipinga kumbe ndio wanataka kuvitekeleza
  2. Lema ni kimeo kwenye Chama kwani anaonekana ni mpambe wa kundi la Mbowe. Na Lema anaonekana ana visa na Shibuda, kwani Shibuda wakati wa kikao cha bagamoyo alimwambia Lema hana adabu na ataenda kumshitaki kwa wazee wa Arusha
  3. Kitendo cha Slaa kukaa kimya ni kuona aibu kwa hoja yake ya kifisadi (kama mtendaji mkuu wa chama) ya kununua magari chakavu
  4. Uamuzi wa kumvua Shibuda madaraka ni wa kukurupuka kwani ulipitia vikao halali vya chama vya shinyanga
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  chadema sio chama cha zidumu fikra za mwenyekiti
  Ni halali kutofautiana ila muhimu ni kwa maslahi ya nini hasa?binafsi au chama?mwenyekiti anakosoleka,zitto anakosoleka.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani haya magari yamechakaa kiasi, gari kama ni grade 5 kwa hali ya uchumi ya Tanzania ndi yanayonunuliwa na watanzania wengi, Na tofauti yake na magari mapya ni ndogo sana. Badala ya kununua gari mbili, wanaweza kununua gari 20 na zikasaidia kampeni hadi zaidi ya 2015.

  Do a proper evaluation, sio blabla. Chakavu is a relative term.:help:
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tatizo lenu mnacho hubiri sicho mnacho kitenda, Slaa ilibidi awe mpole , hili dili lingepita angekuwa na cha kwake Tshs 50m. Matendo yenu yanaaanza kudhihirika kwa watanzania kumbe mpo kwa maslahi yenu binafsi
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tetea tu ila hakuna hoja hapo yenye mashiko ! ufisadi utawamaliza
   
 6. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  All politicians are the same... Especially linapokuja suala la fedha!
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama hali yenyewe ni hii , nimeanza kuamini wale mapacha 3 kuwanunua hawa viongozi wa CDM ili wawatetee !
   
 8. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hoja unaianzisha, unaijadiri na kuitolea hitimisho wewe mwenyewe. Hypocrisy of highest order
   
 9. i

  ismila Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ufisadi sasa umehamia chadema?wanaka kununua mitumba!kweli rangi ya kinyonga sio rahisi kuijua mpaka awe kwenye mazingira flani kama hayo ya pesa kwa mbowe na lema.tafakari
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Lini Chadema ilipinga kununua magari ya mtumba serikalini?
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Toa hoja zenye mashiko, jamaa kumbe ni mafisadi bana ! hongera zitto kwa kuwaumbua
   
 12. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIASA ZA BONGO SAFI SANA, MDUDU WA MIGOGORO AMEINGIA KWENYE CDM YETU MACHO :crying:
   
 13. b

  bansenbana Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tunaelekea kuzuri kwenye kuwatambua wanaopinga ufisadi kwa dhati na wanaotumia vita dhidi ya ufisadi ili wapate madaraka ili nao waweze kupata nafasi ya kufanya ufisadi.

  Tukumbuke aliyosema Mwadhama Pengo ''Hivi hawa wanaopiga kelele za ufisadi ni kweli kuwa wanauchukia kweli ufisadi au wanaona wivu kuwa wenzao wanakula? na wakipata nafasi hawatafanya hayo wanayoyapigia kelele?''
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unajua hadi pesa ambayo Slaa alikuwa avute kwa hii deal?

  Kiongozi mzuri ni yule ambaye anasikiliza kwanza maoni ya watu na watu wawe huru kumwaga dukuduku zao na wakishamaliza, anapima kushoto na kulia na kutoa jibu sahihi...... Ukijiingiza kwenye mabishano kama wewe kwa kuja kuwaga habari, kuijadili wewe na kumalizia wewe utafikiri unafanya mapenzi hapa, basi nampa pole sana mkeo na wanao bila kuwasahau nduguzo.

  Kuna mambo mengine ya kuleana hayafai. Mtu kapewa pesa ajenge barabara na pesa zinapotea na barabara haijajengwa, bado unataka eti "iundwe tume kutafiti......."

  Shibuda na Zitto si watu wa kuamini. Wanasahau tu kuwa nusu ya UWT wanariport kwake yeye Slaa. Kila wanachokifanya, CDM wanapata habari zao. Zitto alitaka kuingizwa kwenye uongozi wa juu wa CDM kwa kupewa hela kibao na kufanyiwa kampeni za juu ili apande kichama. CCM na kundi lao kama wewe wakaanza kufurahi kuwa sasa CDM itakuwa chini ya Zitto kama Mwenyekiti. Wangelifanikiwa, sasa hivi CCM ingelikuwa inakula kuku tu. Mpango ukagunduliwa na Zitto na Kafulila wake sijui wakapigwa STOP. Mwenzake kahamia NCCR na yeye akabaki bado apige hatua kusubri mambo yabadilike.

  Sasa alitaka kumwingiza ndugu yake Shibuda. Hawa walijichambua mapema kabisa baada ya uchaguzi kwa kujionyesha wasivyoenda na mipango ya chama. Waligoma kwenda bungeni na baadaye kubwabwaja. Shibuda akaenda kwenye mnuso wa Kikwete wakati CDM wote walitakiwa wasifike huko. Akaendeleza maneno yake mbovumbovu akifikiri kwa kufanya hivyo atakiuwa chama kumbe imekula wake. Yeye na genge lake hawatafanikiwa milele....................................

  [​IMG]

  Shibuda kwenye mnuso wa Kikwete ambao CDM waliugomea........ Hivi yeye ni masikini hata MAJI nyumbani hana hadi aje hapa.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hapa chini kama picha ya Zitto vile akihutubia wana CCM, teteteeee............ Eti Mwenyekiti wa CDM.....

  [​IMG] [​IMG]
   
 16. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hili suala la magari chakavu limemuumbua sana Slaa kama mtendaji mkuu wa chama, kwa kusema asivyotenda ! Slaa ni ndugu na mapacha 3
   
 17. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuhusu ununuzi wa magari chakavu ni uongo mkubwa sana kwani , suala la kununua magari ya chama halikuwa agenda kwani lilishapitishwa kwenye kamati kuu iliyopita ya tarehe 19 March 2011 wakati mpango kazi wa mwaka ulipopitishwa na iliamuliwa kuwa tununue magari mapya tena sio kutoka Japan wala India .

  Suala la ununuzi wa magari mapya lilijadiliwa kwenye kikao cha Bagamoyo cha last Disemba wakati mpango kazi wa mwaka unaandaliwa , huu ni uongo mwingine wa Gazeti la mwananchi na mtakumbuka waliwahi kuandika uongo wakati fulani mpaka mwanahalisi walipoweka hadharani e mail za mawasiliano walikaa kimya kwa aibu.

  Kusema kuwa Mnyika aliunga mkono hoja ya kupinga ununuzi wa magari cahakavu ni uongo kwanio wala hakuwepo kwenye kikao kwani yupo safarini nje ya nchi safari ya kamati yake ya Bunge.
   
 18. t

  thinktank Senior Member

  #18
  May 2, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala la ununuzi wa magari mapya lilijadiliwa kwenye kikao cha Bagamoyo cha last Disemba wakati mpango kazi wa mwaka unaandaliwa , huu ni uongo mwingine wa Gazeti la mwananchi na mtakumbuka waliwahi kuandika uongo wakati fulani mpaka mwanahalisi walipoweka hadharani e mail za mawasiliano walikaa kimya kwa aibu.

  Kusema kuwa Mnyika aliunga mkono hoja ya kupinga ununuzi wa magari cahakavu ni uongo kwanio wala hakuwepo kwenye kikao kwani yupo safarini nje ya nchi safari ya kamati yake ya Bunge


  Waliokuwepo kwenye kikao watupe habari za uhakika. Kama yaliyotokea ni kweli binafsi sioni ubaya wa mwananchi kuripoti kwa sababu hata Chadema si chama cha Malaika. Wana mapungufu yao kama binadamu na inapotokea udhaifu wao ukawekwa hadharani sidhani kama ni busara kulaumu chombo cha habari kinachohusika. Vinginevyo kama Chadema wanataka wasafishwe kila mara hata wanapokuwa wamechemka.
   
 19. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mtoa hoja kuna kitu sijaelewa hapo....Ufisadi uko wapi? Ni kwamba walitaka kununua magari chakavu kwa bei ya magari mapya au ilikuwaje?
   
 20. N

  Nanu JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  GeniusBrain, inaonyesha kuwa upo ndani ya CDM na una mambo mengi. Kama wewe si mnafiki hebu tupe mtiririko wote na kuonyesha jinsi ambavyo Dr. Slaa angepata TZS50million. Figure huwa hazitolewi kichwani tu, tofauti na sentensi za kawaida. Hata hivyo post yako ina walakini kwa sababu unazijibu hoja na kuzijadili peke yako. Wewe umeleta hoja, acha watu wajadili na wanaolengwa wakanushe au wanyooshe mambo. Zitto, Dr. Slaa, na wengine wengi wa CDM ni members wa jf, wacha waseme. Unless otherwise wewe ni agent wa Zitto, Shibuda, au CCM yenye lengo la kuidhoofisha CDM. Lakini nakubaliana na watoa mawazo kuwa lazima watu katika uongozi wajifunze kuelewa kutoelewana kwa minajli ya kukuza uongozi bora ndani ya Chama!
   
Loading...