Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA - Iringa

unafikiri ukiwaita watu kenge ukweli utajitenga? Mkuu NGuvu aliyokuwa nayo mrema huwezi kulinganisha na hii ya chama cha wachagga, kile kilikuwa chama kilichosheheni watu kona zote za TAnzania.

jiulize idadi ya Watu mwaka 1995 linganisha na yasasa...
 
Chama cha wachaga Iringa mnataka nini??hata Mrema alijaza watu,katibu kawambia nyie sio wa kwanza!
Eti walikwenda kuishtaki CCM , wananchi tunaona ni mwendawazimu pekee anaweza kukubaliana na namna kodi za wananchi zinavyochezewa kwa kufanya vurugu ndani ya bunge?
 
Ubarikiwe sana mohamed Mtoi kwa updates hizi!, CCM kazi kwenu endeleeni kutufukuza bungeni sisi tutawafukuza mpaka Uraia. Nyie subirini.

Asante mkuu.

Pamoja tutashinda hila na ghiliba zao.

"Kuendelea kuikumbatia ccm ni maafa" Dr slaa.
 
Leo tuna muda wa kufuatilia mkutano wa chadema kwa sababu hakuna mktano wa CCM Morogoro...
 
'' Tanzania yatajwa kuwa ndiyo nchi pekee ambayo imekithiri kwa Umaskini hapa Afrika Mashariki,... Ingawa Madini ya Tanzanite, Dhahabu, Almasi, Gesi, Mafuta, Maziwa, milima, Bahari,... Rwanda Yapaa Kiuchumi.
 
Ndio maana wenye akili zao wanajua CHADEMA haiwezi kusimama peke yake bila kuegemea katika muhimili wa dini.

Takwimu za matokeo ya 2010 zinaonyesha a big jump ya wabunge by 336% kutoka 2005! What a propaganda.

Ila hii sera ina mwisho wake wake ambao huenda usiwe mzuri.

Practice politics, dini tuwaachie wenyewe!
Moja kati ya jambo lililonifurahisha katika
Mkutano wa juzi wa ccm ni kuachana na maneno haya ya kipumbavu, naamini wamegundua hayajawasaidia kama walivyodhani, hata nape sikumsikia akiongelea ukabila kama alivyozowea, tushindane kwa hoja za msingi haya mengine ni sawa na uhaini kwa taifa letu, au mmeanza kukata tamaa?
 
UMATI MKUBWA WA KISIASA KAMA HUU KWA CCM SIKU HIZI NI GHARAMA KUBWA SAWA NA BEI YA BASI MOJA AINA YA 'MACOPOLO PARADISO' ILA KWA CDM YOTE NI HIARI TU

Wakuu, umati mkubwa kama huu unaojihiari tu wenyewe kwenda kuwasikiliza Makamanda wetu wa uhakika CHADEMA, kama ingalikua ni kwa upande wa watani zetu Wa-Kijani lazima

(1) ingewagharimu hadi Tsh 53,000,000/- kuwakusanya watu kwa kuwalipa fedha na kuwasafirisha kwa malori,

(2) Nape na Mzee wa Tembo wangehitaji kitu kama mikutano ya ndani zaidi ya 60 ili kubembeleza watu wajitokeze,

(3) Wa-Kijani wangehitaji ziara ya wiki 2 mfululizo kutembelea si chini ya vijiji 50 Iringa ili siku ya mkutano waweze kupata japo robo ya watu kama tunaowaona katika umati hapo chini lakini watoto wa shule za msingi wakiwa ndio wengi zaidi ambao mara nyigi hujitokeza kwenda kujionea wenyewe kwamba 'FISADI HUWA NI MTU WA AINA GANI VILE',

(4) Kwenye mkutano mzito kama huu wa leo, laiti kama ingalikua ni kwa wale watani wetu Wa-Kijani, lazima kumbi mbali mbali nchini zingekua zimebaki zikiwa zimenuna kwa kuwa tu wasanii lukuki wamekusanywa kwenda kubembelezea umati wa kisiasa wasiondoke hata kama sera ya siku ni kuporomoshea CHADEMA matusi mazito mazito kama yale ya 'Waziri Mkuu Muandaliwa wa CCM hapo 2050 - Mhe Serukamba et al'.

Jamani, acheni CHADEMA tuendelee kupendwa kwa hiari ya wananchi wenyewe bil ya kuwapa hata senti tano kwa kuwa wanafahamu fika nini maana ya 'Vita Dhidi ya Ufisadi - CCM' na ugumu wake wanaoupata makanda wetu kila siku kwa ajili ya umma wa Tanzania kupata ahueni baada ya kukiondoa CCM pale Magogoni.

CDM vita dhidi ya ufisadi bungeni mbeeeeele kama tai mpaka kielewe na kusaidi kurejeshea ndugu zetu Wa-Maasai ardhi ya kule Loliondo kabla hajachelewa!!!!!!




 
Uko kusakana kuwe kwa amani mkawii kuja na mikoba ya dentist au mambo ya pedicure manicure.

Khaa..!! hadi nyie wenye chama chenu mnaogopa..!?? kweli nchemba balaa
 
====== Picha =======
attachment.php


attachment.php

Nimeipenda simplicity ya Chadema. Hapo Diamond akija ata perform wapi?
 
Back
Top Bottom