Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

wewe kama mdogo wake na Mbowe aliyeko marekani nini? Nasikia anajiuza huko

nipo tanz_mainland we gamba,marekani ama ulaya mi nimekuwa mpagazi kama Chris Lukosi,ZeMarcopolo..box kama we mwanaume bebea kariakoo.
 
Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa bungeni na ndugai wamenguruma katika manispaa ya Iringa wakiongozwa na katibu mkuu wa chama Dr.Slaa ambaye wakati wote wananchi walikuwa wakimuita rais wao wa moyoni. Kikubwa ambacho kimenistaajabisha ni maerefu ya watu walioacha kazi zao na kuja kusikiliza nondo zilizowasilishwa na wabunge wa CHADEMA. Mkutano ulikuwa wa amani kabisa huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi na usalama kila eneo.Jambo kubwa ambalo watu wamebaki wanashangaa ni ustaarabu wa viongozi na wananchi kwa ujumla maana hakuna aliyeonekana kumbughudhi mwenzie licha ya msongamano mkubwa uliokuwepo hata kama polisi wasingekuwepo.

Katika mkutano huo mambo mengi yamejadiliwa hususani yafuatayo;

1. Suala la mabadiliko ya katiba; waheshimiwa wote hasa Mh.John Mnyika ameelezea kwa nini CHADEMA wanakusudia kujitoa kwenye mchakato huo iwapo tume ya mabadiliko ya katiba mpya isiporudia zoezi la kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba huko mawilayani ambayo yamegubikwa na ufisadi.

2.Kufukuzwa kwa wabunge bungeni; waheshimiwa wabunge wamewaeleza wananchi kile kilichotokea bungeni kuwa ni kutokana na kiti cha spika kutotenda haki na kuwa na upendeleo kwa chama tawala na serikali kwa ujumla, wamewahoji wananchi kwamba ni yupi alitakiwa kutolewa bungeni kati ya mbunge wa ccm aliyeporomosha tusi la nguoni na la aibu kabisa na mbunge wa CHADEMA aliyeomba mwongozo! Dr.Slaa akawambia wabunge wake mbele ya wananchi kuwa kamwe wasirudi nyuma bali huo uwe mwanzo mpaka hapo chama tawala na serikali watakapotenda haki.

3. Kesi ya Lwakatare pia imeongelewa kwa umakini mkubwa sana kiasi kwamba wananchi wengi wameonekana kukerwa na uanzishwaji wa kesi hiyo huku wengi wakivituhumu vyombo vya usalama na serikali kuhusika kwa vitendo mbalimbali vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji bila kuonesha juhudi za makusudi kukomesha vitendo hivyo.

4. Hali ngumu ya maisha pia imekuwa ni gumzo kwa wananchi wengi huku wananchi hao wakiwa na shauku kubwa kuwa chama cha CHADEMA 2015 ndicho chama tawala na wala si vinginevyo.Katika hali isiyo ya kawaida maneno ya Dr.Slaa yalioneka kuwakuna hata maaskari polisi waliokuwa katika mkutano huo pale aliposema kuwa wanatumiwa na wakubwa zao wakati wao wakiendelea kusota katika dimbwi la umaskini na kuwambia wasupport CHADEMA uli kiweze kuwakomboa.Maaskari wengi tuliokuwa nao wamefurahishwa na maneno hayo huku wakisema ni ukweli mtupu Dr.anasema.

Wananachi wameaswa kuwa makini katika chaguzi za 2014 kuhakikisha CHADEMA kinapata ushindi mkubwa ili kuweza kuwakomboa watanzania na hali ngumu ya maisha waliyonayo kwa hivi sasa, kwamba raslimali za taifa zinawanufaisha wachache.Dr.Slaa amekuwa mwalimu siku ya leo kwa kuanza kuwaelimisha wananchi ili waweze kujitambua kulinda raslimali zao na kuhakikisha kuwa zinatumika kwa manufaa yao na siyo ya viongozi wa juu. Vile amewaomba wananchi kuhakikisha 2015 CHADEMA ndicho chama kitakachoongoza taifa hili kwa kukipa kura za kishindo kwa upande wa urais, wabunge na madiwani.

Mh.Wenje amewambia wananchi kuwa ccm wanamtegema Lusinde kuwashauri namna ya kuimarisha sarafu ya sh. yetu halafu yeye anawashauri eti waweke picha za Nyerere na Karume sh.itaimarika, mara baada ya msemo huo wananchi waliangua kicheko kikubwa na cha kuwakejeri wabunge wa ccm.

MBUNGE Wa Iringa Mjini MCHUNGAJI PETER MSIGWA amedhihirisha kuwa yeye ni jembe linalokata pande zote kwa hoja makini na kuonekana kuwa mtu mwenye msimamo mkali na asiyeyumbishwa na mtu yeyote; ameorodhesha baadhi ya mambo ambayo amefanikiwa kuyafanya jimboni ikiwa ni pamoja na taa za umeme mjini, barabara, maji na huduma za kielimu.

Katika mkutano huu wananchi kwa hiari yao kabisa wamechanga zaidi ya laki tisa(900,000) kwa ajili ya wabunge wao kuendelea na mikutano sehemu nyingine.

CHADEMA kinapendwa sana kuliko maelezo, vijana wa ccm wengi wao leo wamejificha kwenye vibanda vyao huku wakijisemea kuwa hawajawahi kufanya mkuatano ukawa mkubwa vile hata angekuja rais wao.

Kwa ushahidi zaidi angalia picha; ikikukera tafuta sumu ya panya unywe tutakupa maziwa ufufuke lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, huwezi kuzima upendo wa wananchi walionao kwa CHADEMA kwa kufukuza wabunge wao bungeni hata wangefukuzwa wote hawa jamaa wanatisha huku mitaani nawambia, vijana wa ccm siku hizi yale mashati wanayaficha kwenye mabegi maana fedheha kuyaonesha hadharani.
 

Attachments

  • UMATI 6.jpg
    UMATI 6.jpg
    42.7 KB · Views: 775
  • UMATI HUO 1.jpg
    UMATI HUO 1.jpg
    29.9 KB · Views: 785
  • umati 2.jpg
    umati 2.jpg
    30.5 KB · Views: 206
  • UMATI 5.jpg
    UMATI 5.jpg
    35.8 KB · Views: 232
  • CDM 1.jpg
    CDM 1.jpg
    37.2 KB · Views: 282
  • VJN WAKIJITOLEA KUSUKUMA GARI.jpg
    VJN WAKIJITOLEA KUSUKUMA GARI.jpg
    29.1 KB · Views: 281
Nimefurahishwa na harakati hizi, mkutano umeisha bila kumtukana mtu.Hii ndiyo tafsiri sahihi ya demokrasia na uhuru wa kukutana na kutoa maoni.Hongereni CHADEMA!
 
CCM wachovu kweli, majungu tu, sasa wamesikia wamesafishwa na CCM wanaamua kwenda kujikosha

Kila mtu analitambua hilo. Kuna mdau alidokeza kwamba wewe thatha uko Chadema kiroho na kiakili na ccm upo kimwili tu sasa nimeanza kuyamini maneno yake. Unaona ulivyoandika ukweli wa moyo wako? siku ukichoka kutumika karibu nyumbani tutakupokea tu hat kama umeendekeza njaa na kuishia kuwatukana ndugu zako...
 
Last edited by a moderator:
Wee vipi tena
Mbona unatokwa povu?

Tunasubiri kontena la mitumba kutok UK mwezi June. Unadhani utatuamia malori mangapi na ubwabwa magunia mangapi na wanamuziki wangapi kuujaza huo uwanja? ili tuanze maandalizi mapema...
 
Yaani naona aliyetoa kibali cha kufanya mkutano hapo Iringa ana wasiwasi na kibarua chake. Kilichofanyika Iringa leo ni kufuru!!
 
Huu umati nafananisha na Ile niliyo kuwa naiona kwenye Kampeni za Uraisi nchini kenya
 
mkuu ni kweli nilikuwepo pale wakati mnyika wenje raisi mawalajiwa sugu msigwa wakieleza ukweli kuonyesha kuungwa mkono na wananchi wa iringa walichangiwa papohapo sh 900,000 magamba kunyweni sumu tu la sivyo njoon cdm
 
vp mkuu,nasikia maumivu ya kichwa chako yameanza tena taratibu baada ya kuona town kwenu iringa Magwanda yanashine..eti unataka ubunge,mtajaa watukanaji bungeni.

Chris Lukosi, Warundiwana msemo unaosema ‘mtu anayeshibahakosei hadithi’. Ndiyo maana ww hukosei hukosei kusema ujinga. Watu hawa wanakwendamkutano wa chadema kwa sababu ya kupata tumaini na mwanga mpya wa maisha. Hawaendi kwa sababu ya kusikiliza midundo ya miziki kamailivyokuwa juzi kwa liccm lako Moro.Hawaendi kwa sababu ya usafiri chee,hawaendi kwa sababu ya kupata fulana, kofia wala chakula. Hiki ndo unachotakiwakuelewa!! Kwa ujinga wako Chris unashindwa kujua kuwa enzi za Mrema, watu walikuwa na imani na mtu mmojaanayeitwa Augustin Mrema na sio chama chake NCCR Mageuzi. Ungalimtoa Mrema,chama kile kisingepata watu unaowataja leo hii (kulingana na akili yako). Leo hii watu wanashabikia Chadema na serazake! Hawamshabiki viongozi pekee! Kwamba akikosekana kiongozi mmoja wa juu watubado tutakusanyika kwenye mikutano... kwa sababu ya sera za chama. Namaza kwa kusema ashukuriwe Mungu aliyekutenga wewe harakazaidi toka kwa kwa familiya ya wapenda ukombozi wa pili wa Tanzania. Bado haijaniingia akilinikuona kuwa mtu kama wewe ulipata mwanya wa kuaminiwa na watu na kukupa uongozi.Nafurahi kuwa Mungu aliweza kuliona haraka hilo na akakutenga mbali na tumainimpya! Lukosi huna huruma na watanzaniawanaoteseka kwa sababu ya utawala mbovu na wakifisadi wa ccm na serikali yake. Kwakuwa ww unaendelea kula kuku zinazovunda kwenye friji za Uingereza, ndo maanahukosei kutoa maneno ya kejeli kwa watanzania wanaotaka kuijenga upya nchi yao.
 
There are currently 1646 users browsing this thread. (84 members and 1562 guests)
 
Ni ngumu mtu kuweza kuchangia pesa chama halafu asipige kura! Kwa maana nyingie hizo 900,000 ni kura nyingi sana.
 
Back
Top Bottom