Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu ya CDM 30.04.2011

Tunaelekea kuzuri kwenye kuwatambua wanaopinga ufisadi kwa dhati na wanaotumia vita dhidi ya ufisadi ili wapate madaraka ili nao waweze kupata nafasi ya kufanya ufisadi.

Tukumbuke aliyosema Mwadhama Pengo ''Hivi hawa wanaopiga kelele za ufisadi ni kweli kuwa wanauchukia kweli ufisadi au wanaona wivu kuwa wenzao wanakula? na wakipata nafasi hawatafanya hayo wanayoyapigia kelele?''

Hivi hii ni hoja ya kikaoni imejadiliwa ufisadi uko wapi hapo na magari yalonunuliwa yako wapi hapo. Wote mnaosema ufisadi hapa ni wajinga hamjui maana ya ufisadi.
 
Hivi hii ni hoja ya kikaoni imejadiliwa ufisadi uko wapi hapo na magari yalonunuliwa yako wapi hapo. Wote mnaosema ufisadi hapa ni wajinga hamjui maana ya ufisadi.

Duh, kweli nimeamini uelewa wako ndio mdogo sana, sasa sijui tukusaidiaje , ila nakushauri tu hapa JF sio sehemu yako nenda face book, huko ndio kukushauri kwangu na kukusaidia
 
Nimesahau kidogo, hebu nikumbushe ni picha zipi....

Kama ni za Zitto akihutubia kwenye mkutano wa CCM, ziko hapa: KABWE WA CHADEMA AWAHUTUBIA WANA CCM AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE WA LUDEWA

na kichwa cha habari: KABWE WA CHADEMA AWAHUTUBIA WANA CCM AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE WA LUDEWA ambaye ni wa CCM.


Sikonge

Naomba nitumie zile picha kwa inbox yangu ya PM AMA kwenye Masanilo@jamiiforums.com kuweka kumbu kumbu sawa bila Shaka lawama haziendi kwa brushing na photoshop
 
Hapa chini kama picha ya Zitto vile akihutubia wana CCM, teteteeee............ Eti Mwenyekiti wa CDM.....

1299641452download.jpg
1299641531IMG_2941.JPG

Lack of critical argumentation. Kumbe Mbowe akishikwa pabaya mnatapatapa hivi? kweli ZK ndio mpiganaji wa kweli Daima.
 
Kama hali yenyewe ni hii , nimeanza kuamini wale mapacha 3 kuwanunua hawa viongozi wa CDM ili wawatetee !
Mkubwa,sio kila mwenye macho anaona mbele,as the man said,all politician in third world country aims at getting profits!thats final,ila kwa suala la kununuliwa na mapacha watatu sina uhakika kwani waingiapo madarakani akina Slaa watapata zaidi ya hizo million ulizozitaja.
 
Alianza Tambwe Hiza kupeleka watoto kule karimje ili kutaka watu waache kujadili mambo ya msingi, saizi tena tunaona wengine wametumwa JF, najiuliza sana inakuaje mtu anatumia almost 2hrs kujibiza na watu humu JF uku hatoi data bali anatumia maneno yakufikirika???
Inamana siku hizi jf imekua uwanja wa mashindano ya blaablaa ili mshindi apatikane???
hivi inakuaje mtu anatoa mada then anamjibu almost kila mchangiaji??? kama jambo unalijua kiasi cha kuona hamna wa kukuchallenge iweje ulilete humu tulijadili???
Binafsi sioni hii kama ni mada ya kuijadili nakati aliyeileta inapingana na kila hoja bila kujali context na limitations.
 
ZK ni kichwa sana pale CDM, wakimtoa tu na chama kitabakia historia
Sio kila kichwa CDM kimesimama vilivyo,jaribu kufuatilia mienendo ya kila kiongozi wa CDM,utaona ni nani kichwa maji,fuatilia mahusiano ya Zitto na magazeti!Mkuu sio kila usomalo kwenye gazeti ni sahihi kuhusu mwanasiasa fulani.Unakumbuka kichwa cha habari cha gazeti fulani la kila siku"ZITTO AWASHA MOTO TENA CHADEMA"Unafahamu nini kilijiri mpaka gazeti likaandika vile?usijari nitakupa link!
 
Hii si sehemu ya matusi kama wengi mnavyo dhani,mmekosa ujengaji wa hoja madhubuti kwa maendeleo ya taifa,manabaki kutukanana!sio mpango,pliz stop that!
 
Mwanaume kumsifu mwanaume mwenzio na tena unafanya hivyo siku nzima, inaleta wasiwasi........

Angalia na wewe usiingie kwenye mkumbo wa SIKU NZIMA kumsifia Mwanaume mwenzio na hadi kuandika eti "Zitto kawalalia CDM na sasa anawapumulia...." umeyajuaje haya kuwa Zitto huwa analalia wanaume wengine?

Aisifiaye Mvua kweli imemnyeshea. JF sasa imeingiliwa na Mibwabwa kibao......... Ngoja niwahi IMAX
Lack of critical argumentation. Kumbe Mbowe akishikwa pabaya mnatapatapa hivi? kweli ZK ndio mpiganaji wa kweli Daima.
 
Kilichojiri kikao cha kamati kuu ya CHADEMA siku ya Jumamosi tarehe 30.04.2011
Ø Zitto apinga mpango wa ununuzi wa magari ya Chama ya mitumba kutoka India yenye thamani ya Tshs 480 milioni. Ambapo Prof. Baregu ,Dr. Mkumbo na Mnyika nao wanaunga mkono hoja hiyo
Ø Lema ataka Zitto ang’olewe kutokana na kupinga wazo hilo la ununuzi wa magari ya mitumba (chakavu), na kumshutumu kuwa anamtetea Shibuda
Ø Zitto amwambia Mbowe mpango wake wa kujenga makundi ya mtandao utakuja mletea matatizo
Ø Kamati kuu yatengua uteuzi wa Shibuda wa kukaimu uenyekiti wa chama Shinyanga , na kundi linalo mpinga Zitto kumshutumu kuwa akikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao
Ø Wakati wa mvutano huo Dr. Slaa alikuwa kimyaa na hakusema lolote
Ø Shibuda akiri kusikia taarifa hizo na anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vya maamuzi

Source : Mwananchi 02.05.2011

My note :

  1. CDM wanahubiri wasicho kitenda kwani mpango wa kununua vitu chakavu wao wanajifanya kuvipinga kumbe ndio wanataka kuvitekeleza
  2. Lema ni kimeo kwenye Chama kwani anaonekana ni mpambe wa kundi la Mbowe. Na Lema anaonekana ana visa na Shibuda, kwani Shibuda wakati wa kikao cha bagamoyo alimwambia Lema hana adabu na ataenda kumshitaki kwa wazee wa Arusha
  3. Kitendo cha Slaa kukaa kimya ni kuona aibu kwa hoja yake ya kifisadi (kama mtendaji mkuu wa chama) ya kununua magari chakavu
  4. Uamuzi wa kumvua Shibuda madaraka ni wa kukurupuka kwani ulipitia vikao halali vya chama vya shinyanga


Kumbe nako huko CHADEMA kuna vituko!!!!!! na makundi juu. hawafiki mbali hawaaaaa. Kwanza wajue Shibuda ni sisiem
 
Mwanaume kumsifu mwanaume mwenzio na tena unafanya hivyo siku nzima, inaleta wasiwasi........

Angalia na wewe usiingie kwenye mkumbo wa SIKU NZIMA kumsifia Mwanaume mwenzio na hadi kuandika eti "Zitto kawalalia CDM na sasa anawapumulia...." umeyajuaje haya kuwa Zitto huwa analalia wanaume wengine?

Aisifiaye Mvua kweli imemnyeshea. JF sasa imeingiliwa na Mibwabwa kibao......... Ngoja niwahi IMAX

Kumbe kulaliwa na ZK NI vibaya , basi jivue magamba !:israel::israel::israel::israel:
 
Kwani haya magari yamechakaa kiasi, gari kama ni grade 5 kwa hali ya uchumi ya Tanzania ndi yanayonunuliwa na watanzania wengi, Na tofauti yake na magari mapya ni ndogo sana. Badala ya kununua gari mbili, wanaweza kununua gari 20 na zikasaidia kampeni hadi zaidi ya 2015.

Do a proper evaluation, sio blabla. Chakavu is a relative term.:help:

Umeeleza vizuri kuliko nilivyokuwa nataka kuelezea. Nimeshakugongea "laiki".
 
Haya sasa.............
Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.

Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.

Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.

Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.
 
Umeeleza vizuri kuliko nilivyokuwa nataka kuelezea. Nimeshakugongea "laiki".

Acheni kujitetea nyie kama chama mbadala kinacho tarajia (na huendi isiwe hivyo mpaka yesu ashuke) kuchukua dola, ni vizuri kuonyesha maneno yenu kwa vitendo. Na ndio maana Prof Baregu aliwasisitizia hilo ndani ya kikao
 
Hivi ununuzi wa magari chakavu ni Ufisadi maana hata mimi ninalo gari chakavu? Au Ufisadi ni vita baina ya Lema na Zitto..Jamani hata siuelewi hii mada inahusu vitu gani haswa kwani asilimia kubwa ya watanzania hununua vitu chakavu hadi nguo wanazovaa acha magari..
 
Hivi ununuzi wa magari chakavu ni Ufisadi maana hata mimi ninalo gari chakavu? Au Ufisadi ni vita baina ya Lema na Zitto..Jamani hata siuelewi hii mada inahusu vitu gani haswa kwani asilimia kubwa ya watanzania hununua vitu chakavu hadi nguo wanazovaa acha magari..

Huwezi elewa kwani umeisha ziba masikio na macho. Tofautisha ununuzi wa gari lako na mkeo, na wa chama cha siasa. Kama chama cha siasa inabidi uonyeshe kwa vitendo kile mnacho hubiri, sio nyie na wabunge wenu mnahubiri vitu chakavu visinunuliwe serikalini na kwenye halmashauri kwani kufanya hivyo mtaruhusu mwanya wa ufisadi ? sasa nyie mnataka kununua vitu chakavu huo kwenu sio ufisadi ? au ufisadi ni kwa serikali tu ? jivue gamba !
 
Huwezi elewa kwani umeisha ziba masikio na macho. Tofautisha ununuzi wa gari lako na mkeo, na wa chama cha siasa. Kama chama cha siasa inabidi uonyeshe kwa vitendo kile mnacho hubiri, sio nyie na wabunge wenu mnahubiri vitu chakavu visinunuliwe serikalini na kwenye halmashauri kwani kufanya hivyo mtaruhusu mwanya wa ufisadi ? sasa nyie mnataka kununua vitu chakavu huo kwenu sio ufisadi ? au ufisadi ni kwa serikali tu ? jivue gamba !
Mkuu hili sio kweli kwani masharti ya ununuzi wa vifaa chakavu ni katiba ya Taifa, haizuii vyombo vingine nje ya serikali kutofanya hivyo. Na hakuna mahala popote ktk katiba ya chama inazuia chama kutonunua vitu chakavu iwe ya CCM,CUF,TLP au CDM. nenda maofisi mwao utakuta vitu chakavu na mkuu wangu unajikuna pale unapoweza.

Swala la Zitto kupinga ununuzi huo ni wazo lake kupinga ununuzi huo na haihusiani na sababu za kitaifa kutonunua vitu chakavu, ila ni ushauri ambao hutokea ktk vikao vyovyote vile. Soma vizuri utaona kuna wajumbe wamepinga ununuzi huo hivyo ni ktk majadiliano..Hata mimi naweza pinga magari kununuliwa toka India, haina maana maamuzi ya CDM kununua magari India ni Ufisadi bali napinga wazo hilo unless nitaonyesha ufisadi umefanyika vipi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom